Hatua za haraka zinahitajika, Wafuatao wameihujumu CCM

Ushindi wa CDM una tafsiri yake kwa CCM naamini kwa watu makini lazima wachanganye na akili zao other wise hawatakuwa na sababu kuendelea kuwa wakaidi mbele ya wananchi
 
Nimeipenda sana tafakuri yako na inaonyesha ni namna gani umekomaa kisiasa.......ila isiishie katika tafakuri hii je nini kinatakiwa kufanyika maana kama hali itaendelea hivi aamin nakwambia 2015 itakuwa mbaya zaidi
 
Iwe kwa kura kiduchu au nyingi CHADEMA WAMESHINDA hongereni sana. Ukombozi wa Tanzania ni wa Watanzania wenyewe. Arumeru mmeonyesha njia. "MMETHUBUTU, MMEWEZA NA MSONGE MBELE"
 
Wewe ni mnafiki huna lolote, hayo makosa yenu unatwambia sisi ili iweje, nenda kazungumze huo ujinga wenu kwenye vikao vyenu na hili ndilo anguko la CCM. Tayari katika bara la Africa tumeshuhudia vyama kadhaa vikongwe vikianguka na sasa ni zamu yenu buriani CCM.

Kidogoo kidogo baadhi ya wanacdm humu ndani muanze kufanana na ushindi wa kisayansi wa Arumeru na kuachana na tabia za matusi na midomo hasi kama huu unaomfanyia mwenzio.Yani unavyoongea na thread ya mwenzio as if JF ni Jukwaa la CDM na si Jukwaa la siasa Tanzania.Yeye kuzungumzia CCM humu ndani ya Jukwaa ni haki yake ya msingi kwa mujibu wa sheria za Jamii Forum nawe una haki sawa kama mwanaCDM au Mwanachama wa chama chochote.

Kuna sababu ya wanaCDM humu ndani ya Jukwaa kuonekana tofauti na siasa za CCM mitaani za matusi na uhuni,badala yake kuendesha siasa za uungwana na ustaarabu.Ni muhimu sana kuwa na IDENTITY ambayo MMM alipata kusema siku za nyuma kuwa Wanacdm lazima wafanane,kwani utofauti wao na CCM ndio sababu ya umma kuamua kuchagua nani anstahiki kwa mujibu wa umma unavyo waona viongozi na wananchama wake.

Yeye kaleta maoni yake uyapendi tetea hoja yako dhidi yake, sikupenda kauri yako ya "nenda kazungumze huo ujinga wenu kwenye vikao vyenu na hili ndilo anguko la CCM. " kwani ulitaka amweleze nani kama si mimi au wewe au wanachama wenzie ambao nao ni member wa Jamii Forum.

CDM kuna sababu kubwa sana kutofautina kihaiba na CCM kwa mambo mengi sana ,kwa kuwa Mwanachama wa CDM atakavyoonekana sasa ndio atasaidia kuongeza imani kwa umma ifikapo mwaka 2015 wananchi kwa ujumla wao waone kuna sababu zote za kuwapa nafasi CDM za kulitumikia Taifa na si wawape CCM kwa sababu hizo hizo watakazo wapimia.Lakini kwa style hii kama ya Lusinde na wenzie tofauti haitoonekana wazi kuwa CDM ni nani na CCM ni nani.
 
Sababu za kushindwa CCM mbali na hiyo ya Lusinde, hizo zingine ukweli wake umejificha sana kama upo; ukweli ni kuwa CDM imejifunza na kujua mbinu wazitumaizo CCM kuiba kula na kupora ushindi.
 
Mkuu hakuna haja ya witch hunt kwa sasa. Kinachotakiwa si kuanza kuparurana makucha bali Chama kukaa chini hasa kinapoelekea uchaguzi wake wa ndani na kujitathmini nini malengo yake hasa?

  1. Kupeana madili ya kandarasi za serikali
  2. Kutumikia wananchi na kuipeleka nchi mbele
  3. Kulinda majambazi na mabaka uchumi provided yanachangia chama na kuvaa nguo za kijani
  4. Kuhakikisha Tanzania inaendelea na maendeleo hayo yanaelekezwa kwa wananchi si viongozi

Baada ya kupata majibu haya then wajiangalie je, malengo hayo yatafikiwa kwa chama kuwa na timu ya aina gani?. Katika ulimwengu wa siasa, under free and fair elections incumbents always huwa na wakati mgumu sana wa kujitetea kwa maneno kwani wananchi waliishawapatia nafasi ya kufanya matendo wakaifiligisa. Kitu pekee kinachoweza kuokoa chama kilicho madarakani si tu kuonesha wapiga kura kuwa ipo kwa ajili yao bali kufanya yale yaliyo na manufaa kwa wananchi. CCM wameshindwa kutumia nafasi hiyo ya kuonesha kuwa wapo kwa ajili ya wananchi na badala yake wanaonesha ubinafsi wa hali ya juu kuanzia bungeni mpaka katika utendaji wa serikali. Anaposimama mtu bungeni na kusema tukifanya hizi tunaitafutia kifo CCM ni dhahiri chama hiki kinaonekana wazi kuwa kinaangalia masilahi yake zaidi ya masilahi ya wapiga kura.

CCM inachotakiwa kufanya ni kuonesha wananchi kuwa wao hawajali kama watadumu milele au la bali wanachojali ni kuona Tanzania inakuwa nchi ya ahadi na neema kwa kila mtu milele (Siyo slogan za uchaguzi). Mkifanya vitu hivi hamna haja ya kutumia wapuuzi kama Lusinde kupanda jukwaani kutoa matusi mbele ya watoto wanaojifunza civics na wazee, kwani waswahili husema chema chajiuza...

Kuendeleza lawama na kutafuta mchawi ni muendelezo wa ubinafsi ndani ya CCM. Kuna wanachama wengi wa CCM hawaridhiki na CCM na wanaiona CDM kuwa ni mbadala. Utatumia polisi kuumiza watu na kuwafanya wasikupinge kwa maandamano ila huwezi tumia polisi kuwafanya watu wakuamini na kutoa ushirikiano katika utawala wako. Yaani itakuwa ni mbio za kuelekea kuzimu kwa Taifa. Kuchukua maamuzi magumu ya kufukuza watu haitasaidia bali kuchukua maamuzi magumu ya kutokulinda mtu atakayepokea au kutoa rushwa katika uchaguzi wa ndani itakuwa ni one step closer. Vyombo vya dola vikiachwa vifanye kazi yake bila lawama wala woga wa watendaji kupelekwa kuwa washauri wa mgambo tandahimba, CCM inaweza kujiokoa. Watanzania wa leo wanaiona CCM kama genge la wezi wa mali ya umma na kufanya maisha yao kuwa duni, CCM needs to fight that image. Ila hilo halitoshi, CCM isiingilie maamuzi ya kura za wananchi, iwe tayari kuachia Ikulu kama ikishindwa, hiyo itakuwa ni another step towards fighting corruption within. Isiwe guarantee kwa mgobea wa CCM kushinda urais, ubunge au nafasi yoyote ile, hii itapunguza wacheza kamali (Wanaotumia hela nyingi kupata teuzi za chama wakijua wazi kuwa wakiisha teuliwa wanakuwa ni kama wameshashinda uchaguzi mkuu na baadae kurejesha pesa zao kwa njia za kifisadi).
 
Hapo ndipo chchm inapokosea, haina haja ya kuanza kukomoana sasa. siasa ni kama mchezo kuna kushindwa na kushinda. Kubalini wananchi hawakuwaelewa jipangeni kwa chaguzi zijazo huku mkiimarisha chama. Pia lazima mfanye study wanchii wanataka nini ili mtengeneze approaches nzuri na hamna sababu ya kulalamika coz dola yote iko chini yenu. Ni hayo tu. Na kwa Cdm mna haki na kila sababu ya kusheherekea ushindi lkn kaeni mkijua ngoma mbichi sanaaa na kazi kubwa iko kwenu hiyo 2015 hasa kubadili upepo wa kisiasa katika ngome za maadui maeneo ya vijijini. Ni hayo tu!!!
 
kuhakikishia Uchaguzi mdogo wowote utakaotokea Kuanzia sasa,CHADEMA watashinda zote hadi 2015.Hakuna sijui cha makosa yenu wala nini? Wewe ndo ulikua unajitapa hapa oooh,mtashinda.Kwa nini hukutoa maangalizo hayo kwenye timu yenu ya kampeni? Mkuu,this is an Indicator for your Information.Hata JK angeenda wembe ni uleule.

Eti Ushindi kiduchu.Upi ni kiduchu kati ya huu na ule wa kwenu wa kuchakachua kule Igunga?

Pole lakini.Najua umepata wakati mgumu hata kuandika thread hii.Umeonyesha ukomavu

Mkuu naungana na wewe moja kwa moja kwasababu humu ndani nilkuwa naona ushauri mwingi kwenda CDM na pia nafikiri walikuwa wanaufanyia kazi sana lakini huyu gamba aliyeleta ushauri muda huu sio wakati wake kwani angetakiwa awashauri kabla ya jana CDM ni chama makini pia washauri wake ni Great thinkers wanachukua ushauri mpaka huku JF
 
Wewe ni mnafiki huna lolote, hayo makosa yenu unatwambia sisi ili iweje, nenda kazungumze huo ujinga wenu kwenye vikao vyenu na hili ndilo anguko la CCM. Tayari katika bara la Africa tumeshuhudia vyama kadhaa vikongwe vikianguka na sasa ni zamu yenu buriani CCM.

Magamba hoi.
 
Mkuu haya nafikiri na siri za mambo yenu mliyofanya ndani ya vikao kama kulikuwa na harufu ya rushwa au kutokukubalika kwa watu wenu hayo ni mambo ambayo kama mwanachama wa chama chenu mkayaongelee ndani ya vikao vyenu
Mtoane kafara nyie wenyewe
Maana hata kama Lusinde atanyang'anywa kadi haituhusu mkaongelee huko ndani ya vikao vyenu
Au kama kuna kuvuana gamba kamalizeni humo ndani ya vikao vyenu
Au UVCCM hawakuwa wamoja kwenye kampeni ni mambo yenu
Kama uliona udhaifu wa kampeni zenu kwa nini hukuwaambia watu wa chama chako kubadilisha mbinu
Na uache unafiki ushindi kiduchu hivi ushindi unaujua wewe
Zaidi ya kura 6000 sio ushindi kiduchu ni ushindi tosha kabisa
Unamkumbuka mbunge wenu wa Shinyanga mjini alishinda kwa kura ngapi
 
TUWAELEWE YUPI KAHUJUMU? MARA KIBABAAAJ AKA LUSINBE MARA EL alikuwa anajipima kama 2015 agombee urais au amwence dr ncmb wa ema kuleata, mara ooh BM kachemsha. mara chemba wa Mgulu sasa yupi? All in All TULIAZNA NA MUNGU TMEMALIZA NA MUNGU JINA LA BWANA LIHIMIDIWE. Nyie BUTIKU, WARIOBA, KITINE WAKISEMA MNASEMA WAMETUMWA SASA KAWAONENI WALE WAZEE WANA DAWA YA CCM KUZIA KIFO KIKUU UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA NA ULE WA 2015
 
Haya nendeni mkayazungumze kule kamati kuu na halmashauri kuu kwani kwa sasa unaonekana unaweweseka tu no body is here to draw attention to nonsense. Ushindi ni ushindi tu huwezi kuu grade kutokana na ghilba na wivu
 
Ndugu zangu wana JF,
Awali ya yote naomba niwapongeze kwa ushindi KIDUCHU mlioupata kule ARUMERU, kiukweli sikupenda CDM iibuke washindi ila nilipenda CCM ishindwe. Ninakiri kuwa kuna tatizo kubwa sana tokea kura za maoni, nguvu ya ushawishi na pesa nyingi zilisababisha SIOI ashinde ilihali kulikuwa na viashiria vya rushwa!

Kuna sababu nyingi zilizopelekea CCM kutoshinda uchaguzi ule ambazo kiukweli zimenikosesha raha na hata kutype kwenye keyboard nashindwa!

1) Lusinde alipunguza idadi ya kura Arumeru kwa kiasi kikubwa, ukitumia lugha mbaya kama zile usitegemee mtu akuchague, inshort ningekuwa na maamuzi katika CCM lusinde ningemnyang'anya kadi ya chama.

2) Waliokuwa ndio wanaongoza kampeni hawakuweza kutoa sababu ni kwa nini muda wote ambao jimbo lilikuwa chini ya CCM na kero mbali mbali hazikushughulikiwa na leo wanaahidi kuzishughulikia, Mfano: Ni ukweli usiopingika mtu kama MKAPA hawezi kuwashawishi wana ARUMERU kuwa atamshauri Kikwete wakati alikuwa Rais na hakuweza kutekeleza matatizo hayo. Mi nafikili ilitakiwa kwa wanaccm kukiri makosa na kuonyesha ni kwa vipi watasahihisha makosa yao, Lakini baada ya kutumia njia hii wakajikuta WANAROPOKWA na kutumia lugah zisizo na staha.

3) Kutumia watu wenye kashfa na wanaoongoza katika makundi katika CCM tena hao hao wanajulikana kuwa hawapo katika kundi moja kama OLE SENDEKA na LOWASA, hii ilidhihirisha Unafiki wa aina yake, Haiingii akilini watu hawa ambao kila kukicha wanaitana mafisadi na kushutumiana mbele ya camera za waandishi leo wanapanda jukwaa moja. Tatizo kubwa ni kuwa wanayoyasema na wanayotatenda ni tofauti tena kwa nyuzi 180[SUP]0[/SUP](Diferent Direction)

4) UVCCM hasa wa arusha nao hawakwepeki katika hili, katika kufikili wanawakomoa wale waliopinga uteuzi wa sioi kwa kuwa unanuka harufu ya rushwa na wengine waliotilia shaka juu ya uteuzi wa sioi wao wakatumia nguvu na wingi wa kura zao kumchagua Sioi lilikuwa kosa la kihistoria.

5) Hakukuwa na kauli ya pamoja katika kampeni za CCM kila aliyepanda jukwaani alisema yake, in short ilikuwa kama watu wamechanganyikiwa.

Conclusion:
Huu ni uthibitisho kuwa LOWASA na kundi lake hawakubaliki katika jamii, na CCM isije kufanya kosa 2015

Hongera CDM ingawa ushindi wenu unatokana na UJINGA na UDHAIFU wa CCM

Ninachokushauri mjomba, achana na hayo. Jali zaidi maisha yako. Huwezi kushindana na CCM. Mambo ya ngoswe muachie ngoswe mwenyewe!
 
Wakulaumiwa ni chama kama chama, kwa kushindwa kuwaomba radhi wananchi wa Arumeru kwa matusi ya nguoni tena mbele ya watu wazima na watoto, watu wenye akili zao walidhani Lusinde alikuwa ameghafilika kama binaadam lakini kitendo cha kukaa kimya bila chama kumkana Lusinde na kauli zake kilimaanisha CCM ndivyo walivyo. Binafsi simlaumu Lusinde kwa aliyoyafanya kwani yeye ni binaadamu na anamapungufu yake kama watu wengine waliovijiweni wakumlaumu ni aliyemtuma kufanya hicho alichokifanya tena nina wasiwasi atakuwa ni mtu mwenye kiti wa chama maana haiwezekani mtu mwingine akamtuma mtu kama Mkapa na Lusinde kwenda kutukana mbele ya wananchi
 
Ulikuwa unachonga sana hapa Mkuu.. mpaka nikafikiria ni mmojawapo wanaokula kwa raha.. Ucimcingizie lusinde matuci kwa kusababisha nyie kukosa kura..! Mkuu chama chako hakikuwa na jipya la kuwaahidi wana Arumeru..! Maana wana maboxi ya ahadi toka miaka hiyo toka CCM.. Na hakuna hata ahadi moja iliotekelezwa..! Tatizo lenu mlidhani watanzania wa miaka ile ndo hawa wa sasa.. Kwamba hawabadiliki..! Kwa hiyo mkaja na ahadi nyingine zinazofanania zile zile.. Na hii sio Arumeru peke yake.. Mna hali ngumu na cjui mtatokea wapi.. Najua mtaongeza nguvu katika kujaribu kukifarakanisha CDM.. Lakini mkumbuke hii ni 2012.. CDM inafanya siasa huku ikijifunza makosa..
Ushauri wangu Mkuu jaribuni kuonyesha japo mna mioyo kwa kutojaribu kuzuia mabadiliko.. Mabadiliko yanayokuja hayana tofauti na tufani (hurricane) ambayo no one can dare to stop it..! kama slogan ya CDM inavyosema.. its people's power..
 
Back
Top Bottom