Hawa ndio wasomi wetu: IFM

kufanya generalization katika ishu kama hii ni uvivu na ufinyu wa kufikiri bwana nguvumali, si kweli kwamba ifm/cbe hakuna wanafunzi smart na walio na akili just be specific to those who cheated, usihukumu na wasio na makosa. Hivi ni vyuo vilivyo makini na vinaongozwa na watu makini na wengi wao wametoka katika vyuo bora na vyenye sifa kama udsm,mzumbe na hata nje ya nchi,

kuwahukumu jamii yote kuwa ni mbovu ni makosa jaribu kufikiri mheshimiwa.

Sawa kabisa mkuu,samaki mmoja akioza si wote wameoza,lakini je kama katika kumi haupati aliye mzima kiasi cha katika mia unapata watatu.What do you conclude.Yaani kama watu watatu wamekamatwa wanafanyiwa mitihani,what about the simple cheating like kuingia na madesa kwenye pepa na kadhalika.Wajaribu kuongeza umakini katika usimamizi wa mitihani na ukali,kama katika hali hii bado chuo kinaweza kutoa wasomi wazuri kama unavyosema basi nadhani wasimamizi wakiwa wakali kidogo tuu kitakuwa bora afrika mashariki na kati katika kada ya wasomi inayotoa.
 
wewe huijui IFM vyema, hiki niuchuo ambacho huwezi kucheat ukakamatwa ukaachwa, huyo mtu anaetajwa kama Andendekisye Mark kwa sasa ni msajili wa chuo, aliwahi kumkamata mkewe katika sup,
tofauti na vyuo vingine IFM ukikamatwa jamii nzima hutaarifiwa , na kwa hilo huwa somo kwa wengine wote.
vyuo vingine hii hubaki kuwa siri ya ndani.
Ukitaka kujua IFM NI NOMA NENDA PALE BOARD YA UHASIBU KAULIZE NI NANI ALIENGOZA MWAKA JANA KWENYE cpa, Huyu anaitwa Hansigar, mwanafunzi bora wa jumla katika mwaka wa masomo uliopita, Hongera Andendekisye kwa kumkamata huyo mdanganyaji wa mitihani.

Kipindi ambacho alimkamata "Mkewe" walikuwa tayari wameoana au?
 
Tukumbuke pia Jumuiya ya afrika masharika hiyooo iko njiani.Tutauweza ushindani kwa staili hii.

Vyuo vya Tanzania vina hali mbaya sana.Mfumo wa elimu usipobadilika ni hatari kubwa.Hapo UDSM wanasajili wanafunzi wengi kuliko hata uwezo wake katika maswala ya miundombinu na mambo mengine ya muhimu.Profesa atamudu vipi wingi wa wanafunzi unaozidi uwezo wake.Hata madarasa ya shida watu wanasoma wamesimama nje.Mfano mzuri ni ile programu ya Zain inaonyeshwa na ITV ya kuvishindanisha vyuo vya East Africa.Kwa kweli vyuo vyetu vinatia aibu hadi unasikia uchungu.
 
Hali vyuoni ni mbaya kwani vijana wanaingia na hawana sifa yaani hata kupata nafasi alitumia janja ya nyani kula hindi bichi aidha kwa wazazi kufahamiana na viongozi wa chuo,kuhonga na kadhalika.Sasa hapo wachache ndio wanasoma na elimu wanayoipata inalifaa taifa baadae.
Hali ni mbaya sana sio IFM pekee na vyuo vingine vingi tu,mtu hana msingi mzuri wa hesabu anang'ang'ania uhasibu kwa sifa tu ili na mie nije kuwa mkaguzi wa mahesabu!Kama hesabu au masomo ya Sayansi ulishindwa waachie wenye uwezo wao wasome.Matokeo yake ndo hayo unatia aibu unahonga,unatumia watahaniwa feki kukufanyia mtihani bila kusahau shahada za chupi!
Jamani wasimamizi wa mitihani na wadahili muwe makini TAIFA LETU LINAANGAMIA NA VIHIYO.
Tuwe wakweli kwenye perfomances zetu ili taifa lipate wataalamu yaani watu ni feki kuanzia nywele,akili,uso,maungo,vyakula hadi tabia.WADAU HIKI NI KILIO CHA TAIFA.:eek:
 
wewe huijui IFM vyema, hiki niuchuo ambacho huwezi kucheat ukakamatwa ukaachwa, huyo mtu anaetajwa kama Andendekisye Mark kwa sasa ni msajili wa chuo, aliwahi kumkamata mkewe katika sup,
tofauti na vyuo vingine IFM ukikamatwa jamii nzima hutaarifiwa , na kwa hilo huwa somo kwa wengine wote.
vyuo vingine hii hubaki kuwa siri ya ndani.
Ukitaka kujua IFM NI NOMA NENDA PALE BOARD YA UHASIBU KAULIZE NI NANI ALIENGOZA MWAKA JANA KWENYE cpa, Huyu anaitwa Hansigar, mwanafunzi bora wa jumla katika mwaka wa masomo uliopita, Hongera Andendekisye kwa kumkamata huyo mdanganyaji wa mitihani.
mzee na wewe umo nini? maana utetezi huu hauna mantiki. hivi kumkamata mkewe kunatusibitishia kuwa ifm ni safi? anastahili hongera wakati ni sehemu ya kazi yake? vipi kuongoza cpa hakutuondolei shaka juu ya ubora wa wanafunzi ifm. je unauhakika gani kuwa yeye hakufanyiwa mtihani? Kamchezo haka kamezoeleka ukweli ni kwamba hata huyu aliyekamatwa angefanikiwa basi wangesema huyu ni mkali wa huko ifm.kumbe si lolote wala chochote. hata wanafunzi wenyewe wanakili ifm kumejaa tumchezo. Pia kazini tunawaona wamekosa kujiamini na kazi wafanyazo, kila kitu lazima aulize hata vile ambavyo unategemea mtu kama huyu inatakiwa awe anajua. Hivi admission office kweli ipo makini? mtu asiyejua kukokotoa ameingiaje huko kwenye mahesabu. Hivi kutarifu jamii ni kazi ya chuo au mapaparazi? na kuwa inabaki kuwa siri, unaweza ukatuwekea evidence ili tuamini. tunaifahamu vizuri ifm lakini simaanishi kila anayemaliza ifm basi ndio katumia kamchezo. no kuna watu safi pia.
 
kama kuna mwanafunzi yeyote wa vyuo vingine mnasoma jf anaelewa fika mzingira ya ifm kuwa ni magumu sana nasema magumu kutokana na jinsi system ya pale ilivyo.....wanafunzi wanafeli sana kwa kuwa wanakaza sana mitihani....haya yanayotokea ni namna tu ya kujihami kutokana na hali hiyo........kuna wale wanaoitwa inservice huwa wanafeli mpaka unaona huruma kwani chuo hakina huruma na hawajari umetoka wapi.......sifagirii wanafunzi kucheat ila wanafanya hivyo kwa kuwa hali pale ni ngumu sana hivyo wanataka kufaulu kwa vyovyote vile.....hakuna asiyejua kuwa ifm is a very marketable college in the country wanafunzi wa ifm wanafanya vizuri sana katika ajira zao.......
 
Shule ya bongo ni ngumu bwana ,vitha ni vitha mura!!!
Hii umeitoa wapi? Labda kuna kozi ambazo wewe unamaanisha? Au la ni yale maneno ya mtaani. Nimesoma Tanzania na nje ya nchi. Loh elimu yetu bado tupo nyuma saana ukienda kwenye vyuo ambavyo viko juu unatapatapa mpaka baada ya muda ndio unajiadjust. Ni wanafunzi wangapi wa Tanzania wanaweza kuandika wanachotaka kusema kikaeleweka bila kumuita atoe maelezo ya nini alitaka kusema? Na hao wanaoandika, maandishi yao yanakuwa formal kiasi gani? Hii inathibitishwa hata na wahadhiri wangapi wanaandika kazi zao kwenye machapisho ya kimataifa?
 
kufanya generalization katika ishu kama hii ni uvivu na ufinyu wa kufikiri bwana nguvumali, si kweli kwamba ifm/cbe hakuna wanafunzi smart na walio na akili just be specific to those who cheated, usihukumu na wasio na makosa. Hivi ni vyuo vilivyo makini na vinaongozwa na watu makini na wengi wao wametoka katika vyuo bora na vyenye sifa kama udsm,mzumbe na hata nje ya nchi,

kuwahukumu jamii yote kuwa ni mbovu ni makosa jaribu kufikiri mheshimiwa.
Yah naungana na wewe kwahili la generalisation. Binafsi nimewahi kufanya kazi huko UDSM na IFM kwa vipindi tofauti. Matatizo ya vyuo hivi yanatofautiana. Tuwe wakweli, UDSM inachukua wanafunzi wengi ambao ni smart kuliko IFM, wakati IFM hawapo smart km UDSM kwa kiasi kikubwa. Lakini judgement ya intake inaweza kuwa si fair kama hatujaangalia kuanzia smartness ilivyopatikana pia (hili naliacha si mada). Ukifika IFM unakutana na walimu wengi waliosoma UDSM na wengine wanaofundisha UDSM wapo IFM kama parttimers. Kwahiyo bado wanafunzi hawa wanafundishwa almost vitu vinavyofanana. Labda tu wa IFM wanabahati moja ya ziada kwamba walimu wao wengi wamesoma nje ya nchi kwenye vyuo bora kuliko hata UDSM kwahiyo wanapata exposure fulani. Lingine labda IFM wao seminars/tutorials zao zipo serious si za kubabaisha kama business school ya UDSM huko FASS (school ya nini sijui kuna afadhali kwingine sina hakika).
Sasa kasheshe kwenye mitihani. UDSM wanacheat inawezekana kabisa kuliko vyuo vingine. Unakuta Nkruma Hall inawalimu watatu wanafunzi 300 unategemea nini? IFM ni tofauti wao roughly 40 students walimu 2 ndio maana wanakamatwa kwa urahisi. Lakini all in all, kucheat ni suala la kimfumo si la chuo husika.
 
kama kuna mwanafunzi yeyote wa vyuo vingine mnasoma jf anaelewa fika mzingira ya ifm kuwa ni magumu sana nasema magumu kutokana na jinsi system ya pale ilivyo.....wanafunzi wanafeli sana kwa kuwa wanakaza sana mitihani....haya yanayotokea ni namna tu ya kujihami kutokana na hali hiyo........kuna wale wanaoitwa inservice huwa wanafeli mpaka unaona huruma kwani chuo hakina huruma na hawajari umetoka wapi.......sifagirii wanafunzi kucheat ila wanafanya hivyo kwa kuwa hali pale ni ngumu sana hivyo wanataka kufaulu kwa vyovyote vile.....hakuna asiyejua kuwa ifm is a very marketable college in the country wanafunzi wa ifm wanafanya vizuri sana katika ajira zao.......

What about Mzumbe?
 
ifm as a center of excellence wanapenda public ijue kuwa kuna matatizo kayika mfumo wetu wa elimu ambapo wanafunzi hawapendi kusoma wanataka kununua mitihani kitu ambacho wameshindwa ifm na badala yake wanaamua kutumia watu ili wawafanyie mitihani tofauti na vyuo vongine ambapo mambo humalizwa kiutu uzima bila mtu yeyote kujua...na hii sio mara ya kwanza kwa ifm kukamata na kutangaza waocheat
 
wanafunzi wa siku hizi (sio wote) hawakai hata library, kazi yao kuzurura na kusoma magazeti ya udaku. ukiwakuta library basi ujue kesho kuna mtihani, au anafanya assignment, na hata kufanya assignment anakuwa hayuko seriuos kabisa. mimi nimefundisha chuo na ninajua vizuri wanafunzi wa leo. ukimuuliza we unamalengo gani atakuambia amekuja kutafuta unga wa watoto. na sio kuelimika. muulize maswala ya nchi yanaendaje hajui kabisa. akienda kijijini wanajifanya wanaongea kiswanglish haya anza kuongea naye kiingereza. hapo utaona hio kiswanglish ni uzushi, ukweli ni kuwa hajui kiswahili wala kiingereza. sasa ukijuiliza anasoma nini ndio balaa atakuletea jina la kozi yake kwa mikwala. hata kijijini anawambia eti anasomea mambo ya social protection kwa kiswahili hawezi. najiuliza anaelewa au anacremu.
Tuwasaidie hawa wasomi wanawaza pesa tu wala hawawazi shule hawa ndio mafisadi wa kesho. hapa ndio unashangaa kuwa mtu yuko BOT baada ya kuwa mlinzi wa pesa naye anaiba. sasa jamani tunaelekea wapi na wasomi hawa?
UKitaka kujua kuwa wanafunzi hawa wanawaza fedha fanya utafiti ni wangapi waliwekeza fedha za mikopo DEC, utagundua kuwa ni wengi kupita kiasi.
 
Nimemaliza Ifm hapo 2009 haya mambo yapo Sana, nakumbuka Kuna mwanafunzi alijirusha kupitia dirishani ghorofa ya Pili alipobainika anamfanyia mtu mtihani.
 
Back
Top Bottom