Hatuhitaji Tume ya Katiba ya JK.....Katiba ya Zamani Tunaijua

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Tunaijua ndiyo. Hatuitaji Kamati wala Tume:


  1. Katiba ya sasa inaruhusu polisi kufyatulia risasi za moto na kuuwa raia na "upelelezi unaendelea"
  2. Katiba ya sasa inaruhusu ufisadi kama huu wa Richmonduli, Dowans, Epa nakazalika
  3. Katiba ya sasa inaruhusu mtu mmoja (jina ninalo) kuteua Rais wa nchi
  4. Katiba ya sasa inaruhusu masikini waendelee kuwa masikini na matajiri (tena wengi wao siyo Watanzania) kuendelea kuwa matajiri.
  5. Katiba ya sasa inaruhusu rasilimali zetu kuvunwa kiholela kwa makubaliano kati ya waziri mwenye dhamana na wawekezaji/wakoloni
Kwa dhambi na dhuluma hizi, wala sihitaji tume wala kamati kuja kunieleza lolote mimi mwananchi. Na wala sihitaji kuwa na hicho kitabu cha katiba kwani yaliyomo ndo hayo hapo juu.

Tunataka katiba mpya!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom