Mkereketwa_Huyu
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 9,217
- 6,349
MziziMkavu, nikishakuwa rais wa Tanzania nitakuchaguwa kuwa waziri wa afya kutokana na michango yako uiletayo humu kwani inawasaidia sana watu nami nikiwa ni mmoja wao. Ulileta mada moja juu ya majini siku za nyuma na nikawapa ile nakala ndugu zangu waliokuwa na hili tatizo kwa muda mrefu. Kwa kweli baada ya kusoma zile habari na kupata uelewa wa uhakika, wakaja pata mganga mzuri tu na sasa binamu yangu ni mzima kwa ajili yako wewe. Bahati mbaya dada zangu wote wameolewa ningekupa mmoja lakini uwaziri utaupata tu bila kujali chama chako (CCM) kwani najuwa utakikana baada ya kupata ulaji, si ndiyo? Basi, subiri 2015.
Last edited by a moderator: