Hatulali chumba kimoja!!

Ni miezi sita sasa huyu mpenzi wangu tangu aanze hii tabia ya ajabu, kama yuko chumbani nikitaka kulala anahamia chumba kingine, nikimfata huko anakwenda kulala sebuleni, sina raha, sina wa kuongea nae,mpaka nimvizie kalala fofofo ndio nijisogeze nilale pembeni yake na akishtuka tu anahama kwingine,nikumuuuliza sababu zinakuwa nyingi lakini hazina msingi, kama mnavyojua raha ya kulala sharti usikie mapigo ya moyo ya mpenzi wako. Wana JF nawaombeni mnipe ushauri wa kina nini cha kufanya ili niondokane na hili balaa?

Acha hizo mjomba, huyo demu hakutaki. Anza wewe kumreject, akija ulipo wewe ndo unaondoka. Ukimwendekeza sana utakuja lia, oh!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom