Hawa Celebrity Wako Wapi Siku Hizi?

GP, Badi Bakule aliimba pia Mwenye kwetu kwaheri (sina hakika na title)
Mwenye kwetu kwaheri,
Kwa heri x2 nawatakia maisha mema
Kwa heri x2 nimeshachoshwa na masimango
Mwana masikini eeh!
Best BAK, plz fanya mambo yako
 
Last edited by a moderator:
hebu jikumbushe wimbo wao maarufu enzi hizo wa MTEGEMEA CHA NDUGU:

intro.....

chandeeeeeee, asubuhi kumekucha kumepambazuka Chandeeeee,
Chandeeeee eeh, tuamke kumekucha tukajitafutie riziki yetuu,
Ooh ooh Chandeeee,
aah Shabani Bakule, mamaa leticia Kato, sema na Adam, Omar Baraka, Almas,
Chande, japokua wanasema riziki haivutwi kwa kamba Chande,
lakini usipoitafuta huwezi kupata, kwa vile mafanikio hayaji ndoto OOH,
aaah mwenda pole, Mr K.H Ngaluma, Kocha wa dunia,

Chande, japokua wanasema riziki haivutwi kwa kamba Chande,
lakini usipoitafuta huwezi kupata, kwa vile mafanikio hayaji ndoto,

sema saaana lakini utakua mpole ghafla,
maisha mtego, ukisepetuka umenasa,
maisha popote, maisha mahesabu,

Chorus,,,,,,,,,

kazi hutaki kufanya, kwa vile kaka ana mali,
elewa mtumaini cha ndugu hufa masikini,
kazi hutaki kufanya, kwa vile kaka ana mali,
elewa mtumaini cha ndugu hufa masikini,

[BADI BAKULE,,,,,,,,,]

oooh, Badi mi nasema, inakupasa uelewe ya kuwa umri haurudi nyuma,
miaka inazidi kwenda mbele maisha ni mapambano,
ona wenzetu wanavyo yatafuta maisha chande,kila kunapokucha pilikapilika haziishi,
wengine maofisini, wakulima mashambani,
na wafanya biashara nao pilikapilika,
wengine ujerumani, wengine south africa, na wengine america katika kujitafutia aaah aaah,
ooh mama leleee, muheshimiwa Richard Ndassa, mueleze Chande ajitafutie kama sisi eeh,
John Badi na Badi Bakule mueleze Chande ajitafutie kama sisi eeh,
na Baraka Musilwa mueleze Chande ajitafutie kama sisi,
kila kunapokucha pilikapilika haziishi, za kutafuta maisha yetu ya leo na kesho,
usipojitafutia hakuna wa kukutafutia,
kwa vile maisha ya sasa ni vuta nikuvute kila mmoja huvutia kwake (ya muamba ngoma), ooh mama iyeee,
utakuja kumulilia nani eeh, wakati umekwishapinda mgongo ooh, na nguvu za kutafuta tena huna,
ukitazama nyuma mzigo mkubwa wa familia eeh, we bwana umekuelemea,

[RASHIDI MWENZINGO,,,,,,,,,,,]

yoyooo, rafiki Chande ananishangaza sana,
yoyooo, rafiki Chande ananihuzunisha sana eeh,
kazi nyingi anazozipata anashindwa kufanya, anategemea cha ndugu wakati uwezo hana iyoyoyo kaka,
kazi yake ni kula kulala kwa kaka yake Mwenzingo,
kazi yake ni kula kulala kwa mjomba wake Bakule,
kazi yake ni kula kulala kwa dada yake Amina,
kazi yake ni kula kulala kwa shangazi Asha Baraka, yoyoo Chande yatakushinda kaka,

[BADI BAKULE,,,,,,,,,]

aah iyoyoyoo eeh yatakushinda Chande,

[AMINA NGALUMA,,,,,,,,,]

hata sisi dadazako, tunakushangaa kwa tabia yako,
unavyojiendekeza kwa kupenda vya bwerereeeee, aibu eeeh


[MUUMIN MWINJUMA,,,,,,,,,]

sure eeh,
ooh ooh Chande weeh,
ooh ooh Chande eeh,
wanihuzunisha kwa vitendo vyako rafiki yangu,
nimesikia kazi yako ni kushinda sebuleni tu,,,, wangoja kuitwa
mara ooh Chande chai tayari huku,,,,, wangoja kuitwa
mchana unauliza shemeji lunchi imewiva,,, alaah,,,,,,,, wangoja kuitwa,
hata kazi ndogo ndogo zinakushinda Chande,
hata jite riziki kidogo ana afadhali,
wacha kutuliza boli, chakalika ndugu yangu, changamkia tenda,

Chorus,,,,,,,,,

kazi hutaki kufanya, kwa vile kaka ana mali,
elewa mtumaini cha ndugu hufa masikini,
kazi hutaki kufanya, kwa vile kaka ana mali,
elewa mtumaini cha ndugu hufa masikini,


,,,,,,,,,

kitu kinaitwa CHANDE mkuu!
 
GP, Badi Bakule aliimba pia Mwenye kwetu kwaheri (sina hakika na title)
Mwenye kwetu kwaheri,
Kwa heri x2 nawatakia maisha mema
Kwa heri x2 nimeshachoshwa na masimango
Mwana masikini eeh!
Best BAK, plz fanya mambo yako

hapana mkuu King'asti,
huo wimbo uliimbwa na WAZIRI SONYO
 
Last edited by a moderator:
nimemuona badi bakule leo,kwa kifupi amechoka kimaisha anapiga live band kibaha maili moja kiteshe band
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom