Hatuhitaji katiba mpya ya CCM!

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
497
236
Tanzania ya leo inahitaji katiba ya nchi iliyotokana na mapendekezo ya wananchi ili ipate uhalali (Legitimacy) ya kuheshimiwa. Mjadala wa muswada wa katiba unaoendelea sasa umekuwa ukipingwa na baadhi ya wanasiasa, Wanaharakati, Mabaraza ya katiba, Majaji na wananchi kwa ujumla. Kwa hali hii tayari katiba inayotarajiwa itakosa uhalali kutoka kwa wananchi kwani watu wanaoendelea kuujadili na wanaotarajiwa kuupitisha mswada huo ni walewale walioandika katiba zenye viraka zinazotuburuza mpaka leo yaani "watu wale wale mawazo yaleyale katika suti mpya"

Kimsingi hatutaki mabadiliko ya rangi au kurasa za katiba tunahitaji mabadiliko chanya ya Content ya katiba.
 
Back
Top Bottom