Gaijin
JF-Expert Member
- Aug 21, 2007
- 11,812
- 5,284
Anaweza kuwa amekosea kujieleza, lakini kimsingi tunahitaji uwiano wa madaktari bingwa na madaktari wa ngazi za chini
Katika nchi ambayo dispensary nyingi za vijijini hazina hata maBwana Afya, kuwekeza kwenye madaktari bingwa pekee hakuna maana kwa sababu watu wengi mno wanakufa kwa maradhi ya kawaida ambayo yangesaidiwa kwa kuwepo madaktari wa ngazi ya chini.
Pia, bila ya kuwepo kwa madktari wa ngazi ya chini, wagonjwa hawataweza kuandikiwa kuonana na daktari bingwa, hivyo huduma ya hawa madaktari bingwa itakuwa kwa wachache zaidi
Kwa hiyo hapa ni suala la uwiano. Tunahitaji kusomesha madaktari wa ngazi ya chini wa ngapi kwa kila daktari bingwa mmoja?