Hatua za haraka zinahitajika, Wafuatao wameihujumu CCM

Uchambuzi wako una mapungufu na hizo ni hisia zako tu. Ukweli ni kuwa CCM hainaminiki tena mbEle na ndani ya mioyo ya Watanzania ambao mulikukwa munawafanya Wadanganyika kwa vipesa vyenu vya wizi. Huko Mwanza na Rungwe nako alikuweko huyo Lusinde, Mkapa na wengineo uliowataja? Kauli mbiu ya Mwanza - Kirumba ni ilikuwa Vijana wote vaaeni nguo za CCM na hakikisha mnakula Kwelikweli vipesa vyao na siku ya siku lala kwa CDM. Nyimbo za Jana Mwanza Viwanja vya Furahisha katika kumtangaza mshindi ilikuwa ".... tumekula pesa zenu na kura tumewanyima.... na bado Kikwete" Wakojacko
 
Low hasa anakubalika kusimama kwake jukwaani kumeongeza kura nyingi sana vinginevyo hali ingekuwa ngumu zaidi. Kuumwa kwake kumeathiri sana, angeshiriki toka mwanzo nadhani tungesema mengine. Anafaa huyu jamaa apewe nafasi kupeperusha bendera 2015. Kilicho mcost Sioi ni ile tu baba yake kuwa ndo anamrithi na ubunge, kwa mazingira ya sasa watu wengi wasingekubali kwenye jimbo lolote pia suala la utata wa uraia nalo lilicount
zingatia anacho sema mtu si ya kwako yeye alisema haumi alikuwa Ujerumani kucheki hali ya macho na akademostrate alivyo mzima sasa kuumwa kulikuaje

kuhudhulia kampeni kulitegemea sana na ratiba na mipango ya kikosi dhaifu cha kampeni kilicho undwa kimsingi jamaa (mtoa mada) amejitahidi kueleza ukweli ila sema amesahau kuwa hali sasa si ile ya 1995

 
Ndugu zangu wana JF,
Awali ya yote naomba niwapongeze kwa ushindi KIDUCHU mlioupata kule ARUMERU, .............UDHAIFU wa CCM


Ushindi kiduchu ??????!

Waliojiandikisha kupiga kura ~120,000 waliopiga kura ~60,000. Ambao walizuiwa kupiga kura na Tume ya uchaguzi kwa kuwa nyima form no.17 ni ~60,000, hawa walinyimwa makusudi nafasi ya kupiga kwa sabubu wengi walikuwa vijana ambao wangepigia CDM-Nassari kura. Tufikiria asilimia 10 %ya kura za wale walionyimwa fursa kupiga kura zingeharibika, basi kura ~50,000 zingeenda kwa CDM-Nassari.

Kwa maneno mengine:

CDM-Nassari wangepata kura 50,000 +32,000 = 82,000 (75.9~76%)

CCM-Siyoi wangepata kura 26,000 (~24%)

Kwa mnyumbilisho huu wa takwimu bado unaamini ushindi wa CDM ni kuduchu ?
 
Kidogoo kidogo baadhi ya wanacdm humu ndani muanze kufanana na ushindi wa kisayansi wa Arumeru na kuachana na tabia za matusi na midomo .........................

Hakuna sababu ya kubembeleza wanafiki. Apeleke unafiki wake huko huko. Huu utafiti wa kisayansi kwanini aje nao sasa, tangu mwanzo alikuwa wapi? Ulikuwa unafuatilia alichokuwa anaposti wakati wa kampeni? Ina maana utafiti wa kisayansi unakuja baada ya kushindwa? DSN, fuatilia alichokuwa anabandika wakati wa kampeni ndiyo uje kumtetea hapa, usiishie kuwa "fair" kwa kutetea mizoga. Huyu jamaa akafie mbali, No Retreat No Surrender.

Ushindi wa CDM hautokani na udhaifu wa CCM bali uimara wa Watanzania.
 
CCM inastahili kuvuna ilichopanda. Kwa mwenendo mzima kuanzia wapi walime na mbegu gani wapande. Walipanda mahindi wakatarajia kuvuna kahawa! Wapi!
 
Ndugu zangu wana JF,
Awali ya yote naomba niwapongeze kwa ushindi KIDUCHU mlioupata kule ARUMERU, kiukweli sikupenda CDM iibuke washindi ila nilipenda CCM ishindwe. Ninakiri kuwa kuna tatizo kubwa sana tokea kura za maoni, nguvu ya ushawishi na pesa nyingi zilisababisha SIOI ashinde ilihali kulikuwa na viashiria vya rushwa!

Kuna sababu nyingi zilizopelekea CCM kutoshinda uchaguzi ule ambazo kiukweli zimenikosesha raha na hata kutype kwenye keyboard nashindwa!

1) Lusinde alipunguza idadi ya kura Arumeru kwa kiasi kikubwa, ukitumia lugha mbaya kama zile usitegemee mtu akuchague, inshort ningekuwa na maamuzi katika CCM lusinde ningemnyang'anya kadi ya chama.

2) Waliokuwa ndio wanaongoza kampeni hawakuweza kutoa sababu ni kwa nini muda wote ambao jimbo lilikuwa chini ya CCM na kero mbali mbali hazikushughulikiwa na leo wanaahidi kuzishughulikia, Mfano: Ni ukweli usiopingika mtu kama MKAPA hawezi kuwashawishi wana ARUMERU kuwa atamshauri Kikwete wakati alikuwa Rais na hakuweza kutekeleza matatizo hayo. Mi nafikili ilitakiwa kwa wanaccm kukiri makosa na kuonyesha ni kwa vipi watasahihisha makosa yao, Lakini baada ya kutumia njia hii wakajikuta WANAROPOKWA na kutumia lugah zisizo na staha.

3) Kutumia watu wenye kashfa na wanaoongoza katika makundi katika CCM tena hao hao wanajulikana kuwa hawapo katika kundi moja kama OLE SENDEKA na LOWASA, hii ilidhihirisha Unafiki wa aina yake, Haiingii akilini watu hawa ambao kila kukicha wanaitana mafisadi na kushutumiana mbele ya camera za waandishi leo wanapanda jukwaa moja. Tatizo kubwa ni kuwa wanayoyasema na wanayotatenda ni tofauti tena kwa nyuzi 180[SUP]0[/SUP](Diferent Direction)

4) UVCCM hasa wa arusha nao hawakwepeki katika hili, katika kufikili wanawakomoa wale waliopinga uteuzi wa sioi kwa kuwa unanuka harufu ya rushwa na wengine waliotilia shaka juu ya uteuzi wa sioi wao wakatumia nguvu na wingi wa kura zao kumchagua Sioi lilikuwa kosa la kihistoria.

5) Hakukuwa na kauli ya pamoja katika kampeni za CCM kila aliyepanda jukwaani alisema yake, in short ilikuwa kama watu wamechanganyikiwa.

Conclusion:
Huu ni uthibitisho kuwa LOWASA na kundi lake hawakubaliki katika jamii, na CCM isije kufanya kosa 2015

Hongera CDM ingawa ushindi wenu unatokana na UJINGA na UDHAIFU wa CCM

kumkashifu vincent 'Nyerere' wamejipalia makaa.
 
unahitaji elimu ya uraia, tafadhali wana Jf mavuno hayo. Mfundisheni na ikiwezekana avue gamba.
 
wewe ni mnafiki huna lolote, hayo makosa yenu unatwambia sisi ili iweje, nenda kazungumze huo ujinga wenu kwenye vikao vyenu na hili ndilo anguko la ccm. Tayari katika bara la africa tumeshuhudia vyama kadhaa vikongwe vikianguka na sasa ni zamu yenu buriani ccm.
kwanini usimuulize na zile kata tulizowadunda sababu ni zipi???all in all ccm imechokwa
 
Hongera CDM ingawa ushindi wenu unatokana na UJINGA na UDHAIFU wa CCM
Mkuu, kusema kuwa CDM wameshinda kwa ujinga na udhaifu wa CCM inaweza kuwa sahihi; tatito ni pale statement hiyo inapoonekana kuconclude kuwa Ushindi wa CDM haukutokana na juhudi zake katika kunadi sera zake. Hukuwa na haja ya kusema "ingawa". CDM wameshinga kwa sababu ya umakini na umahiri wao katika kuwashawishi wapiga kura, period.
 
Kweli wewe mpiga kelele! hizo percent umezitoa wapi? wewe ndio NEC? Nina wasiwasi furaha inakupelekea kufikilia hata yasiokuwepo!
Jana wewe ulikuwa na nyodo sana usimsingizie Lusinde kumbe hata wewe unamatusi ya reja reja. Ule wimbo wa kura za vijijini umeishia wapi, hii ni karne mpya.
 
Hakuna hujuma wala mtoto wa hujuma, CCM ilishapoteza dira toka siku nyingi tu, hicho tulichokiona Arumeru ndo matokeo yenyewe, hata kama wangehutubia wananchi hadi wakawapigia magoti,na kulia sana bado wasingeshinda.
 
Acheni kulaumiana, cdm ni moto wa kuotea mbali. Pia acheni kutumia gharama kubwa kuficha ukweli kwani watanzania wa leo ni kuku wa kienyeji wanatambua chakula na sumu. Watanzania wanataka matendo na si maneno tena, hasa kwa sisi emmuuuu.
 
Good but myopic analysis. CCM has larger and serious structural problems than simple these few outlined here. If they are serious about governing, they need to rethink and address people's problems. Usifikiri hata mgomo wa madaktari na jinsi walivyoushughulikia kwa mapana yake watu walisahau. Kura zinapigwa kwa sababu nyingi siyo tu kula leo kama kule Igunga walivyofanya. Wachambuzi na watu wanaoipenda Tanzania iendelee na ingare kesho wanaangalia mambo mengi siyo hayo matatizo mepesi ya kina lowasa na sioi tu!!
 
Back
Top Bottom