Hawa ndio freemason?

Mbilimbili

Senior Member
Mar 17, 2012
172
19
Habari wana jamvi, natumaini mmeshinda vyema. Iko hivi kuna dada mmoja simfaham kiundani, tumefahamiana kwenye mitandao ya kijamii. Yeye anasema yupo Senegal kwenye kambi ya wakimbizi, ila anachotaka kunifanyia naona sivyo. Amenieleza wazazi wake walifariki kutokana na vurugu zilizokuwapo Sudan, kwa hiyo wameacha donge nono la U$D 4.5M kwenye account yao iliyopo London. Sasa kinachonipa wasiwasi ni kwamba amenipa details zote za kufanya Transfer ya hiyo hela, iingizwe kwenye account yangu. Naomba mawazo yenu wadau, sababu nadhani wanataka kuniingiza na mimi kwenye huu mtandao wa kishetani.
 
hiyo ni spam, kwenye email yako.. many times huwa ni mahacker..!!!! wanajaribu kukuingiza mjini..!!! watchout Mbilimbili
 
Last edited by a moderator:
Matapeli hao hata mimi walishawahi kunitumia na maelezo ni hayohayo............na rafiki zangu wawili vilevile.
Lengo lao ukishaonekana kuwakubalia watajifanya wanamuomba lawyer akusaidie then ata-demand fee kidogo na wewe utadhani kweli kwa sababu ni amount ndogo lakini baadaye watakupiga kibomu tena na tena na tena.

Sikuwahi kuwajibu ila nilipoona hivyo nika-google jina lake huyo dada ikatokea website inayohusiana na mambo ya fraud wakanipa hayo maelezo hapo juu! Hakuna freemason hapo ni utapeli tu
 
Huyo si ni yule mtoto wa Generali Coroma? Ni hacker huyo atakuspam . Piga chini wewe hiyo mtu ni balaa. Badae atakwambia kuwa anatunzwa na Padre mmoja hivi kambini na baba yake aliacha mamilioni mengi kwa benki. Mwambie "I'm not interested in you"
 
Huyo si ni yule mtoto wa Generali Coroma? Ni hacker huyo atakuspam . Piga chini wewe hiyo mtu ni balaa. Badae atakwambia kuwa anatunzwa na Padre mmoja hivi kambini na baba yake aliacha mamilioni mengi kwa benki. Mwambie "I'm not interested in you"

hilo la Padre ashaniambia.
 
Nina nakala 7 za w2 tofauti walio ni2mia email kama hyo,kama co candy huyo atakua florencia ndo wasumbufu xana ktk fb.ukitaka kuamini search jina la huyo manager wa bank uone result.
 
HAWANA JIPYA HAO, WAPO WENG KWEL MITANDAON! HATA MIM NMEMIT NAO SANA KTK MTANDAO www.waplog.com!BT NLIWASHIT, BT WAKO VZURI KIUTAPELI UTADHANI KWELI!Ukikaa vbaya inakla kwako
 
ANGALIZO:Ukitaka kuwajua HACKERS nenda GOOGLE andika email hiyo then utapata uhakika kuwa hao ni matapeli. KUMBUKENI hakuna mafanikio rahisi humu duniani so msipende vya bwerere wandugu fanyeni kazi
 
ANGALIZO:Ukitaka kuwajua HACKERS nenda GOOGLE andika email hiyo then utapata uhakika kuwa hao ni matapeli. KUMBUKENI hakuna mafanikio rahisi humu duniani so msipende vya bwerere wandugu fanyeni kazi

na kweli hapa kazi tu.
 
bado utapeli wa aina hii unaendelea?

Mkuu hao ni wezi, watakwambia umtumie hela kwa ajili ya chargesili helazije kwako, ukituma tu umeumia hutomsikia tena....
 
Hivi utapeli huu bado unaendelea tuu!!
Wana JF nawakumbusha tena, tusiwe tunapenda short cut katika mafanikio kwani mara nyingi mwisho wake huwa ni mbaya.
 
Dah hata mimi waliniambia nimeshinda bilioni moja na milioni mia nne za tanzania wakataka nitume hela ya kuzi transfer ama kuzisafirisha nikagoma nikaachana nao mana nilijua ni walewale matapeli
 
Back
Top Bottom