Hatuwezi kupata rais kama JK

Mods com' on!!!!!!!!! Hii ni haki kweli? Bora FaizaFoxy afunguliwe ila huyu asulubiwe..... Pls Mods!!!!!!!

Hapana huyu mimi nilisema ndiye Faiza Foxy chunguzeni majibu yake. Faiza Foxy mara nyingi majibu yake huwa ni short kama huyu yaani anajionesha
 
mtazamo wangu bora apewe miaka kumi kuongoza nchi tutapata maisha bora kila mtanzania

jane_000, nionavyo mimi umechanganya mambo mawili
1. Miaka 10 ya kuongoza tayari anayo hiyo nafasi na alikwisha kupata kiapo cha mwisho kumalizia hiyo miaka
2. Maisha bora kwa kila mtz - hili kasema hata mzee Nyerere, Mwinyi na Mkapa hawakulifikia walimaliza changamoto zilikuwepo ambazo awamu zilizofuata zilianzia kufanya kazi . Hivyo basi awamu hii nayo haiwezi kumaliza yote imefanyia hayo yaliyowezekana mfano. Kutoa msamaha kwa wale walioweza kurejesha fedha za EPA n.k.
 
Jane bana..............watu wameshadiscuss eti upigwe ban lakini wapi............mwana unatisha

Akili za kitoto kweli kweli, unajibandika ID kumi na kujipongeza. Leo ni tarehe 16 Feb 2012 ndio siku ya kuzaliwa kwako hapa JF. haya ya Jane kuombewa ban umeyajuaje?
 
poo1.jpg
 
Akili za kitoto kweli kweli, unajibandika ID kumi na kujipongeza. Leo ni tarehe 16 Feb 2012 ndio siku ya kuzaliwa kwako hapa JF. haya ya Jane kuombewa ban umeyajuaje?

Wewe nawe bumpkin kweli watu tangu 2006 wanaingia kamaguests angalia kwenye utambulisho wa wageni wapya nimejitambulishaje wewe. Kwa taarifa yako wasomaji wengi wa Jf ni guests ukilinganisha na wanachama. Wewe uliyejiunga tarehe 5 January mwaka huu ndo unaona unajua saana. Lione kwanza. tehetehetehetehetehetehetehetehetehetehete
 
JK Asaidia Vijana









Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika hatua mbalimbali za kusaidia kufyatua matofali ya kisasa kwenye kambi ya mafunzo ya ujasiriamali na ujenzi kwa vijana 380 toka wilaya zote za Mkoa wa Pwani za Kibaha mjini Kibaha vijijini, Mafia, Kisarawe, Mkuranga na Rufiji.


Kambi hiyo ya mwezi mmoja iliyo katika kijiji cha Msoga, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, ni moja kati ya kambi kadhaa zinazoandaliwa mkoani humo, ambapo ikimalizika hii ya ujenzi mnamo february 29, itafuatia ya upandaji miti na mazingira itakayokuwa katika Chuo cha Elimu Kibaha. Baada ya Hapo itafuatiwa kambi ya ukulima wa mazao ya mbogamboga wilayani Rufiji.


Rais Kikwete ameusifu mkoa wa Pwani kwa kubuni kambi hizo na kutaka mikoa mingine iige mfano huo ili kuwapa vijana ujuzi wa kuweza kujiajiri wenyewe.


Ameahidi kuendelea kusaidi vikundi vya vijana vya aina hiyo ambavyo amevitaja kama hazina nzuri ya maendeleo na utatuzi wa vitendo wa tatizo la ajira.


Rais Kikwete ametoa mashine za kufyatulia matofali ya kisasa 76 ambapo kila moja kati ya vikundi 38 vilivyopo vitapewa mashine mbili mpya na waliyofanyia kazi wataondoka nayo na kuwa ya tatu. Pia Amewapa vijana hao mifuko 3800 ya saruji (kila kundi mifuko 100), viatu vigumu (gum boots) pamoja na mananasi toka shambani kwake.

Usanii mtupu!!!!
 
Back
Top Bottom