Hawa ndio wabaya wa waislamu na uislamu wenyewe kwa Tanzania...

Status
Not open for further replies.
Chama soma hoja badala ya kuleta uzushi. Naona umeanza kuthibitisha aliyosema Mtoi. Maana badala ya kuangalia nini kimeongelewa unaanza shutuma na jazba.

Jazba nizitoe wapi? Ukweli utabaki kama ulivyo; upo mfumo ambao hauna malengo mema kwa nchi yetu; uwe mfumo kristo au mfumo shetani ni jina tu; tatizo lipo na linafahamika kwa kina labda kama unataka kuleta malumbano ya kiccm na kichadema nitakubaliana na wewe.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Nadhani hujamuelewa Mtoi; amedai haoni tatizo liliopo liwe ni mfumo kristo kama unavyodaiwa au mfumo wa ukandamizaji; cha kushangaza amekuja mawazo ya kurekebisha mfumo ambao hauna tatizo; yeye haoni tatizo la mfumo mzima kwa sababu lengo lake kuu ni kutaka kuishutumu CCM; ushauri ni serikali kuvunja MoU na taasisi zote za kidini hapo ni pa kuanzia tu.
Chama
Gongo la mboto DSM

MM is a PhD holder! Usijilinganishe na wewe mbambaishaji
 
Jazba nizitoe wapi? Ukweli utabaki kama ulivyo; upo mfumo ambao hauna malengo mema kwa nchi yetu; uwe mfumo kristo au mfumo shetani ni jina tu; tatizo lipo na linafahamika kwa kina labda kama unataka kuleta malumbano ya kiccm na kichadema nitakubaliana na wewe.

Chama
Gongo la mboto DSM
Mfumo wowote unaokandamiza Waislamu kama upo, basi unakiri kua chama chako CCM kinahusika.

Maana hakuna mfumo-dini utakao-exist bila blessings za chama tawala. Lakini ukiambiwa hili bado utaendelea kua Lumumba's follower huku ukikubali uislamu unakandamizwa.

Mkuu, kaa chini uji-study upya falsafa na uumini wako kwenye dini na chama ili usiwe na "double standards".
 
Sikupenda kuongeza neno, lakini Nimeumia sana kuona "Chama" bado anabisha ukweli huu !

Mkuu ukweli upo si kweli mamilioni ya waislamu wanacholalamika hakina msingi; usiumie jaribu kunielemisha labda kuna kitu sijakielewa; mfumo mzima wa elimu una matatizo ya kimsingi; ukija na hoja hafifu kama muuza njugu hutaliona tatizo.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mfumo wowote unaokandamiza Waislamu kama upo, basi unakiri kua chama chako CCM kinahusika.

Maana hakuna mfumo-dini utakao-exist bila blessings za chama tawala. Lakini ukiambiwa hili bado utaendelea kua Lumumba's follower huku ukikubali uislamu unakandamizwa.

Mkuu, kaa chini uji-study upya falsafa na uumini wako kwenye dini na chama ili usiwe na "double standards".

Mkuu hakuna suala la double standard; tatizo wanalolamika waislamu wa Tanzania ni msingi; kumbuka serikali yetu inajiendesha kwa misingi na taratibu tuliyoiiga kutoka kwa wakoloni; na mengine yameongezewa kutokana na mifumo ya kichumi tuliyonayo sasa hivi. Si kweli kuwa waislamu hawataki kusoma au kujiendeleza yapo matatizo ambayo yanachangiwa na mfumo mzima serikali pamoja na mashinikizo mengine.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Adui wa dini yeyote ni imani yake muumini wa dini hiyo. Kudhania kuwa dini tofauti na yako, kikundi, mtu au taasisi fulani ni adui au wapinga imani au maendeleo yako kiimani ni fikira potofu kwakua hakuna yeyote kati ya sisi wanadamu ajuea contacts za Mungu zaidi ya sala, kufuata kanuni zake na mafundisho ya mitume wake wote.

Mtu aneye hujumu dini yako ni yule anaye text au email MUngu kuwa watu wa dini fulani usiwape shavu wakifika mbinguni....zaidi ya hapo yeye ndio anatusubiri kutuhukumu kadri ya makosa yetu. Tunagombana nini sisi wanadmu hali wote sisi ni watuhumiwa mbele yake?

Mfano rais awe muislamu yeye pamoja na baraza lake lote la mawaziri, mimi kama muislam nafaidika na kipi? Same applied mfano huo kwa wakristo.

Kibanga Msese

 
MM is a PhD holder! Usijilinganishe na wewe mbambaishaji

Ahaa haaa Ph.d mkuu zisikutishe zinauzwa kama njugu kama unataka sema na wewe tukutumie; na kama ni kweli MM ni Ph.d nitahoji zaidi hiyo Ph.d ilipopatikana kiwango cha uchambuzi wake ni hafifu sana kama vile certicate ya chuo cha ualimu Eckenford cha Kange.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu hakuna suala la double standard; tatizo wanalolamika waislamu wa Tanzania ni msingi; kumbuka serikali yetu inajiendesha kwa misingi na taratibu tuliyoiiga kutoka kwa wakoloni; na mengine yameongezewa kutokana na mifumo ya kichumi tuliyonayo sasa hivi. Si kweli kuwa waislamu hawataki kusoma au kujiendeleza yapo matatizo ambayo yanachangiwa na mfumo mzima serikali pamoja na mashinikizo mengine.

Chama
Gongo la mboto DSM
Serikali ya CCM, sio??
 
Nadhani hujamuelewa Mtoi; amedai haoni tatizo liliopo liwe ni mfumo kristo kama unavyodaiwa au mfumo wa ukandamizaji; cha kushangaza amekuja mawazo ya kurekebisha mfumo ambao hauna tatizo; yeye haoni tatizo la mfumo mzima kwa sababu lengo lake kuu ni kutaka kuishutumu CCM; ushauri ni serikali kuvunja MoU na taasisi zote za kidini hapo ni pa kuanzia tu.

Chama
Gongo la mboto DSM

Chama pengine mnatofautiana vitu vidogo sana. Kwa kweli ukifanya bishara ktk soko moja na Bakheresa ktk bidhaa za aina moja kuna uwezekano akakumeza sana na ikibidi hata nyumbani kwako zitauzwa bidhaa zake. Mtoi na wengine wanaotofautina na wewe ni kwamba mfumo Kristu unaokena tatizo kwa vile waislam wameacha misingi fulani ya kiutawala kiasi cha kuwafanya wawe kama lonely gazelle, kila muislam anaishi kivyake ktk maendeleo ila kama kundi wanapolalamika huku kila mtu akiwa mjuaji na hakuna kiongozi wanayemheshimu zaidi ya hawa wana mihadhara. Hawa wana mihadhara wanaolinda himaya zao hawawafundishi utifu kwa viongozi wote halali hata wa miskiti tuu na si Bakwata wenye kuweza tiliwa shaka.

Sasa waislam wamejiachia kiasi cha kufanya mfumo Kristu uzibe nafasi liyopo wazi ktk nyanja zote. Hapo ndipo Mfumo Kristu unapoonekana kila mahali hadi katk maisha binafsi ya muislam. Sasa hawa wanamihadhara hawawezi toa tafsiri sahihi ya hali hiyo. Wao walichosoma mara ya mwisho toka kwa wanamihadhara wa kimataifa na si wasomi wa kimataifa ni kwamba watu wa magharibi waliiba elimu kwa waarabu. Ni ngumu huyu kuwa na maelezo ya hizi tofauti zaidi ya kutumia neno dhuluma. Mbaya na wasomi kama km nyie hamjaona jukumu lenu ktk kuondoa hizo kasoro.

Nimeshaona wachungaji wa Kilokole ambao hawakuandaliwa katk hayo na elimu yao si kubwa, wakipigwa stop na waumini wao wakati wakijaribu ongelea vitu wasivyovijua, wengi wenye akili timamu huwa wanawarefer waumini walio wazuri ktk hayo ili wawaeleze wengine kuhusu huo utaalamu nao wanaunganisha na mafundisho ya imani.

Kwa upande wa waislam kunakuwa na kukosa uaminifu, mtu kama Lipumba mwanasheria akiingia miskitini akipewa sifa ya elimu yake basi hayupo tayari udhi mtu kwa vile pia ana maslahi ya kisiasa basi hatoongea kitu ili kumkwaza mtu. Hapa lipaswa sema thoery za kweli za uchumi hata kama kuna sheikh karuka mipaka katika porojo bila kujenga licha ya kudhalilisha basi pangekuwa na faida kwa waumini, sheikh na yeye mwenyewe.

Kwa hiyo nawe inabidi uwe mdau, ili hizi nguvu za waislam ktk shari ziwe ktk uzalishaji. Sidhani kama kuna muislam keshawahi nyang'anywa kitu mkononi alichtafuta kwa jasho yake ili we masikini? Bila hivyo mtaona wakristu na maisha yao kila mahali hadi kwenye nyumba zenu(kama bidhaa za bakhresa) halafu mkipigwa fix kuwa huo mfumo ulipendelewa mnajikuta mmeamini. Huwezi soma chekechea kanisani,primary na secondary shule za kanisa au mkristu, ukaenda chuo cha kikristu huku ukipewa adftari yaliyotoka ktk nchi za kikristu kwa msaada wa wakristu wa huko, halafu ukatibia hospital ya kanisa na mtaalamu Padri, ukakamua alizeti ktk kituo cha kanisa. Pengine pia ukatibu wazazi wako ktk siku ya kutibu macho iliyoandaliwa na wazungu wamissionary walijitolea halfu kadhani utakosa nyumbani daftari lenye nembo ya taasisis ya Kikristu, miwani iliyotolewa na hawa jamaa, sheria za nchi nyingi duniani zimetengenezwa kwa influence za tafsiri ya mafundisho ya Yesu.

Watu hukombolewa kwa fikra na si zile futari za kina Kikwete na Manji. Muangalie Prof. Safari anavyojiamini. Kwa vile kachagua kuwa na life yenye kiasi kwa kila kitu, usomi wake una thamani kuliko wa Lipumba.
 
MM kabisa siafikiani na wewe katika mtazamo wako sio kwamba umekosea hila ndio mtazamo wako ambao umehitimisha kupitia kidini dini.

My school of thoughts is based on facts and reality of life either wewe huwe muislamu au wewe ni mkristo, the responsible organ of educating the social is the government. Lazima kuwe na right mechanism ya kuwaelimisha watu towards the facts of life, religious is not supposed to do so. If it does hayo ni matokeo ya kuambatanisha elimu ya dunia na religion, true christianity is better at providing that understanding so far but it includes Christianity reasoning in the process.

But a state has to better that responsibility for all sorts of groups and the education has to be centred on social facts, something our government has failed to do so. Hizi ndio sababu za kuzaliwa kwa dominant religous thinking. Tumeachia other institutions to teach the masses, what otherwise would have been the responsibility of the government, and organized groups are doing a better job to their followers (kama ni kweli based na ninayosoma humu ndani).

Lawama zinaenda directly kwa mawaziri wa elimu na serikali for their part to formulate a system that gives its citizen the right tools towards their social understanding. Dini ni dini na namna za kuishi ni namna za kuishi, kuingiza dini katika namna za kuishi tayari ni kuikosea jamii.

Kwa maana hiyo hata kama wakristo wamesoma zaidi na kujiona wao ni bora zaidi it is wrong (and in the long run it dont serve the national interest at best), hivyo bado hawajaelewa misingi ya kuheshimiana au kupigania misingi ya usawa hili kuepuka machafuko baina ya wasiosoma. Au hata waislamu ambao hawajasoma elimu dunia na wapo so conservative on their religious lines of thinking na wao wapo right based on their socialization influence.

Point hapa ni wanasiasa kuelewa the effects of education that favors the whole, badala ya kutumia ushamba wa kidini na mengineo kwenye kutengeneza sera za elimu bora ya mtanzania in general. Maana mipaka imeshachorwa kama lunde ni letu wenyewe na so far kinachoendelea ni cha mtoto ukiwaka moto kwa sababu ya kutoelewana kidini au kikabila huwe mkristo au muislamu ugenini wewe ni mkimbizi tu.

Kwa maana hiyo sorry but i must say kuwalaumu waislamu ni hoja dhaifu, lawama inatakiwa kwenda serikalini wao ndio watunga sera za elimu na mbinu za kuielimisha jamii in total hili kuweza kukabiliana na facts za maisha yao hili kuweza kuishi pamoja. Educational policies are supposed to aim towards understanding and respecting each others in our societies, those are important elements either ziwe zinatolewa shule zaki-islamu au za saints fulani. Hiyo ndio elimu inayohitajika na so far serikali imeshindwa tunga hiyo syllabus kwenye elimu yetu ya jamii. Inategemea tu common sense reasoning which is based on a person educational level.
 
Ni ukweli mtupu.

Wakati tunapata uhuru shule nyingi zilikuwa ni za Wakristo. Wamisionari wao walihakikisha kuwa popote penye Kanisa panakuwa na shule pamoja na hospitali. Waislamu walikuwa na shule chache sana. Haijalishi kuwa nia ya wakoloni wale ilikuwa watupe elimu ya kuweza kuwatumikia tu, lakini ilileta mwangaza kwa walioipata. Mwalimu Nyerere kwa kuliona hilo akaona kuwa wakristo wanaendelea kuanzisha shule mpya na waislamu hawana mpango. Akaona maono ya mbali kuwa taifa litakuwa na wasomi wakristo wenye nuru na waislamu wengi walioko gizani na akafanya maamuzi magumu ya kutaifisha shule zote za wakristo ilo na waislamu nao wasome.

Kwenye rangi, hayo ni maeneo ambayo watu wengi hawayaoni either kiukweli au kwa makusudi.
 
Afadhali kuna waislamu wengine wanaouona ukweli wa mambo; mimi nimetoka familia yenye mchanganyiko wa dini utadhani nyumbani kwetu ni umoja wa mataifa, kwahiyo tumejikuta tukiwa na mitazamo ya aina tofauti sana na watu wengine kuhusu dini.

Jambo la wazi ni kuwa dini zote ambazo viongozi wake ni wa kuokoteza tu, zimekuwa zinawatumia wafuasi wao vibaya kwa manufaa ya viongozi hao.

Kwetu hapa, viongozi wa kiislamu wamekuwa ni wa kwanza katika kuwatumikisha vibaya wafuasi wao kwa manufaa binafisi yao viongozi hao.
 
BAKWATA imekuwa ni kama taasisi ya CCM, wanamuweka wanaye taka wao. Lazima tupiganie bakwata kiwe chombo huru cha waislamu na tuweke viongozi wenye maono mapana tunao taka sisi sio ccm hii itasaidia kurejesha imani kwa BAKWATA.

Napendekeza Qualification ya kuongoza BAKWATA iwe ni PhD kwa kuangalia uwezo wa elimu akhera na elimu dunia lakini pia pamoja na uwezo wa kuongoza na kusimamia mambo. Chuo kikuu cha MUM kinaweza kusaidia kuratibu kupatikana wataalamu na watendaji wengine wa bakwata ambao nao kiwango cha chini cha kuanzia kiwe shahada moja na kuendelea.

Si ndo maana ponda alikua anataka kumngoa nyinyi wenyewe mkaanza kumzonga Ponda. Kumbe yeye hili kaisha liona. Akina Ponda ndo waliogundua hata baraza la mitihani limewanyonga waislam katika matokeo yao,,,, hili pia mwanzo mlimpinga. Sasa wewe toa njia mbadala unataka waibadilishaje hiyo bakwata wakati nyinyi wenyewe na serekali yenu mnaikumbatia,,,,
 
Mada hii ni muhimu sana; kwa sababu naamini yanayosemwa yanaweza kuwekwa kwa upande mwingine vile vile. Tatizo la Watanzania siyo Uislamu au Ukristu; kwa sababu tutake tusitake Waislamu wataendelea kuwepo na Wakristu wataendelea kuwepo na bila ya shaka wapo wenye imani nyingine vile vile. Ninaisoma makala hii na michango ya watu nikiwa na matumaini makubwa zaidi kuwa hatujapotea bado kama taifa.
 
Mwanangu Mohamedi Mtoi kwanza na kupongeza kwa kutoa mawazo mazito na yenye uoni wa mbali.

Nina ugomvi na watu wengi kutokana na kuwapa ukweli mchungu kuwa tatizo la nchi yetu si udini bali ujinga, umaskini na ufisadi. Kwa ambao tunazijua taasisi za kielimu za kiislam, ni kweli hazina mfumo wa kielimu wala mpangilio. Nenda pale AlHaramain utalia. Wanaajiri walimu wa kiislam ambao wengi wao hawalipwi vizuri. Watoto wanapewa mizigo ya masomo ya dini tena kwa lazima bila kutoa motisha wa kufanya hivyo.

Pili baada ya kukopngeza na kutoa machache, acha niongelee hili la mfumo-Kristo. Kwanza hakuna kitu kama hicho zaidi ya kuwa jinamizi linalowasumbua baadhi ya watu wanaotaka kutumia waislam kufikia malengo yao ya kisiasa. Nadhani waanzilishi wa mfumo huu ni akina profesa Kighoma Malima.

Ni bahati mbaya kuwa vijana wengi wa kiislam walioelimika, ima hawataki au wanaogopa au hawajihangaishi kutafuta ukweli. Wengi wa wasomi wa aina ya Mohamed Said wameshikilia vita ya kutengeneza wakimlaumu marehem Mwalimu Nyerere. Hata baada ya kufa hawampi nafasi wakafikiri kama watu hai zaidi ya kufikiri kwa jazba na kuelekea nyuma. Ukiwa na wasomi kama Mohamed Said wenye kinyongo na chongo utegemee nini mwanangu?

Mwisho kabisa ni kwamba tunapaswa kuwaelimisha watanzania kuwa tulipodai uhuru tuliudai kama watanzania na si waislam wala wakristo bali watanzania. Uislam na Ukristo vimeletwa lakini utanzania wetu hakuletwa. Isitoshe kwa umaskini tulio nao kama tutaanza kuchinjana wenyewe tutakufa kwa njaa na si matundu ya risasi wala mapanga. Je ni wangapi wanaliona hili?

Nakupongeza tena mwanangu Mohamed Mtoi kwa kuja na fikra mbadala.

Hapo kwenye nyekundu nakubaliana na wewe 100%
 
Asha Dii na Mohamed Mtoi asanteni sana wanangu mmenipa matumaini sana. Mimi ni mkrisot mtu mzima nina marafiki ndugu na majirani ambao ni waislam. Ninawapenda na ninashirikiana nao vizuri sana. Matukio yaliyotokea yamenipa simanzi kubwa mno lakini hoja zenu zilizojaa hekima na busara zimenirudishia matumaini makubwa. Ninaamini wote wenye mapenzi mema na nchi yetu wamezisoma na watazitafakari ikiwa ni pamoja na mimi ili tuweze kusaidiana kama watanzania kutafuta suluhu ya tatizo lililopo na mengine yatakayojitokeza kwa upendo na amani. Hakika nyie ni taa na chumvi kwa jamii yetu. Mmeonyesha njia na kutoa changamoto zenye mashiko. Mnastahili pongezi na kuungwa mkono na watanzania wote bila kujali imani ya mtu aliyo nayo. Mungu awabariki sana. Mungu ibariki Tanzania
 
Mkuu Nicholas;

Rejea post yako #30 nimekupata vilivyo binafsi kama kijana wa kiisalamu naijiamini nilivyo; pili sishabikii tafrani za kidini kwenye mzingira yangu ya kazi nafanya na waislamu; wakristo, wayahudi na wapo ambao haamini Mungu na hawataki kumsikia; je labda tujiulize hawa ambao hawataki kusikia kuwepo kwa Mungu tatizo lao nii nini? Argument yao hafifu lakini ina uzito "if the so called God exist then all these wars, killings; corruptions; tornados, hurricanes you mention the rest would have never happened".

Hiyo ndiyo argument yao kwa imani yangu sikubaliani nao ila kwa misingi ya kuheshimiana nakubaliana nao; Hakuna mafundisho yanayosisitiza dhuluma ila watu waliopewa jukumu la kusisimamia misingi ya dini ndiyo wanaoharibu kwa faida zao binafsi.

Turudi kwenye tatizo la Tanzania historia ya matatizo ya kielimu yalikuwapo tangu zama za ukoloni; wakristo walijiendesha zaidi kama taasisi; na walitumia sheria zilizopo kujinufaisha kieleimu na kiuchumi; hilo tatizo lipo hadi leo; labda kwa kugusia hizi MoU kati ya taasisi za makanisa na serikali ni kwa manufaa ya watanzania au makanisa?

Wengi mtahoji serikali ilianzisha BAKWATA kwa lengo kuwasaidia waislamu nakubaliana na hilo je BAKWATA ya leo ipo kuwasaidia waislamu au ni kikundi cha mashekhe wachache wanaojinufaisha na chombo hicho; BAKWATA haiwakilishi mawazo ya waislamu walio wengi mimi ni mmoja wapo wa waslamu hao; BAKWATA imekuwa kizingiti kila inapoanzishwa taasisi ya kiislamu yenye lengo la kumkomboa Muislamu; kama utakumbuka miaka ya 1982 wakati Ansaar Sunn wanaingia Tanzania walipigwa vita sana na BAKWATA; cha ajabu leo hii Ansaar wanafanya vizuri sana kwenye nyanja ya elimu shule zao karibu zote zinafanya vizuri kitaifa; niligusia yapo matatizo ambayo kama waislamu tumechangia na yapo ambayo kama serikali kwa kiasi kikubwa imechangia; mojawapo ni hizi MoU; labda nikuulize kulikuwa na ulazima gani kwa serikali kuzipa taasisi za kidini mamilioni ya pesa wakati hospitali zinazoendeshwa na taasisi hizo hazitoi huduma zake bure kwa wananchi?

Mkuu tusijadili kama wauza njugu kama anavyotaka kulazimisha Ph.d MM hii hoja ni nzito.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Lazima kuwe na right mechanism ya kuwaelimisha watu towards the facts of life, religious is not supposed to do so.

1. Jee, una maana gani na kauli yako hapo juu? Tupe mfano wa "right mechanism kuwaelimisha watu towards the facts of life, religious is not supposed to do so"

2. "If [religious] [sic?] does hayo ni matokeo ya kuambatanisha elimu ya dunia na religion, true christianity is better at providing that understanding so far but it includes Christianity reasoning in the process"

3. "... a state has to better that responsibility for all sorts of groups and the education has to be centred on social facts". How and to what extent has the government "failed to do so" na ni namna gani "Hizi ndio sababu za kuzaliwa kwa dominant religous thinking"?

4. Una maanisha nini na kauli yako ya
"dominant religous thinking"?
Tafadhali tupatie mifano halisi.

5. "Tumeachia other institutions to teach the masses, what otherwise would have been the responsibility of the government, and organized groups are doing a better job to their followers (kama ni kweli based na ninayosoma humu ndani)." Jee, ni institutions gani hizo unazodai "are doing a better job to their followers", na kwa kiwango gani? Na jee, una ushahidi wowote kuhusu hili?

6.
"Lawama zinaenda directly kwa mawaziri wa elimu na serikali for their part to formulate a system that gives its citizen the right tools towards their social understanding." Jee una maana gani na "right tools toward their social understanding"?
Hebu tupatie mifano.

7.
"Dini ni dini na namna za kuishi ni namna za kuishi, kuingiza dini katika namna za kuishi ni kuikosea jamii."
Hebu tuwekee mifano ya "kuingiza dini katika namna za kuishi", huku ukielezea sababu zako kwamba ni "tayari ni kuikosea jamii"

8.
"Kwa maana hiyo hata kama wakristo wamesoma zaidi na kujiona wao ni bora zaidi it is wrong (and in the long run it dont serve the national interest at best)"
Tafadhali fafanua jinsi gani Wakristo kusoma zaidi "is wrong" pamoja na kutufahamisha unamaanisha nini haswa kwa kauli yako kwamba "[Wakristo] kujiona wao ni bora zaidi it is wrong".

9.
"hivyo bado hawajaelewa misingi ya kuheshimiana au kupigania misingi ya usawa hili kuepuka machafuko baina ya wasiosoma. Au hata waislamu ambao hawajasoma elimu dunia na wapo so conservative on their religious lines of thinking na wao wapo right based on their socialization influence."
Kwa hiyo unategemea Wakristo wote waliosoma wawe pia wamepitia kozi ya "misingi ya kuheshimiana au kupigania misingi ya usawa hili kuepuka machafuko baina ya wasiosoma"? Jee, hii kozi inatolewa na chuo gani, na kwa vigezo vipi?

10. Tuwekee mifano halisi ya "the effects of education that favors the whole" na isitoshe maana ya "ushamba wa kidini na mengineo kwenye kutengeneza sera za elimu bora ya mtanzania in general."

11.
"What educational policies and programmes are there to respect each others are important either ziwe zinatolewa shule zaki-islamu au za saints fulani, hiyo ndio elimu inayohitajika na so far serikali imeshindwa tunga hiyo syllabus kwenye elimu yetu ya jamii. Inategemea tu common sense reasoning which is based on a person eduacational level."
Kama nimekuelewa vizuri hapo juu, ni kweli kwamba una advocate sera tofauti za elimu kwa Waislamu na Wakristo kwa lengo pekee likiwa "to espect each others"? Hebu tupe mfano wa nchi yoyote duniani iliyofanikiwa kutunga sera ya elimu "tailor made" kuendana na matabaka ya dini, kiuchumi, kikabila etc katika jamii?
 
Mada hii ni muhimu sana; kwa sababu naamini yanayosemwa yanaweza kuwekwa kwa upande mwingine vile vile. Tatizo la Watanzania siyo Uislamu au Ukristu; kwa sababu tutake tusitake Waislamu wataendelea kuwepo na Wakristu wataendelea kuwepo na bila ya shaka wapo wenye imani nyingine vile vile. Ninaisoma makala hii na michango ya watu nikiwa na matumaini makubwa zaidi kuwa hatujapotea bado kama taifa.

Mwanakijiji tatizo si Uislamu wala Ukristo tatizo ni mfumo hizi MoU zina manufaa gani kwa mtanzania wa kawaida? Hata US taasisi za kidini za kanisa Katoliki zilikuwa zinapewa pesa na serikali za jimbo na serikali kuu kwa lengo la kuboresha elimu na huduma za afya; watu wengi walifungua kesi mahakamani kuhoji kwanini taasisi za kikatoliki zinapewa pesa kwa misingi na madhumuni gani?

Matokeo ya kesi hizo waliofungua walishinda taasisi za Kikatoliki leo zinajitafutia njia nyingine za kutafuta pesa kwa ajili ya kuendesha shule na mahospitali yao; nadhani hilo halina tofauti na wanacholilia Waisalmu wa Tanzania; na ukiangalia kwa undani zaidi wapo wakristu wanaathirika na mfumo uliopo tukio la juzi Sumbawanga la wanakijiji kuchoma mali za kanisa ni moja wapo laiti tukio hilo lingetokea Pangani wahusika wangeadai Waislamu wamechoma moto mali za kanisa.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom