Hatutarudi nyuma – Sheikh Farid

Mie kwa kuongezea ujumbe kwa Mohamed Aboud, hivi wewe wa wapi? inabidi tujiulize - mapinduzi ya mwaka 1964 wewe ulikuwa wapi? inaonesha ulikuwa hujaja zanzibar (unguja na pemba) kweli enhe?
 
Mimi naona swali la muhimu moja tuu. Hawa mashehe wanapata wapi nguvu? Who is behind them
 
Hatutaki Muungano
Today 14:29

Junior Member
Array
Join Date : 30th May 2012
Posts : 2
Rep Power : 0
Likes Received : 0

Likes Given : 0



Duh! Leo leo!!
 
siyo kutafuta uhuru ila tu baadhi ya wazanzibari wanafanya uvunjivu wa amani jambo ambalo hatari kwa maisha ya wapenda amani:lock1:

Amani haitokuwepo kama hujaanza na vita - Hivi kweli kama mwanamke uliye muoa akikwambia kuwa sikutaki tena basi niache, utaendelea kuishi nae - labda kwa wenye vichwa vilivyozidi nyuma - sasa sisi tumesema basi hatutaki tena muungano jamani hebu tuacheni na ki-jinchi chetu, hivi mumeona wapi watu 45Milioni kufanya muungano na watu 800,000 maajabu ya Mussa haya.
 
Hivi jamani muungano unazungumziwa kwenye misikiti? Tuwe watu wakutambua kuwa unapoanzisha cheche ya moto anaglia usiwe wa kwanza kuungua.Kama Zanzibar siwaichukue?Inatusaidia nini Wadanganyika?Siyo tu waongee kuvunja muungano na hao WaZanzibar walioko Huku Danganyika waanze kuondoka si basi kila mtu abaki na chake?Tumewachoka bwana anzeni tu!

Hata mimi kinachonshangaza na kunipa hofu ni upinzani huu kuanzia msikitini, kuna ajenda gani nyuma ya pazia?
 
Hii move ni nzuri lakini kwanini wanafanyia 'msikitini'??

Hivi makanisa yakichomwa kwa mazingira haya nani alaumiwe kama si wao??

Kwa nini wasifanyie suala hili nje ya ulingo wa 'dini'??

BTW, Hongereni wakuu tuko pamoja hadi 'kieleweke' huko Zenj!!
 
Is this Sheikh still at large?

Baada ya kuona hiyo picha, nimeingiwa na wazo kwamba initiators wa hii kitu kumbe ni masalia ya ile familia ya Al Mazrui, hebu rudini kwenu huko ghuba ya Uajemi msituletee fujo hapa....
 
Hivi huyo Farid na Mwenzake asili yao wapi? au kukulia Zanzibar na Passport ya Oman umenakuwa Mzanzibar automatically? je walisha ukana uraia wao asilia walipofikisha miaka 18?
Maana naona kama wapo kama al Qatada
 
eti nchi yetu..nchi gani ina mikoa miwili tu...fanyeni kazi wazenji nyie acheni kutafuta umaarufu usiokua na mbele wala nyuma

Hata Kama ina kajimkoa kimoja ndo ya kwao ndugu yangu...


Sent from my iPad using Tapatalk HD
 
Ovyo kabisa huyo Sheikh, sina hakika kama yuko na akili timamu! Basi aende msituni kama kika Joseph Koni. Maana njia stahili ya kupata suluhu ya chochote ni kukaa mezani unless kama unataka kumwaga damu.
 
Posted on May 30, 2012 by zanzibaryetu
Kiongozi wa Maimamu Zanzibar, Farid Hadi Ahmed akiongea na waumini katika msikiti wa Mbuyuni Zanzibar jana baada ya sala ya alaasiri

JUMUIYA ya Mihadhara ya kiislamu (Uamsho) imetoa msimamo mkali shidi ya Serikali ikisema kuwa haitarudi nyuma katika kudai uhuru wa Zanzibar.

Wakizungumza katika msikiti wa Mbuyuni uliopo eneo la Darajani mjini Zanzibar, viongozi wa Uamsho wamewataka Wazanzibari kutolegezamsimamo wao hata kama jeshi la polisi limezingira mji wao.

"Umoja wetu ndiyo utakaotukombolea nchi yetu, msikubali kuyumbishwa na kitu chochoe ili kulegeza msimamo wetu. Jambo moja tu, ni mpaka kieleweke.

Bila hivyo hakuna jeshi, hakuna polisi atakaye tuyumbisha" alisema Sheikh Mussa Juma wa msikiti huo na kuitikiwa na wafuasi waliokuwa wamefurika katika msikiti huo "ndiyooooo!"

Wafuasi hao walikuwa wameshikilia karatasi zilizoandikwa "hatuutaki muungano, tunaitaka Zanzibar yetu".

Naye Sheikh Mussa Juma aliyekuwa amekamatwa na jeshi la polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana aliwapongeza wanachi waliotokana kuandaana akisema kuwa hawatarudi nyuma, Tunawashukuru Wazanzibari kwa sababu mmeonyeshwa kutotaka kutawaliwa" alisema na kuwauliza wafuasi hao "mko tayari" nao wakijibu "Tuko tayariii"

Naye Sheikh Farid Hadi Ahmed alisema kuwa kundi hilo linafuata taratibu hivyo halipaswi kulaumiwa kwa kufanya vurugu. Aliwataka pia Wazanzibari kutogawanyika kwa vyama vya siasa,"Muone katika silaha kubwa wanayotumia maadui ni kutugawa kivyama na kikabila au kirangu, inasikitisha sana."

Huku akinukuu Katiba ya Zanzibar ibara ya 23 Farid alisema kuwa kila Mzanzibari anapaswa kuhifadhi mamlaka na uhuru ya Zanzibar.

Aliwahamasisha wafuasi hao kuonyesha mabango waliyokuwa wameshikilia na kumtaka mkuu wa jeshi la polisi kutambua hitaji kubwa la Wazanzibari.

"Hebu mwonyesheni IGP mlichonacho….. mnautaka muungano hamuutaki? (wote wakajibu) "hatuutaki!).

Huku akitoa mifano, Farid aliendelea kusema kuwa kilichopo ni wimbi la Wazanzibari kudai nchi yao.

Alisema kuwa kama vile maji ambayo yakizibwa katika njia yake husambaa mitaani, hivyo ndivyo Wazanzibari wanavyosambaa mitaani kudai nchi yao.

Alitetea kitendo cha jumuiyta hiyo kuandamana akisema kuwa si kosa kisheria kutembea barabara.

"Kwani mtu akitembea kwenye nchi yake anatembea kwa kibali? Sisi tumeamua kutembea… waliokuja na wake zao wametemebea na Mwenyezi Mungu kajalia tumetembea kwa furaha yote. Mbona timu zinafanya mazoezi, zinachukua vibali, watu wanakwenda hitimani wanapewa vibali?" alihoji.

Faridi alitangaza siku ya Mei 26 kuwa ni ya maandamano kwa Wazanzibari na kuwataka wanajeshi wa Kizanzibari kujiandaa kuwaunga mkono katika maandamano hayo.

Huku akikwepa lawama kwa kundi hilo kwamba limekuwa likichoma na kuharibu makanisa, Sheikh Farid aliwalaani watu wanaounganisha kundi hilo na tuhuma hizo, "Tunamwambia IGP kamishina hana uwezo hana uwezo. Wanajeshi tunao…. Vikosi vina watu 8000 waambie wajindae wasibebe silaha ni ndugu zetu… waje wakae barabarani wala sisi hatuhitaji ulinzi" alisema na kuongeza,

"Lakini tuna wasi wasi na hawa wanaolipua makanisa na sisi tunawalaani vibaya, hawa tunaamini ndiyo wale wale waliokuwa wakisimama na kutukana matusi, tena wana visu, wana nondo, wana pesa Mheshimiwa IGP waambie wakupe rekodi."alisema Farid.

Licha ya Waziri katika Ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais Mohammed Aboud kukemea mihadhara hiyo, jeshi la polisi halikuthubutu kuingilia mkutano huo.

Magari yaliyosheheni askari polisi yalionekana yakipita mbali na eneo hilo bila kuwabughudhi.

Hapa inahitajika busara kubwa sana ama sivyo Nchimbi & Co watakuja kuadhirika

maandamano na mikutano imepigwa marufuku lakini watu wanakutana kama kawaida bila kuogopa

hii Arab Spring imewapa sana watu moyo
 
Hata mimi kinachonshangaza na kunipa hofu ni upinzani huu kuanzia msikitini, kuna ajenda gani nyuma ya pazia?

Ndugu yangu usiwe na hofu juu ya hili, sisi Wazanzibari tuna-experience ambayo nyie wenzetu wa bongo hamna, Tukipitia chama wasema hawa wanataka kutugawa na kumwambia tendwa wafute na watatusimamisha mara moja. Ila kwenye msikiti nani ataufunga - hayupo na kama wanataka wajaribu tu, wameona Trailer ile 26th na 27th. Sasa sisi hatuna ugomvi na wakristo wala wabara waliopo hapa unguja na pemba - ikiwa hawatoingilia wala kujifanya wao wako kimbelembele kitawakuta kilichompata firauni. Maana saivi hatutanii kwa hili - hadi nchi ipatikane.
 
Jibu muhimu ni moja tuu, Wazanzibari ndio walio nyuma yao na ndio wanaowapa nguvu hizo, Zanzibaris are behind them and fully committed

Zanzibar inamilikiwa na msikiti gani? Hizi pesa za Alshabab na Boko haram zitawamaliza! By the way ninyi ni wepesi sana kwetu!
 
Ovyo kabisa huyo Sheikh, sina hakika kama yuko na akili timamu! Basi aende msituni kama kika Joseph Koni. Maana njia stahili ya kupata suluhu ya chochote ni kukaa mezani unless kama unataka kumwaga damu.

Hivi wewe umeambiwa na nani kama unaakili wewe mwenyewe, kwasababu ukionacho kwenye sura ya mwenzako ndio ulichonacho wewe. Suluhu ya kwenye meza ni kwa wenye akili wanaoambiwa wakajiambia na kusikia - wewe unaambiwa hatutaki muungano unang'ang'ana musijadili muungano ila katiba tu, ebo! hivi hizo ndio unaona wewe ni akili - hebu muulize tena aliyekuambia kuwa unazo kweli. Lakini sishangai akili haikai miguuni ni ajabu hii........?!!!
 
wazanzibar km sheria ya katiba hairuhusu kujadili muungano msitumie dini nawashauri anzisheni kampeni ya nyumba kwa nyumba kwa lengo la kuiweka kando ccm 2015,unganeni bila kujali itikadi ,wakiona hivyo wenyewe watalegeza masharti na muungano utajadiliwa vinginevyo ccm wataendelea kuwakandamiza kama ambavyo wamepeendekeza wao badala ya wananchi kwamba wanataka mfumo uliopo uendelee.
 
Back
Top Bottom