Hausigeli akutwa akiwanga kwa tajiri

Maswali ni mengi kuhusu jinsi ya kukomesha utumwa wa kisasa (aka ma-housegirl)
Hivi hakuna sheria inayosema huwezi kumuajiri mtoto chini ya miaka 18? Kama ipo kwanini chama cha mawakili wakike haki chukui hatua kutetea haki za wanyonge kama haka kabinti? Kabla ya ku-deal na uchawi huyo aliyeajiri mtoto wa miaka 15 anatakiwa afunguliwe mashitaka.

Sheria ya ajira inaruhusu watoto kuanzia miaka 15 kuajiriwa mradi zisiwe ajira mbaya kufuatana na Mkataba wa ILO on worst forms of child labour.Je kazi ya uhausigel ni ajira mbaya kufuatana na sheria/ILO Convention? Utakuta kuna ombwe na utata hapo kwa vile hata watunga sheria, watekelezaji wote wanaajiri hausgeli!
 
....Huyu mtoto inawezekana ameonewa au ni kweli amefanya huo uchawi.Baadhi ya hawa wasichana wa kazi wana vituko vyao jamani.
....Kuna binti alikuwa msaidizi wa kazi kwa sista, huyu binti naye alikuwa anaamini sana nguvu za giza......alikuwa amevaa vitu vya ajabu nadhani wanaita hirizi. Sista ni mtu wa imani sana, alivyoletewa msichana akawa anaenda naye kanisani.Siku moja kukatokea kitu cha jabu sana, kanisani kulikuwa na maombi ya nguvu, yule binti akawa kama anapiga makelele na kuongea vitu vya ajabu.Mchungaji akamuuliza matatizo yake, ndipo hapo yule binti akaelezea jinsi alivyokuwa analindwa na nguvu za giza na kwamba amevaa hirizi kiunoni.

Alisema kwamba kuna hirizi alipewa na baba yake huko kijijini ni kinga inamlinda usiku na kuwaona wachawi. Mchungaji alimuombea yule binti na baada ya maombi yule binti akaamua kumpokea Yesu na kukubali zile hirizi zichomwe moto. Hadi leo amekuwa ni msichana mzuri na anaendelea kumsaidia sista.

.........Inawezekana kweli huyo binti alikuwa naye na nguvu za giza, lakini walichofanya hao kumpeleka polisi wala sio vizuri. Wangemuweka kwenye maombi na hizo nguvu za giza zote zingeteketea kwa jina la Yesu na yule binti angebaki tu hapo kwao kuendelea na kazi.


unaona tofauti hapo pretty!!alivyofanya sista inashawishi kabisa kuamini kwani hivyo ndivyo watu wanaomuamini mungu wanapaswa kufanya.binti kaombewa na bado anaendelea kuishi vizuri na sista..lkn hawa wenzetu wao wamemnyima hata nauli eti ya kurudia kwao..unapata hiyo picha hapo!!mie ningewaamni kama wangemuombea hizo nguvu wanazodai za kichawi zimtoke kisha kama walokole waendelee kuishi naye vizuri wakimuongoza kuwa imara ktk kumtumainia mungu!!!
inawezekanaje mtu aliyeokoka na mwenye kumtumainia mungu kiasi cha kuoneshwa kuwa mtoto ni mchawi amnyime mtoto hata nauli ya kurudia nyumbani!!ampeleke polisi!!kama kweli wameokoka wangejua hiyo si vita ya kumalizwa kwa kupelekana polisi bali ni vita ya kumuombea binti(kama kweli) ili wamkomboe kutoka ktk nguvu za shetani na kutomfukuza bali kuendelea kuishi naye ili akue kiroho.kama wanaweza kuomba na kuoneshwa uchawi wangeweza pia kuomba hizo nguvu zikaisha(kama kweli anazo).hapo kuna walakini aisee,watu waliookoka hawawezi kuwafanyia binadamu wengine kama hii familia ilivyomfanyia huyu mtoto..mie ningekua hapo karibu na mie ningepelekwa central wapendwa maana nisigekubali kuondoka bila kujua huyo mtoto hachomwi moto kwa kutuhumiwa uchawi kumbe labda ukweli wa mambo ni dhuluma na roho mbaya za waajiri wake.uonevu kwa watoto wadogo kwangu ni jambo serious sana na inanikosesha raha.sipendi kabisa.basi tu ndio ndio jamii yetu ilivyo!!!
 
Hii tabia ya kuajiri watoto wadogo na kuwanyanyasa lazima ikomeshwe, sasa kumbe wana binti wa miaka 25, mtoto wa 15 wa nini? Hivi tumekuwa wavivu kiasi hiki? Tena usikute mama mwenye nyumba hata kazi hana!!!
 
jamani tudumishe kusali katika familia zetu nimefikiria sana housegirl wangu mpaka naogopa. Mungu nisaidie

Eeeh!

Ndio mnaona hasara ya kulala na kumka kama mbuzi eeh!

Jamani hali si nzuri na dunia ya sasa lolote linaweza kuwa kama la huyu binti!

Mie nishakumbwa na swala la nguo za jr kupotea ghafala zikiwa zimeanikwa ndani ya nyumba!

Lakini kwa kuwa namwamini Mungu wa Mbingu na Nchi; nilimwomba yeye ulinzi wa familia yangu!

Dumuni ktk kuomba na kuwaombea wenzenu!

Hebu chukua nafasi hii sasa kuwaombea watoto wote nchini ambao muda huu wamebaki wao na wasaidizi wetu na pia kuwaombea hao wasaidizi!

Mungu akubariki
 
Back
Top Bottom