Hawa ndio walipa kodi wakubwa nchini; NMB yabwaga Benki zote

Mi naona hii thread inakoelekea hamna tija yoyote! Bora kujikalia tu kimya! Aliyeanzisha hii thread hata hana uelewa wowote kuhusu kodi!
Kodi ina sheria zake na mipaka yake, cha muhimu kabla mtu hujaandika pumba humu, pitia vizuri Income Tax Acts na addendum zake zote, pitia pia audited financials za hayo makampuni ndio utajua kama wanastahili kulipa kodi ama lah!
Kulalama tu hapa mnaonekana kama wendawazimu!

Naona wengi sheria za kodi zimewapitia kushoto kama huyu mbunge aliyeta hii mada!
Siyo kosa lenu lakini!

Wewe ndiye Mwendawazimu kwani unamlaumu mleta mada just kwa kuweka tu list ya mashirika yanayoongoza kwa ulipaji kodi.
Kama unanufaika kwa namna moja au nyingine kwa hayo makampuni yanayokwepa kulipa kodi just shut up your mouth acha watu wajadili.
Ndibalema, mbona ni rahisi sana kumwelewa Rejao anaposema kwamba aliyeleta thread hii ni mbunge mbumbumbu kwa masuala ya kodi. Mizengo Pinda ndiye mbunge aliyeleta thread ndefu mle bungeni akiyataja pia haya makampuni 15 tu.

Alichofanya mbunge mwezake yaani Regia Mtema ni kuchomoa kipande kidogo cha pumba za huyu bwana Pinda na kutuhabarisha humu JF.

Rejao , endelea kuwafundisha ni nani mtoa pumba maana wengine akili yao inawatuma kudhani uwaziri mkuu wa Pinda unaufuta ubunge wake hadi eti ukimsema yeye ni mbunge mtoa pumba basi hiyo haiwaingii.

Endelea kutuletea list ya mambumbumbu wengine huko kwenye magamba na wenye akili tutakuelewa na kisha tutawaelewesha waliopotoka kama Ndibalema.
 
mwanakijiji natamani uandiki zaidi na zaidi.....

nafikiri kuna jambo hukutaka kuligusia ili kuepusha kubadili maudhui ya thread but ni muhimu mno....

go on...

Ujumbe umeshaeleweka Boss.. nikiandika zaidi itakuwa siyo tena kuwatafunia watu itakuwa na pamoja na kuwamezea..
 
Duh sijaona Vodacom, Tigo, Serengeti lazima hizi kampuni kuna mikono ya mafisadi badala ya kwenda serikalini kodi hizo wao ndo wanakula. Hawa Voda si wanajigamba ndo wenye wateja wengi TZ iweje wamepitwa na airtel katika ulipaji kodi??

TIGO?! hapana; hawa ni kama CHADEMA tu, wateja wake wengi wapo Dar es salaam na kwenye baadhi ya miji mikubwa na wengi wa wateja wao ni full ku-beep na ku2ma sms!!!! Vodacom, wana wateja wengi sana lakini inawezekana wateja wengi ni ocassional subscriberz.

Airtel, nao wana wateja wengi sana lakini hawa jamaa kv wamejaa sana hadi vijijini, nazani wamelikamata sana soko la international organizations kv NGOs, UN organs, kampuni za kitalii and the like!!! hawa jamaa, hawa-beep wala kutuma msg; bali ni full kwenda hewani na callz zao nyingi ni international callz hivyo sishangai kuona wanabamba kuliko hao Tigo na Vodacom!
 
Ukisikia serikali legellegendiyo hii. Tungependa tujue pia mashirika ya umma yanayoongoza kwa kulipa kodi (PAYE) za wafanyakazi

Ahsante dada Regina kwaupdate hii
 
Kwa nini tunainyoshea Vodacom kidole kwa nini tusijinyoshee sisi wenyewe.Sio leo tumefahamu kwamba Vodacom hawalipi kodi kulingana na mapato yao.Hili lipo ndani ya uwezo wetu,tunaweza kutoa fundisho kama wateja wa Vodacom kwa kuhamia Airtel

Mkuu mimi nashangaa kwanini watu bado wanajadili kuhusu hili. Mimi na ndugu zangu tulishafanya hivyo toka mwaka jana; actually toka tujue Rostam ni mmoja wa wanahisa wa kampuni hiyo. Kama kampuni inakula na mafisadi na haina uchungu na nchi, then kwanini wewe kama customer uendelee ku-invest huko?

Nawasihi wale wazalendo wote waamke, hili haliitaji nguvu nikubadilisha tu nakuchukua service nyingine. Lazima tuwalazimishe watuonyeshe wanapata faida kiasi gani na wanalipa kodi kiasi gani. Hawataki; then they do not need us as customers. Kwa hili ndugu zangu tunaweza, tuhamasishe watu sasa, words of mouth inasambaa vizuri sana tu hamna gharama.
 
Ujanja tu wa kuchezesha figa,
Watu wame-specialize kwenye kutafuta weakness ziko wapi wacheze na figa.
Kampuni inajifanya haijawahi kupata faida hata mwaka mmoja toka imeanza, lakini cha ajabu "haifi", inaishi tu
 
1.Voda inazidiwa na Airtel kwa ulipaji wa kodi wakati,voda ina wateja wengi(mapato mengi) kuliko airtel?
2.Makampuni makubwa ya madini yamezidiwa na kampuni ndogo tu Resolute?

Wana JF aka GT naomba mnijuze hii inatokana na nini? Nawasilisa Hoja
Unategemea kampuni ya Rostam kulipa kodi?
 
sasa inabidi tuwe na moyo wa uzalendo sisi watanzania wote, sababu ukiona iyo list almost 60 percnt ni kampun za ndan hakuna export apo ona tbl, konyagi,tcc,nmb zote ni leading tax payers it means thaman ya shiling lazima ishuke kila siku.

alaf hii group five ni kampun ya nan na inahusika na nn?
 
Kuna issue nyingine ya ya kujiuliza je wich key sector(s) does Tanzania economy rely on

Is it
Financial- Finacila sysytem ikicolapes UK, US ndio zinaumia zaidi
Cosumer economy- Hii pia UK , US wanaitegema Sana. So prchsing powwr y wananchi ni kitu muhimu . Kwa tanzania sio sana
Manufacturing & Industry- Hii ni kama Japan, Germany, CHina .
Military- Hii sijui kama niko sahihi lakini nadhani kwa UK, USA ,Russsia ni industry kubwa sana
Mining economy- Israel, Australia, Canada ni nchi ambzo zinafaidika sana na hii sekta. Ishangaza Tanzania
Agricutural- Tunasema Kilimo ni uti wa mgngo lakini mbona hakuna hata kampuni moja inajihusiaha na kilimo kwenyehiyo list
Tourism----

Sasa ukiangalia haraka haraka inaonekana Tanzania nayo tuna finanancial sector driven economy wakati ni asilimia chache sana ya watanzania wana acess na hizo financial insttutions.

Jamani mi sio mchumi napenda wachumi watuambie kitaalam uti wa mgongo wa Uchumi wa Tanzania ni sekta gani hasa
 
mkuu unauliza hilo swali huku jiulize
inakuwaje watanzania chini ya milioni mbili ndio wanatumia benki
halafu unaona benki zinazidi kulipa kodi kuliko makampuni ya mafuta kwa mfano....
 
1.Voda inazidiwa na Airtel kwa ulipaji wa kodi wakati,voda ina wateja wengi(mapato mengi) kuliko airtel?
2.Makampuni makubwa ya madini yamezidiwa na kampuni ndogo tu Resolute?

Wana JF aka GT naomba mnijuze hii inatokana na nini? Nawasilisa Hoja

1. Kibiashara inawezekana kuwa Voda ina wateja wengi lakini pia inawezekana kuwa gharama zao za uendeshaji ni kubwa kuliko Airtel.

2. Migodi ya madini uwekezaji wake ni kubwa sana kiasi huchukuwa muda zaidi kulipa gharama za uwekezaji mpaka kufikia kulipa kodi ya mapato, ndio maana serikali imeweka malipo ya mrabaha wa asilimia 4 iwe wamelipa gharama au hawajalipa hizo lazima wazilipe, tumeona mgodi mmoja umeanza kulipa kulipa corporate tax baada ya kuwa wamemaliza kufidia gharama za uwekezaji, na hivi karibuni tutaona kipato cha kodi cha migodi kikipita mapato mengine yote. Projections zinaonesha kuanzia 2012 mchango wa migodi katika makusanyo ya kodi utakuwa juu sana.
 
Tafadhali naomba mnielezee kwa undani zaidi kwa mlio bahatika kuangalia live (au Mh. Mtema), wakati Mh. PM alivyokuwa anaiwakilisha, vipi yeye alikuwa anaichukuliaje. Maana nakuambia kinachoendelea kwa sasa hivi hapa nchini kwetu watoto na wajukuu wetu watakuja kutumaliza. Maana watakapokuta kila kitu kimemalizika na wakaisoma historia ya nchi ilivyokuwa imeneemeka (Maana itakuwa haina kitu tena) nakuambia hamna patakuwa hapatoshi.

Ingawa hapo awali tulivamiwa na wageni (wazungu) na kutunyonya nguvukazi na malighafi lakini ukweli ni kwamba mababu zetu (Mkwawa, Kinjekitile, Mrambo, etc) walipambana. Wengine wakadhiriki kujiua kuliko kuona tunanyanyaswa hivi hivi ndani ya nchi yetu. Sasa leo tuna waambia tuchukeni tu (e.g. MADINI) hatuyahitaji.

TUTAFAKARI!!! TUCHUKUE HATUA
 
Ah! Sijui tukodi wapi kiongozi. Tumechoshwa na watawala.
Mi naona hata Gadafi angetufaa, maana kama kaweza kugeuza jangwa kuwa nchi ya kilimo sembuse huku ambako kila kitu kipo. Cha msingi zaidi ninachoona ni kwamba wapo viongozi wenye nia ya dhati ila hatujawapa nafasi. Tafadhali inapotokea nafasi kama ya Igunga hebu chukua uamuzi wa busara uone mabadiliko. Angalizo: 2015 usije ukachanganywa na maneno ya muda mfupi (wakati wa kampeni) ukasahau mlolongo wa matukio kama haya
 
Mengi ambayo nami nilitaka kuyazungumza naona tayari yameshaguswa na wengine; ya kwangu ni kujaribu tu kuweka context ili tunapozungumzia suala la kodi tuangalie na upande wake wa pili.

a. Jumla ya kodi zote zilizolipwa na makampuni hayo 15 ni Shilling Bilioni 949.2 yaani ni sawa na kusema 0.949 Trilioni Shillings.

b. Kwa mujibu wa hotuba ya Zitto mapema wakati kikao cha bejeti kinaanza alitudokeza kuwa "Wakati Waziri akisema Bungeni kuwa Bajeti ya mwaka 2011/2012itapunguza posho kama sehemu ya mkakati wa serikali wa kuthibiti matumizi, nanukuu "kupunguza malipo ya posho mbalimbaliyasiyokuwa na tija (uk.53)", ukweli ni kuwa Bajeti ya serikali ya mwaka2011/2012 imetenga jumla ya shilingi 0.987 trilioni ambazo ni sawa naasilimia 13 % ya recurrent budget ya serikali kwa ajili ya kulipa poshochini ya vifungu vinavyojulikana kama "Personnel allowances (nondiscretionary na In-kind"). Kwa hiyo, kauli ya Waziri Mkulo kuwaserikali itapunguza posho sio kweli. Tunautaka umma waWatanzania usikubali kurubuniwa" Yaani Bunge limetenga Shilingi Bilioni 987 kwa ajili ya posho. (hii nimenukuu kutoka katika taarifa yake kwa vyombo vya habari baada ya hotuba ya bajeti)

c. Zitto akatudokeza kitu kingine pia kwenye hotuba hiyo hiyo Matumizi mabaya ya fedha za umma yameendelea kuwa kikwazokikubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.Uchambuzi wetu juu ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2009/2010 pekee, umebainitakribani jumla ya Tsh trilioni 2.4 za fedha za umma zilitumika vibaya,ambazo ni sawa na asilimia 25% ya bajeti yote ya mwaka huoambayo ilikuwa na jumla ya Sh 9.5 trilioni.

MASWALI KATIKA MAUDHUI:
1. Tunaweza vipi kuzungumzia na kufurahia ulipaji mkubwa wa kodi katika mazingira ya matumizi mabaya na yasiyo na tija ya kodi hiyo? Tuna uhakika gani kuwa kama watu wakilipa kodi zaidi fedha zaidi hazitatumiwa vibaya ceteris paribus.

2.
Je tunaweza kuimarisha na kutengeneza mfumo mzuri zaidi wa kodi bila ya kutengeneza mfumo mzuri zaidi wa usimamizi wa fedha za umma? Iweje tuone maji kutoka kwenye mto yapo na yanakuja ili kumwagilia bustani zetu lakini wakati huo huo kuna wajanja wanadiverge maji hayo kwenda kwenye shamba la jirani? Tudai maji zaidi, ili wao wanidiverge zaidi kwenda huko au hata maji kidogo tunayopata tuyasimamia na kuyatumia vizuri – tuzibe nyufa na mifereji inayokwenda kwa jirani au tufanye nini ili tujue nini kina kwenda kwa jirani na kwa makubaliano gani?

3. Siasa za vyama vyetu vya kisiasa ziko vipi katika pande hizi mbili za suala la kodi na matumizi yake? Je vyama vinaamini nini kuhusu kodi kama msingi wa itikadi zao? Maana masuala ya kodi ni mojawapo ya masuala yanayotofautisha sana vyama vya kisiasa duniani, kwetu sijui kuna tofauti gani hasa kuhusu kodi. I mean, kuna tofauti gani katika mitazamo ya kodi, mapato na matumizi kati ya CCM na CHADEMA au CUF? Tukumbuke kuwa Kodi ni siasa na siasa ni kodi. Hivi viwili havitengani, havitenganishwi, na havitenganishiki. Tusiangalie suala hili la kodi kwa macho ya kiuchumi tu; Taxes are what make politics tick!

Nimeandika zaidi ya nilivyotaka kuandika.

MMM
MMM,Kama kodi zingekusanywa vizuri na matumizi yake kuwa appropriatelly allocated,ie kupelekwa kunakohitajika pengine tusingetegemea misaada na kuyumbishwa kama wendawazimu kama ilivyo jivi sasa.Ufisadi mwingi sana mizizi yake imeanzia kwenye hizo loopholes.Msingi wa serikali yeyote ile ni ukusanyaji wa kodi.Hiyo pesa iliyotakiwa ikusanywe however inaenda to a few individuals.And thats where the pronlem is.
 
Mengi ambayo nami nilitaka kuyazungumza naona tayari yameshaguswa na wengine; ya kwangu ni kujaribu tu kuweka context ili tunapozungumzia suala la kodi tuangalie na upande wake wa pili.

a. Jumla ya kodi zote zilizolipwa na makampuni hayo 15 ni Shilling Bilioni 949.2 yaani ni sawa na kusema 0.949 Trilioni Shillings.

b. Kwa mujibu wa hotuba ya Zitto mapema wakati kikao cha bejeti kinaanza alitudokeza kuwa "Wakati Waziri akisema Bungeni kuwa Bajeti ya mwaka 2011/2012itapunguza posho kama sehemu ya mkakati wa serikali wa kuthibiti matumizi, nanukuu "kupunguza malipo ya posho mbalimbaliyasiyokuwa na tija (uk.53)", ukweli ni kuwa Bajeti ya serikali ya mwaka2011/2012 imetenga jumla ya shilingi 0.987 trilioni ambazo ni sawa naasilimia 13 % ya recurrent budget ya serikali kwa ajili ya kulipa poshochini ya vifungu vinavyojulikana kama "Personnel allowances (nondiscretionary na In-kind"). Kwa hiyo, kauli ya Waziri Mkulo kuwaserikali itapunguza posho sio kweli. Tunautaka umma waWatanzania usikubali kurubuniwa" Yaani Bunge limetenga Shilingi Bilioni 987 kwa ajili ya posho. (hii nimenukuu kutoka katika taarifa yake kwa vyombo vya habari baada ya hotuba ya bajeti)

c. Zitto akatudokeza kitu kingine pia kwenye hotuba hiyo hiyo Matumizi mabaya ya fedha za umma yameendelea kuwa kikwazokikubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.Uchambuzi wetu juu ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2009/2010 pekee, umebainitakribani jumla ya Tsh trilioni 2.4 za fedha za umma zilitumika vibaya,ambazo ni sawa na asilimia 25% ya bajeti yote ya mwaka huoambayo ilikuwa na jumla ya Sh 9.5 trilioni.

MASWALI KATIKA MAUDHUI:
1. Tunaweza vipi kuzungumzia na kufurahia ulipaji mkubwa wa kodi katika mazingira ya matumizi mabaya na yasiyo na tija ya kodi hiyo? Tuna uhakika gani kuwa kama watu wakilipa kodi zaidi fedha zaidi hazitatumiwa vibaya ceteris paribus.

2.
Je tunaweza kuimarisha na kutengeneza mfumo mzuri zaidi wa kodi bila ya kutengeneza mfumo mzuri zaidi wa usimamizi wa fedha za umma? Iweje tuone maji kutoka kwenye mto yapo na yanakuja ili kumwagilia bustani zetu lakini wakati huo huo kuna wajanja wanadiverge maji hayo kwenda kwenye shamba la jirani? Tudai maji zaidi, ili wao wanidiverge zaidi kwenda huko au hata maji kidogo tunayopata tuyasimamia na kuyatumia vizuri – tuzibe nyufa na mifereji inayokwenda kwa jirani au tufanye nini ili tujue nini kina kwenda kwa jirani na kwa makubaliano gani?

3. Siasa za vyama vyetu vya kisiasa ziko vipi katika pande hizi mbili za suala la kodi na matumizi yake? Je vyama vinaamini nini kuhusu kodi kama msingi wa itikadi zao? Maana masuala ya kodi ni mojawapo ya masuala yanayotofautisha sana vyama vya kisiasa duniani, kwetu sijui kuna tofauti gani hasa kuhusu kodi. I mean, kuna tofauti gani katika mitazamo ya kodi, mapato na matumizi kati ya CCM na CHADEMA au CUF? Tukumbuke kuwa Kodi ni siasa na siasa ni kodi. Hivi viwili havitengani, havitenganishwi, na havitenganishiki. Tusiangalie suala hili la kodi kwa macho ya kiuchumi tu; Taxes are what make politics tick!

Nimeandika zaidi ya nilivyotaka kuandika.

MMM
Mnaumiza vichwa bureee! CCM has to go.. hii ndio solution peke yake..
Niliwaambia toka zamani kwamba hakuna utaratibu mzuri wa kukusanya kodi, nanyi hamwishi kumsifia Mkapa kwa sifa za kuunganisha unganisha. Mkuu wangu, haya mashirika yamekuwa na yataendelea kuwa mashirika yanayochangia kodi zaidi ya mashika yote kwa sababu ndio tulikowekeza kiukweli toka Ujamaa. Hizo Beer, sigara na Banki ndiko kuna mzunguko, benki zikiwa na mikopo ya mwaka au miaka miwili interest za asilimia 30, na watu wakipoteza ardhi nyumba na hata assets zao.. Hizi porojo za wawekezaji kutoka nje sidhani kama wapo ktk mashirika 100 bora. Na nakuhakikishia haya mashirika yalikuwa ya serikali yakichangia kwa juu hata kabla ya kutaifishwa..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom