Hawa ndio wawekezaji wetu wakubwa

kutoka uchina hadi kusukuma mabox kariakoo.je watanzania hatuwezi kazi hii?

si swala la kusukuma hapa ukweli ni kwamba watanzania tunapenda ukubwa (uboss) na hata ukiona hapo mtanzania unashangaa kuwa mchina asingeweza kusukuma, tujifunze na tubadirike. Na si swala la siasa ya hovyo hapa twende tukachape kazi bila kuchagua hakuna kazi isiyolipa, kumejitokeza zana ya kuona hili ongezeko la wachina linatokana na urahisi wa kukwepa kodi kutokana na mfumo wetu mbovu wa kukusanya kitu ambacho ni uongo mtupu, wenzetu wameona huku kuna fursa kwani hata vyakula vyao sisi tunaona ni vya hovyo wao wanajipatia vitoeo hivyo kwetu bure kabisa kama vyura, nyama za punda, nyoka na vinyonga na kupata 100% saving, sisi tungali tukiagiza nyama za kopo, juice, maua, kahawa, soya, mbaya zaidi mpaka sindano na mitego ya panya kutoka south africa. Tumechagua ushalobalo na hii ndiyo kiboko tunachopata.
 
Huu ni utandawazi opportunities. hata wewe ukiwa na pesa yako ya kutosha unaweza kwenda china ,usa, uk na kokote duniani kufanya biashara au kuwekeza. unaweza kwenda uza hata mishikaki, chips, vinyago, icecream, khanga, batiki, ubuyu ili mradi ufuate sheria. Trade liberalization inafanya kazi.
Na wewe pia ni Great Thinker!
 
Back
Top Bottom