Hauna Rafiki?, Kuna Marafiki wa Kukodisha Siku Hizi

Dr. Chapa Kiuno

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
443
18




Thursday, September 24, 2009 5:36 AM
Kama siku utaamua kutembelea Japan na hauna rafiki yoyote unayemjua nchini humo usitie shaka hata kidogo kwani kuna makampuni mengi yanayotoa marafiki feki wa kukodisha ambao unaweza ukatumia nao muda kwenye shughuli zako za kila siku.


Kutokana na maisha ya kazi za Japan yanayowafanya watu wengi wawe wapweke, makampuni yanayotoa marafiki wa kukodisha nchini humo yameongezeka kwa kasi sana siku za karibuni.

Kama unahitaji watu watakaojifanya kuwa marafiki zako wa karibu sana wakati unapopiga misele kwenye mitaa ya Japan basi usitie shaka kwani kuna makampuni mengi yapo yanatoa huduma ya kukodisha marafiki feki.

Makampuni hayo yanatoa watu watakaojifanya marafiki au hata ndugu wa karibu kwenye misiba na hata sherehe za harusi.

Ukitaka hata mtu wa kujifanya mume wako au mke wako usiwe na hofu kwani kampuni za marafiki feki zitakutatulia tatizo hilo.

Kampuni ya kwanza ya marafiki feki ilianzishwa nchini humo miaka tisa iliyopita lakini hivi sasa kuna kampuni kubwa zaidi ya 10.

Mojawapo ya kampuni hizo inayoitwa Hagemashi Tai ikiwa na maana ya "Nataka kukufurahisha" huwatoza wateja wake sawa na Tsh. laki mbili kwa rafiki mmoja feki wa kupiga naye misele.

Kama unahitaji rafiki feki wa kujifanya rafiki wa karibu na kutoa hotuba ya kukusifia kwenye harusi yako basi kuna malipo ya ziada ambayo hutolewa.

Mfumo wa maisha ya kisasa ndio unaosemekana kuchangia watu wengi kuwa wapweke na kuwa na marafiki wachache sana wanaowazunguka hivyo kuhitaji marafiki zaidi feki wa kupiga nao stori au kuwa karibu nao wakati wa sherehe au kwenye misiba.

Hiroshi Mizutani, mmiliki wa kampuni ya marafiki feki ya Office Agents yenye wafanyakazi 1,000 alisema kwamba marafiki feki anaowakodisha kwa watu huwa wanavaa nadhifu na huonyesha furaha wakati wote kama vile watu wenye kazi bora duniani.

Iwapo marafiki feki watahitajika kusimamia harusi basi hujifunza historia ya wanandoa mapema kabla ya kuhudhuria harusi.

Wasanii wengi wa maigizo wamekuwa wakilichangamkia dili hilo la marafiki feki na makampuni mengi bado yanahitaji wasanii zaidi watakaoigiza kama marafiki feki katika maisha ya kweli ya kila siku.
</SPAN>

 
huku bongo kuna kikundi cha kukodi kulia harusini,kuwaachanisha wapenzi na mkodombwe
 
Yaambie hayo makampuni yaje yawekeze Tanzania manake hawa marafiki wa hiari ni majanga bora wa kukodi hata akikugeuka utajua ni sawa tu
 
Hapana siyo hao banna walioko kweny Kampun naenda nachukua halaf na signe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom