Elections 2010 HATUDANGANYIKI kuwa kauli mbiu ya Waislamu kuelekea Uchaguzi Mkuu

Huduma

Member
Jan 26, 2008
68
1

  • Kususia FUTARI za kisiasa na za Wamarekani.

VIONGOZI wa dini ya Kiislamu wamejifungia katika Msikiti wa Mtambani wakiandaa tamko muhimu katika historia ya Uislamu nchini.

Shur aya Maimamu imekuwa ikipitia kwa makini kila sentensi na aya zinazokusudia kuwaunganisha Waislamu dhidi ya wale wanaotia vikwazo kwa maendeleo ya dini hiyo na Waisalmu nchini.

Habari toka ndani ya Shura hiyo zinaeleza kwamba maimamu wamevutiwa sana na yule msichana ambaye watu wa umri wa babu zake, baba zake, kaka zake na vijana wenzake wote wanamtongoza kwa siri au bayana lakini yeye kang'gang'ana na silaha moja tu: 'SIDANGANYIKI!' Kwa kuwa Waislamu nchini wamekuwa wakihadaiwa na kila kiongozi anayeingia madarakani masheikh wanataka kuhamasisha Waislamu nchi nzima kukataa katakata tabia ya kudanganywa kama watoto.

Wanadai yapo madai yao na ahadi zilizotolewa na msururu wa viongozi kwamba hiki au kile kitafanywa lakini hakuna kilichofanywa. Kwa sababu hii watawataka Waislamu kutokuwakubali wale ambao kwa namna moja au nyingine wamechangia Waislamu kudanganywa na kuendelea kuchukuliwa kama raia wa daraja la pili katika nchi ambayo babu na nyanya zao ndio waliojitolea kuwa mstari wa mbele kudai uhuru wake.

Haikufahamika kama maimamu hao wakialikwa safari hii na wakubwa wa serikali KULA FUTARI pale IKULU kama watakubali au la. Kwa mujibu wa redio mbao maimamu hao wanadhamira ya kuwatolea nje wale wote watakaojaribu kuwaalika kufuturu ili kujiongezea pointi za kisiasa huku wakiwanyang'anya Waislamu hata kile kidogo walichonacho.
 
Mods Unganishi hii mada na thread husika then FUNGIA huyu Member
 
kama raia wa daraja la pili katika nchi

Kama kuna kitu wamekipatia basi ni hiki! Ushahidi ni karipio la Marmo!
 
Huyu ndenge wa uchumi ni mpuuzi tuu maana anataka kusupress opinion ambazo haziendani na mawazo yake. I dare say it because its a fact, ni mpuuzi tuu..
 
Mods Unganishi hii mada na thread husika then FUNGIA huyu Member

Afungiwe kwa kipi na wapi hii thread inapohusika zaidsi ya hapa? Hizi si ndio siasa zetu siku hizi? Hili ni zao la waraka wa Kanisa na hadi leo thread inaendelea . Kwani Kingunge aliposema si mlimbeza? Wacha tuvune tulichopanda.
 
haya ni maandishi tu haina haja ya kuwa mwoga Ndege Ya Uchumi, sasa ungekuwa mjadala wa ana kwa ana ungekimbia? changia kama huwezi endelea kusoma tu.
 
Huyu ndenge wa uchumi ni mpuuzi tuu maana anataka kusupress opinion ambazo haziendani na mawazo yake. I dare say it because its a fact, ni mpuuzi tuu..

Mod tunakosa Mtiririko Mzuri, Unganisha hii thread zimekuwa Nyingi, kuna kama thread tatu za waraka wa Waislam.

Halafu Kinyambisi Naomba Ufiche Upuuzi wako na Uonyeshe Hekima zako
 
kujiongezea pointi za kisiasa huku wakiwanyang'anya Waislamu hata kile kidogo walichonacho.

hebu tuweke wazi na hicho kidogo ni kitu gani hicho?
 
Afungiwe kwa kipi na wapi hii thread inapohusika zaidsi ya hapa? Hizi si ndio siasa zetu siku hizi? Hili ni zao la waraka wa Kanisa na hadi leo thread inaendelea . Kwani Kingunge aliposema si mlimbeza? Wacha tuvune tulichopanda.

Sasa ndugu yangu, naona wewe uko hapa kupiga soga tu, hapa kuna Threads zaidi ya Mbili zinazohusu hii habari, wewe kwa u Great Thinker wako huoni kama kuna umuhimu wa Kuziunganisha ili zilete Mantiki.

Come On Ngekewa
 
Mods Unganishi hii mada na thread husika then FUNGIA huyu Member

NyU, that is not so kind of you

... you didnt even give a chance for anyone to digest and learn from a thread [and probably aliyeleta mada angeweza sema kitu badae], please let us learn.

Msimamo wa HATUDANGANYIKI ni mzuri na labda hata viongozi wa kikiristu wangefanya hivyo si ajabu hata wale matajiri wabaya wasingeweza kurubuni makanisa na kuzikwa kifalme wakati hawasali na mali zao ni dhalimu

The spirit ya Hatudanganyiki ni nzuri sana kama inachukuliwa bila uadui wa kidini na kijamii
 
Last edited:
Mimi nausuburi kwa Hamu sana Waraka Huo maana sio Fair kuanza kuchangia kitu ambacho bado hakijatoka offically, I welcome it as far inatoa Fursa kwa Watanzania wengi zaidi kuelewa haki zao za Kimsingi na za Kikatiba .

Angalizo: I think they are doing this a it is their constitutional right and not because RC wamefanya hivyo:
 
Mi ni mkristo kamili kabisa.......ila hii kauli mbiu yao sioni kama ina ubaya kama ikichukuliwa ya kitaifa kuliko kidini zaidi........lkn kutakuwa tunabomoa kama tutaanza kuseme dini hii ndio ilileta uhuru......hii ndio ilileta hki na kile.
 
Sasa ndugu yangu, naona wewe uko hapa kupiga soga tu, hapa kuna Threads zaidi ya Mbili zinazohusu hii habari, wewe kwa u Great Thinker wako huoni kama kuna umuhimu wa Kuziunganisha ili zilete Mantiki.

Come On Ngekewa

Naona kwa thread hii unaona ziko nyingi. Unajuwa kuwa hivi sasa ishaingia ya Kardinali Pemgo ikizungumzia waraka wa wakatoliki? Ziangalie ziko ngapi? Reaction kama yako ndio sawa na ya serikali yaani tunakuwa double standard. Wacha Threads ziendelee isiyo na faida itakufa natural death.
 
Mi ni mkristo kamili kabisa.......ila hii kauli mbiu yao sioni kama ina ubaya kama ikichukuliwa ya kitaifa kuliko kidini zaidi........lkn kutakuwa tunabomoa kama tutaanza kuseme dini hii ndio ilileta uhuru......hii ndio ilileta hki na kile.

Unajuwa Papo, hili suala la dini ni baya kulitanguliza katika jamii. Usijidanganye kuwa utakaa kimya kwa hili na uje huo waraka na utaona.
 
Naona kwa thread hii unaona ziko nyingi. Unajuwa kuwa hivi sasa ishaingia ya Kardinali Pemgo ikizungumzia waraka wa wakatoliki? Ziangalie ziko ngapi? Reaction kama yako ndio sawa na ya serikali yaani tunakuwa double standard. Wacha Threads ziendelee isiyo na faida itakufa natural death.

Am out coz Simjui hata huyo Pengo
 
Tuko Pamoja Dege la Uchumi, i hope mods wataunganisha hizi threads

Labda cha kuangaliza tu ni kwamba wasije wakakataa hata kukaa na americans au any other person asiye mkristu simply because they are biased... if that happen then watakuwa wameua ile dhana chanya ya "Hatudanganyiki" na kuleta ya "Hatukubali" --- Two different stuffs

Pamoja Mazee
 
For Great Thinkers would have seen this coming....
JF m,embers, quote my word.. '2010 ni Uchaguzi utakao igawa Tanzania kwa visingizio cha Mafisadi..JF imenifundisha mengi sana ambayo sikuyajua..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom