Ndugu zangu wana JF,
Awali ya yote naomba niwapongeze kwa ushindi KIDUCHU mlioupata kule ARUMERU, kiukweli sikupenda CDM iibuke washindi ila nilipenda CCM ishindwe. Ninakiri kuwa kuna tatizo kubwa sana tokea kura za maoni, nguvu ya ushawishi na pesa nyingi zilisababisha SIOI ashinde ilihali kulikuwa na viashiria vya rushwa!
Kuna sababu nyingi zilizopelekea CCM kutoshinda uchaguzi ule ambazo kiukweli zimenikosesha raha na hata kutype kwenye keyboard nashindwa!
1) Lusinde alipunguza idadi ya kura Arumeru kwa kiasi kikubwa, ukitumia lugha mbaya kama zile usitegemee mtu akuchague, inshort ningekuwa na maamuzi katika CCM lusinde ningemnyang'anya kadi ya chama.
2) Waliokuwa ndio wanaongoza kampeni hawakuweza kutoa sababu ni kwa nini muda wote ambao jimbo lilikuwa chini ya CCM na kero mbali mbali hazikushughulikiwa na leo wanaahidi kuzishughulikia, Mfano: Ni ukweli usiopingika mtu kama MKAPA hawezi kuwashawishi wana ARUMERU kuwa atamshauri Kikwete wakati alikuwa Rais na hakuweza kutekeleza matatizo hayo. Mi nafikili ilitakiwa kwa wanaccm kukiri makosa na kuonyesha ni kwa vipi watasahihisha makosa yao, Lakini baada ya kutumia njia hii wakajikuta WANAROPOKWA na kutumia lugah zisizo na staha.
3) Kutumia watu wenye kashfa na wanaoongoza katika makundi katika CCM tena hao hao wanajulikana kuwa hawapo katika kundi moja kama OLE SENDEKA na LOWASA, hii ilidhihirisha Unafiki wa aina yake, Haiingii akilini watu hawa ambao kila kukicha wanaitana mafisadi na kushutumiana mbele ya camera za waandishi leo wanapanda jukwaa moja. Tatizo kubwa ni kuwa wanayoyasema na wanayotatenda ni tofauti tena kwa nyuzi 180[SUP]0[/SUP](Diferent Direction)
4) UVCCM hasa wa arusha nao hawakwepeki katika hili, katika kufikili wanawakomoa wale waliopinga uteuzi wa sioi kwa kuwa unanuka harufu ya rushwa na wengine waliotilia shaka juu ya uteuzi wa sioi wao wakatumia nguvu na wingi wa kura zao kumchagua Sioi lilikuwa kosa la kihistoria.
5) Hakukuwa na kauli ya pamoja katika kampeni za CCM kila aliyepanda jukwaani alisema yake, in short ilikuwa kama watu wamechanganyikiwa.
Conclusion:
Huu ni uthibitisho kuwa LOWASA na kundi lake hawakubaliki katika jamii, na CCM isije kufanya kosa 2015
Hongera CDM ingawa ushindi wenu unatokana na UJINGA na UDHAIFU wa CCM
by cZg wa ETU: nilifikir we hv grown up politically kumbe bado kuna bendera fuata upepo ka weye? Haya funguka kakosea nn? Acha majungu tujenge Tz 'kama shida ni panya rangi ya paka isiwe kikwazo'Wewe ni mnafiki huna lolote, hayo makosa yenu unatwambia sisi ili iweje, nenda kazungumze huo ujinga wenu kwenye vikao vyenu na hili ndilo anguko la CCM. Tayari katika bara la Africa tumeshuhudia vyama kadhaa vikongwe vikianguka na sasa ni zamu yenu buriani CCM.
Unaweza kunifafanulia kwa nini NEC ilizuia matumizi ya fomu iliyokuwa inaruhusu raia asiye na kadi ya kupiga kura lakini yumo katika oradha ya wapigakura wanaotambuliwa na NEC wakati sheria inaruhusu matumizi ya fomu hiyo ?Kweli wewe mpiga kelele! hizo percent umezitoa wapi? wewe ndio NEC? Nina wasiwasi furaha inakupelekea kufikilia hata yasiokuwepo!