Hawa AIRTEL vipi

Mulangila Mukuru

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,945
724
Jamani naomba mnisaidie labda nipo mbali na media, nilikuwa na nimejiunga na huduma ya Airtel ya 400MB ambayo huwa naitumia siku zote, ilipofika jana ikaisha leo saa 10 jioni nikajiunga tena kwa utaratibu uleule baada ya kuona nimeshapewa 400MB nikafungua page ya yahoo nikaanza kuatach mafaili flani wakati nataka kutuma net ikakata kuangalia salio najikuta nina 0MB balance nikashangaa maana nilikua sijamaliza hata nusu saa na sijadownload chochote.

Nilipouliza uduma kwa wateja nikaambiwa kujiunga ni mara moja kwa mwezi na mwezi haujaisha toka nijiunge.ninavyojua mimi huduma ya 400MB ni no limit sasa je hii kitu ni kweli au wamenichakachua? Naogopa kujiunga tena nina wasiwasi na waudumu wa airtel
Nawasilisha.
 
Jamani naomba mnisaidie labda nipo mbali na media,nilikuwa na nimejiunga na huduma ya Airtel ya 400MB ambayo huwa naitumia siku zote,ilipofika jana ikaisha leo saa 10 jioni nikajiunga tena kwa utaratibu uleule baada ya kuona nimeshapewa 400MB nikafungua page ya yahoo nakaanza kuatach mafaili flani wakati nataka kutuma net ikakata kuangalia salio najikuta nina 0MB balance nikashangaa maana nilikua sjamaliza hata nusu saa na sijadownload chochote,
nilipouliza uduma kwa wateja nikaambiwa kujiunga ni mara moja kwa mwezi na mwezi haujaisha toka nijiunge.ninavyojua mimi huduma ya 400MB ni no limit sasa je hii kitu ni kweli au wamenichakachua? Naogopa kujiunga tena nina wasiwasi na waudumu wa airtel
Nawasilisha.
Mkuu hapo kwenye Red....Si kweli.wanacho kupa ni 400MB tu.Kwahiyo kama uta'download''/upload file zikifika hiyo limit(400mb) tu wanakukatia regardless umetumia dk15 au less.
 
Mkuu hapo kwenye Red....Si kweli.wanacho kupa ni 400MB tu.Kwahiyo kama uta'download''/upload file zikifika hiyo limit(400mb) tu wanakukatia regardless umetumia dk15 au less.

nadhan atakuwa anamaanisha 'no limit' ya mara ngapi unajiunga,na ni kwel,hata ikiisha siku hyo hyo unaweza ukasubscribe upya co lazma mwez uishe..
 
nadhan atakuwa anamaanisha 'no limit' ya mara ngapi unajiunga,na ni kwel,hata ikiisha siku hyo hyo unaweza ukasubscribe upya co lazma mwez uishe..

We umenipata vizuri mkuu ndo ninchomaanisha na huwa nafanya hivyo mara nyingi nashangaa leo kuambiwa eti mpk mwezi uishe ndo maana nasema hawa waudumu nao sijui kma wako compitent na kazi yao.
 
We umenipata vizuri mkuu ndo ninchomaanisha na huwa nafanya hivyo mara nyingi nashangaa leo kuambiwa eti mpk mwezi uishe ndo maana nasema hawa waudumu nao sijui kma wako compitent na kazi yao.
Wakimbie hao Airtel...ndugu yangu if that is the case.
 
Inaonekana ww ulipoambiwa ujibu yes ww sijui haukuona na ukapotezea ss ian maana haukujiunga na bundle so walichofanya wao ni kufyeka pesa iliyokuwepo.
 
Mkuu nafikiri umejichanganya tu kwenye kujiunga...labda ulianza kuattach kabla hujacomfirm ama umeattach zaidi ya 400 MB...na hiyo ya kwamba ikiisha kabla ya mwezi huwezi kujiunga tena sina hakika km ni sahihi kwa kua nimekua mteja mwandamizi wa Zain na Sasa Air Tell ila hii ni case mpya! Ni mara moja waliwahi kutukata kimakosa of which walikuja kurudisha vifurushi walivyotukata kimakosa!
 
Mpaka sasa ninazo msg zao mbili ya kukaribishwa kujiunga na 400MB na ya kupewa hizo 400MB hiyo hela si tatizo sana tatizo ni majibu niliyowa na customer care kwamba kujiunga ni mara moja kwa mwezi na si unlimited ila poa tu ngoja nijaribu tena naona ka sim kanachemka.
 
Sisi lini tutapata kampuni ya simu ya Tanzania? Sudan walianzisha Mobitel miaka ya 90 mwanzoni, nadhani kwa sasa ndio Tigo? ya Sudan, Voda ni Vodafone ya Uingereza kupitia Souzi, Zantel ya Etisalat ya Dubai, Airtel ya mzee Bharti wa India, sisi bado simu ya mezani zipo au nazo zimefungwa? SafariCom ya mabosi wetu Kenya ni kampuni kubwa kuliko makampuni yooote Afrika mashariki na kati na idadi ya watu wao ni ndogo... kuna jambo
 
nafkiri majibu aliyotoa mkuu mikatabafeki yafanyie risachi. wengi hapa tunajisahau.
hakikisha unajibu neno ndiyo na si ndio au kwa urahisi jiibu neno Yes
 
sometimes hawa zain wanazingua, unaweza ukanunua dk 15 au 45 then ukaongea sekunde 20 ukacheki salio lako ukakuta umekatwa charge na ukiangalia dk zako unakuta una 0,cheki pia aina ya anti-virus nyingine zinaji-update automatically, angalia na auto updates weka off, au ukiwapigia waelezee vizuri uwaulize tatizo watakusaidia mkuu
 
Ndg yangu achana na watu wa customer care kabisa, hasa wa airtel ndo hamna kitu kabisaaa! hilo jibu wlilokupa c la kweli, mb 400 kwa shs 2500 haina limit ya kujiunga, ukimaliza hizo mb 400 unajiunga tena, me nilikwisha wahi fanya hivyo na cjasikia tangazo lao kuhusu mabadiliko hayo ila watu wa cc wa airtel ni "upepo" usiwaamini sana.
 
Hawa jamaa ni wezi hakuna mfano.Nina kawaida ya kujiunga na kifurushi cha DATASIKU kinachokupa uwezo wa kutumia MB 20 kwa saa 24,zikiisha wanakutumia meseji ya kuwa MB zako zimeisha na unaweza kulipia sh 40 kila MB badala ya 150 au wanakupa option ya kujiunga tena kwa masharti yaleyale ya kukatwa sh 500 kwa MB 20.
Kwakua nimekua nikifanya hivyo mara nyingi,nimezoea naweza kujiunga saa 2 asubuhi ikaisha saa 6 mchana nikajiunga tena which means masaa 24 yanaisha saa sita ya siku inayofuta.Ndani ya hayo masaa 24 unaweza kujiunga hata mara 10.Nakumbuka nilishawahi kujiunga mara 4 ndani ya masaa 24.
Tatizo nililoliona na ambalo naita ni wizi,ni kwamba kwa hizi siku za karibuni nimekua najiunga asubuhi na inapofika jioni kifurushi kinaisha so inabidi nijiunge tena,Jana nilijiunga saa mbili na saa kumi jioni halafu nikapata dharura sikukitumia kifurushi changu.Nikajua kwa kuwa naruhusiwa kukitumia kwa masaa 24,kingemalizika muda wake leo saa 10 jioni.
Ajabu ni kwamba nilipowasha komputa tu saa 2 asubuhi nikapata msg kuwa kifurushi changu kimeisha muda wake wakati nilikiweka saa kumi na sijtumia.
Nimekasirika sana ikabidi niwapigie kuwauliza kama kifurushi kinaniruhusu kukitumia kwa masaa 24 kwanini kimeisha baada ya masaa 12?Jibu nililopewa ni kwamba hiyo ni lugha ya biashara,masaa 24 yanaisha pale ulipochagua kifurushi cha kwanza kwa siku hiyo.Kwakweli nimechukia kupita maelezo maana huu ni wizi wa mchana.Wanachokifanya ni tofauti na wanachotuambia.
Mimi nawatahadharisha tu,kwamba kila jambo lina mwisho na kuna siku PATACHIMBIKA.
 
Mi mwenyewe kifurushi changu cha MB 400 kimeisha, bt valididy yake bado, so nikijiunga tena naletewa msg kwamba ushajiunga huruhusiwi kujiunga tena hadi mwezi uishe, nimechoka!! Inabidi nisubiri hadi siku 8 ziishe
 
Back
Top Bottom