Sasa napata sababu kwa nini serikali haishtuki hata madaktari wakigoma, na pia napata maana ya kauli ya Mizengo Pinda ya Liwalo na Liwe.
Waziri mwenye dhamana ya afya Hussein Mwinyi akihojiwa BBC leo asubuhi na mtangazaji wa kipindi cha haba na haba Noel Mwakalindile ambaye alitaka kujua kauli ya serikali juu ya upungufu wa madaktari bingwa, waziri akasema kwa sasa focus yao kubwa ni kusomesha wataalamu wa afya wa ngazi ya cheti na diploma kwa kuwa wao ndio wanahitajika zaidi. Amesema kusomesha daktari bingwa ni gharama kubwa kwani daktari bingwa anasoma miaka minne mpaka mitano. Kwanza huu ni uzushi, vyuo vyote tanzania madaktari bingwa wa fani zote wanasoma kwa miaka mitatu tu, isipokuwa KCMC ambako wanasoma kwa miaka minne. Hakuna hata chuo kimoja ambacho daktari bingwa anasoma kwa miaka mitano. Hii inanipa wasiwasi kuona kuwa waziri wetu hajui hata madaktari bingwa wanasoma miaka mingapi, Je waziri wa aina hii anawezaje kutuambia anajua gharama ya kumsomesha huyu daktari bingwa?
Hivi kweli huduma bora za afya Tanzania zitaimarika kwa kusomesha maafisa tabibu? Hii serikali inayojali afya ya watu wake inawezaje kweli kuona gharama kusomesha madaktari bingwa na badala yake kusomesha maafisa tabibu. Au inatumia ujinga wa watanzania kwamba mtu yeyote anaevaa koti jeupe ni daktari na hivyo wananchi watajua serikali yao imewapelekea madaktari wakati ni maafisa tabibu ambao tiba yao ni ya huduma ya kwanza?
Nchini kenya kwa sasa madaktari bingwa wako katika ngazi ya hospitali ya wilaya, na wanamkakati wa kuhakikisha kwamba kila mtu anatibiwa na daktari bingwa ili apate tiba ya uhakika na hivyo afya yake kuboreka. Kwetu hata hospitali za rufaa hazina madaktari bingwa wa kutosha achana na hospitali za mikoa ambazo zenye bahati zina bingwa mmoja tu, na tunawaza kuongeza maafisa tabibu. Hivi kwa nini nchi hii badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma?
No wonder mwaka jana walipunguza budget ya kusomesha madaktari bingwa na hata wale waliopata udahili walikosa udhamini, nilijua serikali haina pesa kumbe kwa mtazamo wao daktari bingwa si muhimu. Namuomba Hussein Mwinyi akiumwa awe wa kwanza kwenda kwa afisa tabibu kutibiwa aone kama hatapewa ppf injection hata kama ana malaria. Waziri Mwinyi ufikiri kwanza kabla ya kukejeli watanzania.
Naomba kuwakilisha.
HIvi kweli kasema hvyo ua umemwelewa hivyo?
Kama kasema hivyo basi yale ninayofikiria juu yake ni sahihi.