Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Hatujachagua meya Arusha - CHADEMA
na Halfani Lihundi, Arusha
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha kimekanusha kufanya mkutano wa kuchagua meya na kwamba hivi sasa halmashauri inatawaliwa na mameya wawili kutoka CHADEMA na CCM.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Diwani wa Kata ya Kimandolu, Estomil Malla, ambaye ndiye aliyetajwa kuwa ndiye aliyechaguliwa kuwa meya kwa upande wa CHADEMA alisema taarifa hizo si za kweli na kwamba CHADEMA haijawahi kufanya uchaguzi kama huo.
Malla alisema aliyetoa taarifa hizo ana lengo la kuipotosha jamii japo kuwa CHADEMA haimtambui meya aliyechaguliwa na CCM, lakini hawajafanya uchaguzi na hawatarajii kufanya, kwa kuwa wanajua kuwa uchaguzi wa kumchagua meya bado haujafanyika Arusha.
Alisisitiza kuwa meya aliyechaguliwa na CCM si halali, kwani katika uchaguzi huo kuna kanuni za baraza la madiwani ambazo zimevunjwa na kubainisha kuwa CHADEMA inafuatilia suala hilo kisheria.
Wakati sisi tunafuatilia suala hili kisheria, hatuwezi kuvunja sheria, kwani kufanya hivyo ingekuwa kinyume cha taratibu, mimi sijui jambo hilo limetokea wapi, maana kila nikipita naona watu wanaiita meya huku wengine wakinishangilia, napenda kuwaambia wananchi wajue kuwa mimi si meya, alisema Malla.
Mbali na hayo, Malla alifafanua kuwa taratibu za kisheria wanazozifuata CHADEMA ni tofauti na mahakama, kwani njia za kisheria zipo nyingi si mahakama pekee.