Hatupaswi kuipongeza Serikali kwa lolote; Bali kuikosoa pale inapokosea!.

Deus F Mallya

JF-Expert Member
Jul 28, 2011
705
440
Mara kadhaa nimesikia Rais,PM,Mawaziri,na Watendaji wa idara za serikali wakisema "Serikali ipongezwe kwa Juhudi zake za kufanya kitu fulani".

Pia nimekuwa nikisikia baadhi ya Wabunge wakisema "Naipongeza/Tunaipongeza serikali kwa kufanya kitu fulani". Binafasi hapa naingiwa na ukakasi nafsini mwangu, kama tunapaswa kuishukuru Serikali pale inapokusanya kodi kutoka kwetu na kutekeleza miradi flani.

Pia izingatiwe kuwa kodi hiyo hiyo ndiyo wanayolipana posho,mishahara na kuweka mafuta kwenye magari yao ya kifahari.

Ninadhani Serikali inapaswa kuwashukuru wananchi kwa kuendelea kununua bidhaa mbali mbali hata pale kodi inapoongezwa kwa lazima.

Nifungueni hapa.
 
Hapo umenena Mkuu.
Pia hatupaswi kuiomba Serikali. Tunapaswa kuiagiza serikali.
Nadhani wengi huwa wanakosea kwa kudhani kuwa Serikali ni li mungu falini likubwa linalofanya vitu kama msaada kwa wananchi.
 
mi naamini mwanadam yeyote anapaswa kupongezwa pale anapopatia na kukosolewa anapokosea.
Hiyo ndio fair play. Mbunge akipatia apongezwe, waziri akipatia apongezwe, mwalim/daktari akipatia apongezwe nk.
Vivyo hivyo na wanapo kosea.
Huo ndo ubinadamu.
 
mi naamini mwanadam yeyote anapaswa kupongezwa pale anapopatia na kukosolewa anapokosea.
Hiyo ndio fair play. Mbunge akipatia apongezwe, waziri akipatia apongezwe, mwalim/daktari akipatia apongezwe nk.
Vivyo hivyo na wanapo kosea.
Huo ndo ubinadamu.

Mtu mmoja mmoja sawa, je serikali kwa ujumla wake ni sawa kupongezwa?
 
Back
Top Bottom