Hatua za haraka zinahitajika kusimamisha vita (Civil War) Ngara

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
WanaJF,

Kwa taarifa zilizotufikia sasa, ni kwamba Wanyarwanda walihamishia Ng'ombe wao Bushubi (Ngara) na wanalisha mashamba ya wenyeji kwa jeuri kubwa. Inaonekana uongozi wa serikali za vijiji na wilaya kama kuna kitu wanaficha.
Kwa wale wanaofuatilia taarifa, iliwahi kulipotiwa kuwa DC wa Ngara ameruhusu wanyarwanda kuingiza mifugo nchini. Katika hatua hiyo, DC huyo alimbambikia kesi mwandishi wa ITV aliyeandika habari hiyo. Mpaka leo kesi inaendelea ...

Mpaka jana taarifa ni kwamba imezuka vita kubwa (Civil War) kati ya Wafugaji hao na Wakulima wa Bushubi

1. Inasemekana jana 31/5/2011 huko Mkalinzi- Mganza waliuawa / walijeruhiwa vibaya watu 8
2. Leo 1/6/2011 huko Keza Mlonzi nako wameuawa / wamejeruhiwa watu 6

Uongozi a namna hii, hauna tija. Ngoja tusikie kama Radio Kwizera watatangaza chochote. Walioko karibu na tukio, mtujuze tafadhari.
 
khe! Watanzania wanateseka ndani ya ardhi yao kwa ajili ya watu wachache wasiokuwa na uzalendo
 
Yes
Keep watching ,tupo njiani kupata taarifa hii kwa ukweli,punde mnaweza kuona hata video hapa hapa.

belived watu 6 wameuawa katiika rabsha hizo.

tunakwenda kwa siri sana unajua hapa kagera kuna maeneo ni HATARI SANA kwa sisi kama waandishi kufika na kupiga picha nk

Subiri tu.
 
Mkuu tunasubiri habari hizo
 
Nashukuru sana. Kijiji cha mulonzi na mukalinzi naambiwa kuna watu zaidi ya hao wameuawa. Hata hivyo DC wa ngara hataki habari hii kufahamika maana ameishapokea mrungula toka kwa hawa wanyarwanda!

Nadhani mnafahamu kuwa alimbambikia yule mwandishi wa ITV kesi kuwa si raia wa Tanzania!

Keep us informed p'se.
 
Yes
Keep watching ,tupo njiani kupata taarifa hii kwa ukweli,punde mnaweza kuona hata video hapa hapa.

belived watu 6 wameuawa katiika rabsha hizo.

tunakwenda kwa siri sana unajua hapa kagera kuna maeneo ni HATARI SANA kwa sisi kama waandishi kufika na kupiga picha nk

Subiri tu.

take care of yourself
 
wanao uawa ni Watanzania am,a wanyarwanda?

Mbona wote ni ndugu moja? Sasa tuanze kuona matunda ya kukurupukia jumuia za Africa Mashariki. Kuna watu tunawaingiza kwenye jumuia ambao watakuja kuwa miiba ya kudumu kwa watoto na wajukuu zetu.
 
DC wa aina gan huyo anaeweza kutetea wageni na kuacha raia wake wanaangamia? Huyu ni sawa na wale madc wanaoacha watu wanakula mizizi au wanakufa kabisa wakigoma kutangaza njaa wilayani kwao kulinda ajira.
 
Mkuu wa wilaya ya Ngara jana jioni alifanya ziara kwenye vijiji ambako watanzania wameuawa. Hata hivyo Mkuu wa wilaya hakuambatana na waandishi wa habari. Waandishi waliokwenda wenyewe, aliwafukuza na walipomfuata baadaye ofisini kwake, alikataa kuongelea suala hilo. Mpaka sasa majina ya waliotambuliwa ni matatu. Yakikamilika yote, tutafamishana.
 
Mgogoro huu ni wa siku nyingi sana viongozi wa Wilaya kama Mkuu wa Wilaya,Mkurugenzi,OCD,Afisa uhamiaji wanyarwanda ndio mradi wao mkubwa.Wanyarwanda wanawahonga viongozi wetu pesa nyingi ili waweze kuchungia mifugo yao katika eneo la Tz kwao rwanda hawezi sheria zao zinawabana mwananchi wa kule haruhusiwi kuwa na ng'ombe zaidi ya 5.Kimbilio lao kuu ni Tz ambako sheria zao hazifuatwi.

Viongozi wote hao akiwemo mkuu wa wilaya hawezi kuzungumza lolote kwa sababu alishapewa mlungurana huu ndio mradi wao mkubwa, kuna kipindi DC alipewa na wanyarwanda milion 300 na kuahidiwa milion 150 nyingine ili awaponde waTz kuwa wao ndio wakorofi bahati mbaya dili likavuja waTz wakamwita mwandishi wa ITV siku ya mkutano wa hadhara,DC baada ya kumuona mwandishi akamfukuza wananchi wakamjia juu endapo atamfukuza huyo mwandishi wanasusia mkutano wake na kweli mkutano ulivunjika baada ya hapo mwandishi wa ITV aliundiwa zengwe kua sio mTZ na makashfa mengi tu

Wananchi wanateseka sana,wanyarwanda ni wakorofi sana wananywesha ngombe zao kwenye visima vya wananchi,wanalisha ngome zao kwenye mashamba ya wa Tz,imagine wakiwa wanchunga ngombe hao wanyarwanda wanakua na bunduki ya SMG na magazine 6.

Suala ya Wilaya ya Ngara kwa kweli ni hatari sana

Mungu ibariki Tz
 
Back
Top Bottom