Hawa ni wasanii waliohit na ngoma moja na kupotea

kende

JF-Expert Member
Dec 2, 2013
3,527
1,664
Kuna wasanii wa Bongo Fleva waliofanikiwa kuhit sana na kujitambulisha vyema but wakashindwa kumaintain either kwa kutoa nyimbo zenye ubora unaoendana na uliowatambulisha or wakaingia mitini kabisa hawakusikika tena na nyimbo nyingine, kwa lugha nyingine tunaweza sema 'waliotea'. Hawa ni baadhi;

1. ZAY B-----> Baada ya kusumbua sana na ngoma yake ya GADO (Original na Remix) akapotea mazima, kuna kipindi hivi karibuni alikuwa anajaribu kurudi but wimbo wake ulifeli kama zilivyofeli nyingine alizoachia baada ya GADO.

2. PIG BLACK-----> Mchizi alisumbua sana mwanzoni mwa miaka ya 2000 na ngoma yake ya 'NINI MNATAKA MAZEE' wenye moja kati ya beat bora kabisa za Majani, alitoa ngoma nyingine kama 'Nisikilize' aliomshirikisha Blue na nyingine kadhaa but hazikufanikiwa kukaribia kiwango cha wimbo uliomtambulisha.

3. K-SAL-----> Alitoa wimbo unaitwa 'MWANA MKIWA' akimshirikisha Feruzi kwenye chorus, ulikuwa mkali na ulihit lakini baada yapo sijui alipotelea wapi.

4. RAH P----> Alikuja kwa fujo na wimbo wake 'HAYAKUHUSU' yenye video kali kwa kipindi hicho, baada ya hapo sijui nini kilimpata.

5. RADO-----> Huyu mshkaji alikuja kwa mbwembwe za bifu na Fid Q, aliachia ngoma kali sana ya Hiphop 'USIULIZE' ilisumbua si kidogo. Then akaachia ngoma ya pili 'WEWE', haikufanikiwa kubamba, akapotea mazima.

6. H-MBIZO-----> Alibamba na ngoma yake ya 'MCHUMBA(NILONGE NISILONGE)' then hakusikika tena.

7. J.I (MTOTO WA NZEGA)------> Jamaa alisumbua sana na ngoma yake ya 'KIDATO KIMOJA' ambapo ilikuwa inabamba both kwenye Redio na Tv, baada ya hapo sijui nini kilimkuta.

8. TOP C------> Alikuja na ngoma iliyohit sana 'SABABU YA ULOFA', ikahisiwa jamaa atakava vzuri nafasi ya Diamond aliyoiacha Sharobaro rec baada ya kujitoa na hivyo kuendelea kuisimamisha vizuri lakini waapi, naye akarudi alipotoka.

9. ADILI (CHAPAKAZI)-----> Huyu jamaa kaanza game kitambo ila wimbo wake wa 'PEKE YANGU' ndo ulifanikiwa kumtambulisha vyema, na baada ya hapo hakufanikiwa tena kuachia ngoma level hizo.

10. IMAMU ABBAS-----> Baada ya kutoka na bonge la ngoma linaitwa 'BILA SANAA' akatoweka kwenye game. Sijui aliotea

#Hawa ndo niliowakumbuka, unaweza ongezea niliowasahau
 
Alicom alikuwa na hits mbili tatu
Tatizo la Alicom ni kwamba Selina ilifunika kupita kiasi to the point, ilimuwea vigumu sana kutengeneza ngoma nyingine ya kuifunika Selina! Katika list Uswahilini Matola nao walisumbua, na wakapotea kama walivyoingia!!
 
Ni kweli uko sahihi jamaa huyo wa Zanzibar alishindwa kumaintain but kwa mtazamo wangu Moyo ulikuwa mkali kuliko Selina. Hao Uswahilini Matola dah wamepotea hadi nimewasahau, vipi Balozi Dola Soul hafai kukaa hapa?
 
Kuna hawa pia:
1/ Maliki, mshikaji kutoka Buguruni line POLICE - Nampenda
2. Kaki P ama Kali Popote, mshikaji kutoka VUNGUNGUTI, ngoma ilikuwa KAA CHINI
3. HAWA HATA NGOMA ZAO SIKUMBUKI:
Caz T
Dan Mcmamo
Mnyalu
Somo na Dojo
Getto boys na albam 1
Ras lion
Oten japo karudi na Kimbunga, bado hajakaa sawa
 
Hapo Maliki tu ndo uko sawa alitoka na hiyo ngoma aliyomshirikisha qchief akapotea. Kali P alikuwa na ngoma nyingine matata 'IMEKAA VIBAYA', hao wengine hujawatendea haki walikuwa na ngoma kubao zilizohit
 
Hapa kama sijakuelewa vizuri hivi. ...
2.Kali P ulikua unamaanisha ile hit song yake ya IMEKAA VIBAYA?
3.Caz T ft Sarah- Nakuhitaji
~Mnyalu mbona alitoa hits nyingi tu? Kama Nampenda nani? Sitobadilika n.k
~Mandojo & Domokaya -Nikupe nini?
Dah...umenikumbusha mbali sana.
 
Ni kweli uko sahihi jamaa huyo wa Zanzibar alishindwa kumaintain but kwa mtazamo wangu Moyo ulikuwa mkali kuliko Selina. Hao Uswahilini Matola dah wamepotea hadi nimewasahau, vipi Balozi Dola Soul hafai kukaa hapa?
Balozi amepitia stages mbili... kwanza akiwa kwenye kundi la DPT na pili kama soul artist! Lakini baada ya kutoa ngoma ya Kwenye Chart kama soul artist, sidhani kama alisikika tena manake ilikuwa kama amejichulia na mistari yake "Wengi wao walikuwepo, sasa hivi wapo wapi, wapo wapi... Balozi bado nipo, ninapanda kwenye chart, kwenye chart...!" Ikawa ndo mwisho wake... ckumbuki ilitangulia hii ngoma au ile featuring ya Mr. II.... manake hizo ndo ngoma zake mbili za mwisho kusikika!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom