Hawa ndio walipa kodi wakubwa nchini; NMB yabwaga Benki zote

Inaonekana sekta ya madini hailipi kwa hakika,
Serikali isimamishe uvunaji/uchimbaji wa madini kwa wawekezaji mara moja,
Tusubiri baada ya miaka mitano ndio tuaangalie jinsi ya kuwekeza kwenye hii sekta ya madini.
Eneo lingine ambalo linasikitisha ni UTALII, sekta hii inaiingiza pesa nyingi
Uwezekano ni kuwa wakusanya kodi hawafuatilii au zinapenya kwa wajanja, nayo iangaliwe upya
 
Dhahabu yetu inapotea bure,haisaidii uchumi wala kustabilize shilingi yetu!

Huko kwenye dhahabu ndo unanitonosha kidonda changu kilicho anza kupona.
Jamaa hawa wanao jidai ndo wenye nchi wameziba pamba masikioni dhahabu jamaa wanasafirisha matani na matani.
Inatia aibu mpaka mchanga nao wanasafirisha hayo mashimo watakuja kufukia na nini? Kama mpaka mchanga wanasafirisha.
 
Wakuu,Salaam!

Kwa wale mliofuatilia Hotuba ya Waziri Mkuu wakati wa kuahirisha Bunge Jana alitoa pongezi na kuzitaja Makampuni au Mashirika yanayoongoza kwa kulipa Kodi hapa nchini.

Alisema kwa kipindi Cha mwaka 2005 na 2011 Makampuni hayo yamekuwa yakifanya vizuri katika ulipaji Kodi.

Aliyataja Makampuni hayo Kama ifuatavyo;

1. Tanzania Breweries Company(TBL) Shilingi Bilioni 165.4
2. National Microfinace Bank(NMB). Shilingi Bilioni 108.6
3. Tanzania Cigarette Company(TCC). Shilingi Bilioni 92. 1
4. National Bank of Commerce(NBC). Shilingi Bilioni 89.9
5. CRDB LTD Shilingi Bilioni 79.2
6. Tanzania Ports Authority(TPA) - Shilingi Bilioni 76.8
7. Tanzania Potland Cement - Shilingi Bilioni 73.4
8. Airtel(T) LTD - Shilingi Bilioni 63.6
9. Tanga Cement Company - Shilingi Bilioni 43.6
10. Standard Charted Bank - Shilingi Bilioni 40.0
11. City Bank. Shilingi Bilioni 35.7
12. Resolute(T) LTD. Shilingi Bilioni 32.1
13. TICTS. Shilingi Bilioni 25.9
14. Tanzania Distillers LTD. Shilingi Bilioni 13.4
15. Group Five International. Shilingi Bilioni 9.5

Haya Wakuu na tujadili na kutoa maoni yetu...
Ukiifuatilia hii nchi unaweza kujinyonga kwa maudhi. Kumbe kuna makampuni kibao yanayofanya kazi ya kutuibia tu hapa nchini na si vinginevyo! Hata hao wanaokusanya kodi ni vichwa vya wendawazimu kwani hawazishtukii kampuni kama Vodacom ambayo kwa vigezo vyovyote ndiyo wanaoongoza kwa uwingi wa wateja na bei ya bidhaa zao, Tigo ambayo hivi karibuni imesomba wateja wengi kwelikweli na ambayo bidhaa zake zinatozwa sawa kabisa na Zain na hata Vodacom?
Halafu kuna faida gani kwa madini yetu kuchimbwa kwa fujo namna hii kama tunachopata kama mchango kwenye kodi ni kiduchu namna hii na hakiingii hata katika fungu la kumi la mapato yetu kitaifa? Kwa lugha rahisi ni kwamba kumbe tungeweza kufunga migodi yoye bila athari kubwa kwenye uchumi wetu. Ni aibu kwa wakusanya kodi na ni tusi kwa taifa kusikia kikampuni kama Group five kipo kwenye kumi na tano bora za walipa kodi wakuu huku kampuni kama Vodacom inayomgusa karibu kila mwananchi ikiwa mbaali kabisa!
Mi nashauri tufanye yafuatayo:
i. Iundwe tume huru ya wachumi waliobobea wakiwemo wabunge haswa wa upinzani chini ya jopo la majaji watatu kuchunguza makampuni yoote yanayokwepa kodi. (Kwa vile hawa wa CCM tayari wameshindwa kwa miaka yote hii kubaini wizi huu na inawezekana makampuni yanayokwepa kodi kama Vodacom yanalipa sehemu fulani CCM).
ii. Kampuni itakayobainika kukwepa kodi ifilisiwe mali zake zote kufidia hasara waliyolipatia taifa.
iii. TRA iundwe upya na Mkurugenzi wake awajibike kwa Bunge.
iv. Watakaobainika katika TRA ya sasa kufunikafunika uhalifu huu wafunguliwe ya uhujumu uchumi.
v. Mwisho wa yote tudai uwajibishwaji wa wahalifu hawa waliojificha kwenye chama kinachonuka rushwa cha CCM na serikali yao.
 
Kwa kila Jumanne na Alhamisi tofali za dhahabu zenye ukubwa wa tofali la kuchoma na uzito wa gramu 12000 zipatazo 400 husafirishwa kwenda nje ya nchi, Hebu jiulize Gramu 1 ya dhahabu huuzwa Tsh 65,000. Je ni kiasi gani cha fedha kinakwenda nje na je kinaweza kukidhi bajeti yetu? Pigeni hesabu kisha mnijulishe...! Je hii pesa haiweza kutuokoa na u-ombaomba kwa wazungu?


Hiyo hesabu ni kwa GGM pekee, bado wapo NORTH MARA, KAHAMA, ULYANKULU, BIHARAMULO.

Kwa nini pamoja na ukwasi huo bado tunaishi kimaskini?

MAWAZO YAKO YANAWEZA KUTUPA DIRA TUKAEPUKA KUIBIWA

MIMI NAAMINI KAMA TUKIKUSANYA KODI KWA MADINI PEKEE, MAISHA MAZURI KWA WATZ YATAPATIKANA BILA KWERE
 
Is this information correct? Ina maana kodi kwenye mafuta hazilipwi kwa kiwango kikubwa? by the way, on monthly basis, which sector contributes more in revenue collection?
 
Misingi ya makampuni kutokulipa kodi, ipo katika sheria za kifisadi kama vile SHERIA YA MADINI 2010, na SHERIA YA UWEKEZAJI TANZANIA. UKIZISOMA UTAPATA MAJIBU YA SERIKALI LEGELEGE KUSHINDWA KUKUSANYA KODI.

SHERIA HIZO NDO CHANZO CHA MAKAMPUNI KUBADILISHA MAJINA KILA UCHWAO LEO.

UDHAIFU UNAOPATIKANA KATIKA SHERIA HIZO, NI WAWEKEZAJI KULIPA KODI BAADA YA WAO KUTANGAZA KUPATA FAIDA. NANI ATATANGAZA KUPATA FAIDA KATIKA MAZINGIRA HAYA?
HAPA KWETU WENYEJI TUNALIPA KODI KULIKO WAWEKEZAJI.

WIZI MTUPU.

 
hawalipi kodi, bado wanajiendesha kwa hasara

Mkuu sasa napata jibu kwa nini Vodacom walihusika sana kumchafua sana Dr.Slaa kipindi cha kampeni.
Fadhira yao sasa ni kukwepa kodi haingii akili kampuni hii ya voda ni kubwa kuliko airtel hapa Tanzania alafu izidiwe na Airtel kulipa kodi ni fadhira hizo kwa mwenye hisa nyingi R.A gamba lililo vuka.
 
Haya ni maajabu ya dunia, yaani pamoja na utajiri mkubwa wa rasili mali kama vile madini, mbuga za wanyama, samaki baharini na kwenye maziwa na mito, ardhi kubwa na yenye rutuba ambao Mwenyezi Mungu ametujalia lakini tunategemea POMBE kama ndiyo chanzo kikubwa cha mapato ya taifa letu.

Kweli akili ni mali, watawala wetu wametuangusha sana, hata Mungu nafikiri anajiuliza kuwa hivi nilikosea wapi kuwaumba viumbe hawa niliowakabidhi utajiri huu wooote ili wawe jamii ya watu matajiri sana duniani lakini wanauachia utajiri ukanufaishe watu toka mabara ya mbali na wenyewe wakibaki kuwa jamii ya watu masikini sana duniani hapa.

Hao si wengine bali ni Watanganyika.
 
Kweli Tanzania ni zaidi tUijuavyo!! Yaani mbwembwe zote za M pesa, Mtandao Mkubwa kuliko yote Africa, Kumbe hata Kodi Hawalipi? Sasa Tukisema usalama wa Taifa unatuhujumu wananchi Tutaambiwa Wachochezi??

Hili inabidi Liangaliwe Upya Hatuwezi kujisifu kila siku nchi ina rasilimali kibao kumbe Hakuna chochote kinaingia kwenye kodi Hii ni aibu sana!! Mwenye kutujuza VODA-MAGAMBA WAPO NUMBA NGAPI?
 
Vodaaaaaaaaa mnatuangusha mnakuwa kama wale wa madini ambao tumenawa mikono kukusanya kodi
 
FUNUNU KUTOKA LARGE TAX PAYERS DEPARTMENT OF TRA

1. Ex Hon. RA anaongoza kwa kukata rufaa kwenye malipo yake ya kodi (Ndo maana Hamna kampun yake kwenye list.

2. Hiyo idara inaongoza kwa rushwa, ukitaka usilipe kodi, unasogeza mpunga wa nguvu kwa Mkurugenzi.

MY TAKE: the department has to be audited and overhauled,

HAWA NDO WANAILETEA HASARA SERIKALI KWA KUTOKUKUSANYA FEDHA
 
Kwa kila Jumanne na Alhamisi tofali za dhahabu zenye ukubwa wa tofali la kuchoma na uzito wa gramu 12000 zipatazo 400 husafirishwa kwenda nje ya nchi, Hebu jiulize Gramu 1 ya dhahabu huuzwa Tsh 65,000. Je ni kiasi gani cha fedha kinakwenda nje na je kinaweza kukidhi bajeti yetu? Pigeni hesabu kisha mnijulishe...! Je hii pesa haiweza kutuokoa na u-ombaomba kwa wazungu?


Hiyo hesabu ni kwa GGM pekee, bado wapo NORTH MARA, KAHAMA, ULYANKULU, BIHARAMULO.

Kwa nini pamoja na ukwasi huo bado tunaishi kimaskini?

MAWAZO YAKO YANAWEZA KUTUPA DIRA TUKAEPUKA KUIBIWA

MIMI NAAMINI KAMA TUKIKUSANYA KODI KWA MADINI PEKEE, MAISHA MAZURI KWA WATZ YATAPATIKANA BILA KWERE

Mkuu haya maneno yanaweza yakakufanya ubadili uraia !
 
Misingi ya makampuni kutokulipa kodi, ipo katika sheria za kifisadi kama vile SHERIA YA MADINI 2010, na SHERIA YA UWEKEZAJI TANZANIA. UKIZISOMA UTAPATA MAJIBU YA SERIKALI LEGELEGE KUSHINDWA KUKUSANYA KODI.

SHERIA HIZO NDO CHANZO CHA MAKAMPUNI KUBADILISHA MAJINA KILA UCHWAO LEO.

UDHAIFU UNAOPATIKANA KATIKA SHERIA HIZO, NI WAWEKEZAJI KULIPA KODI BAADA YA WAO KUTANGAZA KUPATA FAIDA. NANI ATATANGAZA KUPATA FAIDA KATIKA MAZINGIRA HAYA?
HAPA KWETU WENYEJI TUNALIPA KODI KULIKO WAWEKEZAJI.

WIZI MTUPU.

Natamani kulia yote hii ni sera mbaya za chama cha magamba na serikali yao wao kuhongwa mil.200 wanaona wamefaidika kumbe kinacho toroshwa ni mara 100 ya hicho walicho hongwa shame on you CCM
 
Nmb wangeweza kuongoza kama wangeongeza uwajibikaji na huduma bora kwa wateja, kupambana na tatizo la milolongo ya wateja, wangeboresha taratibu za utoaji mikopo, ingawa hivyo nawapongeza.

Nbc wamejitahidi, crdb wamenihuzunisha kidogo, mikakati yao ni ya kimatumizi makubwa, naamini kuna atm za bei mbaya hazina mrejesho unaolingana na mtaji, konyagi oyee! japo si urithi wa watz, watengeneza saruji kuna tatizo. sijawana vodacom inamaana mpaka hela za kuendesha michezo ya kubahatisha wanatuibia, achilia mbali wingi wa wateja wake wanapitwa na wanywa konyagi na wavuta fegi, ndiyo maana namchukia mwanahisa wa voda el, naamini anafanikisha tuibiwe, tigo watasingizia wanapanua mtandao wao ufike vijijini, bandari imetuangusha sana!!

kuna tatizo azam, mohamed ent. ticts, napendekeza tufunge migodi yote tanzania, atakayetangaza nia ya kuchimba ajue madini ni yetu, sisi tutamgawia 25% ya faida kwa kuleta mitambo yake, kama hawataki watuache tutie akili.

Mchango wangu japo kwa uchache mara hii.
 
people should wake up...itafika kipindi tutakufa wote hapa Tanzania... yani kampuni la sigara nalo linaongoza kwa kulipa kodi/? watanzania tuache kuvuta masigara ..vipi migodi? imesamehewa kodi cio
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom