Hawa ndio walipa kodi wakubwa nchini; NMB yabwaga Benki zote

Mnabweka tu kuilaumu serikali kwa kutokusanya kodi!
Hamjui kuwa kukusanya kodi ni jukumu la kila mwananchi na si serikali!!
Hatuitetei CCM, tunajarinu kuwaelimisha mambumbumbu kama wewe!

Lini utaacha kufikiri kwa kutumia masaburi?
Nenda kakusanye kodi wewe uone kama hujatolewa mkuku kama kuku wa Eid
 
Kuna aina nyingi za kodi, iliyoripotiwa hapa na huyu muandaa maadamano wa CDM

Hapa ndio nikasema hii issue ni complex sana kwa mtuma picha, labda ingekuwa ni kutufahamisha mavazi ya waziri mkuu alipokuwa anafunga kikao.
 
Lini utaacha kufikiri kwa kutumia masaburi?<br />
Nenda kakusanye kodi wewe uone kama hujatolewa mkuku kama kuku wa Eid
Naona hujui unachokizungumza!
Tafuta Income Tax Act uisome vizuri labda itapunua kidogo uelewa wako!
 
.....
Mbona Tanzania ndio mzalishaji mkubwa wa 3 wa dhahabu duniani na migodi inayoongoza hapa Tz, ni ile ya GGM na Barrick wakati kwenye ripoti ya PM, hawapo?

Haya makampuni yanatuingiza mkenge sababu yanapokuja yakauja na data za uongo.

Mfano Vodacom wakati wanawezekeza waliforecasts kuwa wataaanza kupata faida nadhani bada ya miaka kama 10. Sijui kama walibadilisha. So kipindi chote hicho account book zao zinanyesha wana recover cost za investment. Nadhani kwenye makampuni haya ya madini ndio janja hiyo hio inatumika. Je Tanzania ina capacity ya kuthibitsha na kukagua haya makampuni au inategema zaidi yawe honest?

Majibu mepesi kwa maswali magumu ni kuwa bado hawajaanza kupata faida wanarudisha gharama zao za uwekezaji teh teh teh teh . Kwa maana hiyo hata income Tax wanayolipa itakuwa ndogo sana . Ni kucheza na balance sheet tu na kutoa pesa ya "mawasiliano" kwa wahusika wakuu basi mchezo kwishney.
 
Vodaaaaaaaaa mnatuangusha mnakuwa kama wale wa madini ambao tumenawa mikono kukusanya kodi

Tunaweza kuamua kuwagomea hawa Voda. Yaani kwa hasira tunaacha kutumia huduma zao, hawana faida kwetu. Uzuri substitutes za huduma zao zote zipo hapa kwetu.

Tumekuwa watu wa maneno kwa nini tusioneshe mfano katika hili??????
 
Hebu tupe ushaidi, labda tunaweza kulifanyia kazi!

avatar23356_4.gif


Ushahidi ulitunzwa kwenye kidevu chako,...too bad rostam kaondoka nacho
so hadi atoke uarabuni huko,....
Vipi umesharudi toka uarabuni?
 
Hiyo list inamaanisha hao tu ndio wanaolipa kodi?
Au wengine wanalipa kidogo hadi imekuwa aibu kusema.
 
Hahaha, kweli shule muhimu, yaani kwa kupewa hizo data hapo juu... unaweza kujadili mambo kwa undani especially kutaja makampuni mengine... mwajua kuna issue za ku-break even, kutengeneza faida etc...

Yes, i hate this country b'se everything is politics... kwa mfano kama Azam ana makampuni matano au 10.... as a group, huwezi kuona Azam as a group kumwona kama mlipa kodi mkubwa kwa sasa babu yaliyoletwa hapo ni makampuni independent... yaani badala ya kusema IPP, imeletwa the Gurdian, Raido one Limited etc... We need to be carefully tukijadili haya mambo.

Mwisho na sikitishwa na kukosekana kwa makampuni ya infrastructure... yaani TANESCO, TRL, ATCL, TTCL, etc... kufa kwa haya makampuni ndio mchawi wa uchumi wetu!
 
Kumbe ndo maana bia na sigara vinapanda kila bajeti, duh naona bajeti yetu inategemea pombe na sigara badala ya kuangalia, vyanzo vinavyo toa mapato makubwa. Wanywaji pombe tupunguze kunywa. Af mwaka kesho tuone wataongeza bei kwenye nini.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mgodi mdogo uliopo nzega wa RESOLUTE T LTD inamana unalipa kod kubwa kulko GGM,BULYANKULU,etc inaniwia vgumu kuamin hlo!
 
Where's Vodacom, Geita Gold, Bulyanhulu, Artumas, Songas,North Mara, Buzwagi????????

Hawalipi kodi, bado wanajiendesha kwa hasara

Pamoja na kodi ya kawaida, makampuni haya yalistahili kulipa kodi ya faida ya ziada "Windfall Profit Tax". Sasa hata ile ya kawaida ni fumbo.

Windfall Profit Tax ni kodi inayotozwa kwa sekta ya uchumi ambayo imepata faida kubwa kupindukia kutokana na kuongezeka ghafla kwa bei ya bidhaa zake. Marekani walitumia kodi hii 2005 kwa kampuni ya mafuta ya EXXON MOBIL ambayo mwaka huo 2004 ilipata faida ya $36 billioni kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta. Faida hiyo ilikuwa zaidi ya matarajio, na Windfall Profit tax ikapata kutumika.

Makampuni ya madini yalipokuwa yanatayarisha Maandiko ya Miradi yao, bei ya dhahabu ilikuwa around $350 kwa ounce, na bado waliona kuwa kwa bei hiyo wangeweza kumudu gharama za kuanzisha mradi (capital expenditure) na kupata faida. Sasa hivi bei ya dhahabu ni karibu $1900 kwa ounce. (Source yangu: Sky News: Gold sets new record). Hii ina maana kwamba kwa kila ounce ya dhahabu inayouzwa sasa, faida isiyotarajiwa ni $1550!!! Na bado hata faida tokana na ile $350 inaonekana si haki yetu.

Wabunge wetu wa pande zote mlio na uchungu na nchi yetu, piganieni Windfall Tax Profiti iingizwe kwenye sekta hii ya madini. Please.
 
Regia
Kama ukiona vyema tafadhali naomba kupata softy copy ya hiyo hotuba
Otherwise kuna usanii mwingi katika suala zima la kukusanya kodi


Wakuu,Salaam!

Kwa wale mliofuatilia Hotuba ya Waziri Mkuu wakati wa kuahirisha Bunge Jana alitoa pongezi na kuzitaja Makampuni au Mashirika yanayoongoza kwa kulipa Kodi hapa nchini.

Alisema kwa kipindi Cha mwaka 2005 na 2011 Makampuni hayo yamekuwa yakifanya vizuri katika ulipaji Kodi.

Aliyataja Makampuni hayo Kama ifuatavyo;

1. Tanzania Breweries Company(TBL) Shilingi Bilioni 165.4

2. National Microfinace Bank(NMB). Shilingi Bilioni 108.6

3. Tanzania Cigarette Company(TCC). Shilingi Bilioni 92. 1

4. National Bank of Commerce(NBC). Shilingi Bilioni 89.9

5. CRDB LTD Shilingi Bilioni 79.2

6. Tanzania Ports Authority(TPA) - Shilingi Bilioni 76.8

7. Tanzania Potland Cement - Shilingi Bilioni 73.4

8. Airtel(T) LTD - Shilingi Bilioni 63.6

9. Tanga Cement Company - Shilingi Bilioni 43.6

10. Standard Charted Bank - Shilingi Bilioni 40.0

11. City Bank. Shilingi Bilioni 35.7

12. Resolute(T) LTD. Shilingi Bilioni 32.1

13. TICTS. Shilingi Bilioni 25.9

14. Tanzania Distillers LTD. Shilingi Bilioni 13.4

15. Group Five International. Shilingi Bilioni 9.5

Haya Wakuu na tujadili na kutoa maoni yetu...
 
Kwa kweli tunahitaji kufanya kitu juu ya hili ikibidi tuandamane kuishinikiza serkali ikusanye kodi ipasavyo
 
Kwa kweli tunahitaji kufanya kitu juu ya hili ikibidi tuandamane kuishinikiza serkali ikusanye kodi ipasavyo

Wahindi walipigania uhuru wao wakiongozwa na Mahatma Ghandi kwa kususia bidhaa za wanaowanyonya na kuwatawala bila matashi yao.

Sisi pia hao wanaotunyonya kama VODACOM, tunaweza kuwafundisha somo la MTEJA ni MFALME kwa kususia huduma zao, kwa kuwa wanatunyonya kwa kutengeneza faida kubwa sana, na kisha hawachangii ipasavyo kwa maendeleo yetu kwa kulipa kodi kiduchu...

Hili halihitaji bunge wala watawala wetu kutuamrisha kama tunaona uchungu kweli.
 
Pamoja na makampuni hayo,lakini ikumbukwe kuwa watumishi wa umma wanaongoza kwa kulipa kodi kutoka ktk mishahara yao kuliko hayo makampuni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom