Hats off to Jenerali Twaha Omar Ulimwengu

Mbona uanaleta kashfa ndugu....wewe hunijui sasa unawezaje kusema sina akili timamu...nmekuomba utueleze huyu Jenerali ni tapeli kivipi wewe unakuwa mbogo...sikatai yeye ni binadamu na labda alipata kukukosea huko nyuma lakini huwezi ukam-generalized kwa wengine tusiomjua hivyo umjuavyo....kwa busara tu tueleze hafai vipi na tukiridhika basi nasi tutamuita tapeli

Nijuavyo mtu anaeganga njaa ni yule ambae daima kwake ni kukamilisha mlo kwa juhudi za wengine .... nimjuavyo Ulimwengu sidhani kama yuko hivyo...yes Mramba yuko mahakamani...Mkapa ana kinga hawezi kupoelekwa mahakamani....Chenge yuko mahakamani....RA atafika tu usijali....ila nimekwambaia pale awali kama Jenerali ni tapeli kama unavyodai je amewahi kushatakiwa? kama ni hivo tueleze hapa...JF THE HOME OF GREAT THINKERS

Great thinker ehee khe khe khe huo msemo au? Soma uelewe, wapi nimekwambia huna akili timamu? Wacha munkari mkuu huwezi ambiwa maana kwa munkari.
 
Originally Posted by Wacha1
Hivi unafahamu maana ya kuganga njaa? Hebu tueleze matapeli kama RA, BWM, JK, Chenge , Mramba etc wote wamefikishwa mahakamani? kufikishwa mahakamani ndio proof? Mkuu I know this guy ni tapeli wa kutupwa na mjanja mnjanja sana kama utakumbuka wale aliokuwa nashirikiana nao kama Salva, marehemu Rutayisingwa etc. Kama ungekuwa na akili timamu usingeropoka.

Kwako wewe mimi nimeropoka...hivo sina akili timamu
 
Mimi nashindwa kuelewa tunapozungumzia watu kutoka nje ....Kama Bashe,Ulimwengu,Kinana,Meghji,Amir Jamal...hawa wote ni wazaliwa wa TZ sio kama kweli wamekuja na kuja kuomba uraia nchini...Kwa maana ingine makosa sio yao kuzaliwa nchini.
Sasa inakuwaje tuna wazungumzia kama vile ni wakuja?...hawa ni wabongo kama sisi hata wewe unajuaje babu yako alikotoka?

Inaonekana watu tumeanza kujijengea chuki hapa maana kuna post nyingi zinaonyesha kama vile ka u racist unamea......mimi nakubaliana na u racist lakini sio kwa wazawa wenzetu bali wale wa kuja.
tatizo langu ni sisi/nchi kuwatumia watu hao positively, badala yake tunawatumia kuhujumuuuuuu nchi/kutuhujumu sisi wenyewe, mfano kuna makampuni yana mishara miwili, yaani wewe wako utakuwa tofauti na mwingine kisa nasabaaaa., wengine kazi yao ni kuleta zaidi watu wa asili ya kwaooooo, sasa hapa utasema tunawatumia vizuri watu hawa au tunatumiwa vibaya (sisi).
mfano jenerali namuunga mkono kwa sababu yeye mwenyewe ameji nasaba na sisi kwa shida na raha, na hajatutumia vibaya, lakini kuna wengine bila kuwawekea control order, utalia na kujutia. kwa hiyo hisia ya u-racism ondoa.
wengine hapa wakianzisha shule za kabila zao itakuwa shida, lakini kuna wengine wana shule za asili ya kwao, sasa hapo utasema watu hao wana nia nzuri na tz, na hizo shule kutokana na control order wanaweka wanafunzi wachache, wa jamii wasio na nasaba nao kufunika uchinvi wao tena wa vigogo.
nafikiri kwa maelezo haya mafupi utakuwa umeelewa.
 
Mbona uanaleta kashfa ndugu....wewe hunijui sasa unawezaje kusema sina akili timamu...nmekuomba utueleze huyu Jenerali ni tapeli kivipi wewe unakuwa mbogo...sikatai yeye ni binadamu na labda alipata kukukosea huko nyuma lakini huwezi ukam-generalized kwa wengine tusiomjua hivyo umjuavyo....kwa busara tu tueleze hafai vipi na tukiridhika basi nasi tutamuita tapeli

Nijuavyo mtu anaeganga njaa ni yule ambae daima kwake ni kukamilisha mlo kwa juhudi za wengine .... nimjuavyo Ulimwengu sidhani kama yuko hivyo...yes Mramba yuko mahakamani...Mkapa ana kinga hawezi kupoelekwa mahakamani....Chenge yuko mahakamani....RA atafika tu usijali....ila nimekwambaia pale awali kama Jenerali ni tapeli kama unavyodai je amewahi kushatakiwa? kama ni hivo tueleze hapa...JF THE HOME OF GREAT THINKERS

Jenerali kuwa tapeli au kutokuwa si swali langu. Mkuu kuwa tapeli mtu mpaka ashitakiwe? Hasa utapeli wa kidokozi.
 
tatizo langu ni sisi/nchi kuwatumia watu hao positively, badala yake tunawatumia kuhujumuuuuuu nchi/kutuhujumu sisi wenyewe, mfano kuna makampuni yana mishara miwili, yaani wewe wako utakuwa tofauti na mwingine kisa nasabaaaa., wengine kazi yao ni kuleta zaidi watu wa asili ya kwaooooo, sasa hapa utasema tunawatumia vizuri watu hawa au tunatumiwa vibaya (sisi).
mfano jenerali namuunga mkono kwa sababu yeye mwenyewe ameji nasaba na sisi kwa shida na raha, na hajatutumia vibaya, lakini kuna wengine bila kuwawekea control order, utalia na kujutia. kwa hiyo hisia ya u-racism ondoa.
wengine hapa wakianzisha shule za kabila zao itakuwa shida, lakini kuna wengine wana shule za asili ya kwao, sasa hapo utasema watu hao wana nia nzuri na tz, na hizo shule kutokana na control order wanaweka wanafunzi wachache, wa jamii wasio na nasaba nao kufunika uchinvi wao tena wa vigogo.
nafikiri kwa maelezo haya mafupi utakuwa umeelewa.

Mimi simung'unyi maneno, wahindi ni wabaguzi, ni wezi na matapeli na nina ushahidi mwingi tu! tena ni maadui wa nchii kabisa! Subiri iko siku wananch wataamka tu!
 
Jenerali kuwa tapeli au kutokuwa si swali langu. Mkuu kuwa tapeli mtu mpaka ashitakiwe? Hasa utapeli wa kidokozi.

Ni kujuzana tu ndugu yangu...unajua mchangiaji alitoka nje ya hoja kidogo....unapomuita mtu tapeli shurti uwe na ushahidi na mojawapo ni kuwa kafikishwa mahakamani
 
Mimi nashindwa kuelewa tunapozungumzia watu kutoka nje ....Kama Bashe,Ulimwengu,Kinana,Meghji,Amir Jamal...hawa wote ni wazaliwa wa TZ sio kama kweli wamekuja na kuja kuomba uraia nchini...Kwa maana ingine makosa sio yao kuzaliwa nchini.
Sasa inakuwaje tuna wazungumzia kama vile ni wakuja?...hawa ni wabongo kama sisi hata wewe unajuaje babu yako alikotoka?

Inaonekana watu tumeanza kujijengea chuki hapa maana kuna post nyingi zinaonyesha kama vile ka u racist unamea......mimi nakubaliana na u racist lakini sio kwa wazawa wenzetu bali wale wa kuja.

Uracist definition yake unaijua? How does someone become a racist by questioning the citizenship of an alien in his/her country. Au umeshaona wanatuhumiwa wahindi tu au baniani au warundi peke yao. Kuwa specific kwanza kabla hujawatuhumu watu humu ndani. Tofautisha being patriotic na being a racists.
 
tatizo langu ni sisi/nchi kuwatumia watu hao positively, badala yake tunawatumia kuhujumuuuuuu nchi/kutuhujumu sisi wenyewe, mfano kuna makampuni yana mishara miwili, yaani wewe wako utakuwa tofauti na mwingine kisa nasabaaaa., wengine kazi yao ni kuleta zaidi watu wa asili ya kwaooooo, sasa hapa utasema tunawatumia vizuri watu hawa au tunatumiwa vibaya (sisi).
mfano jenerali namuunga mkono kwa sababu yeye mwenyewe ameji nasaba na sisi kwa shida na raha, na hajatutumia vibaya, lakini kuna wengine bila kuwawekea control order, utalia na kujutia. kwa hiyo hisia ya u-racism ondoa.
wengine hapa wakianzisha shule za kabila zao itakuwa shida, lakini kuna wengine wana shule za asili ya kwao, sasa hapo utasema watu hao wana nia nzuri na tz, na hizo shule kutokana na control order wanaweka wanafunzi wachache, wa jamii wasio na nasaba nao kufunika uchinvi wao tena wa vigogo.
nafikiri kwa maelezo haya mafupi utakuwa umeelewa.

Tatizo ni kwamba viongozi wa tanzania wana njaa kali na wewe ukikataa wengine wanakubali ndio maana wahindi wanatuweza maana wanajua atatokea mbigiri moja kati yetu atakubali tu.
 
Mimi nashindwa kuelewa tunapozungumzia watu kutoka nje ....Kama Bashe,Ulimwengu,Kinana,Meghji,Amir Jamal...hawa wote ni wazaliwa wa TZ sio kama kweli wamekuja na kuja kuomba uraia nchini...Kwa maana ingine makosa sio yao kuzaliwa nchini.
Sasa inakuwaje tuna wazungumzia kama vile ni wakuja?...hawa ni wabongo kama sisi hata wewe unajuaje babu yako alikotoka?

Inaonekana watu tumeanza kujijengea chuki hapa maana kuna post nyingi zinaonyesha kama vile ka u racist unamea......mimi nakubaliana na u racist lakini sio kwa wazawa wenzetu bali wale wa kuja.
halafu huyu Amiri Jamal mwenye aliende kuzikwa canada, na ndio aliye shikilia wizara ya fedha, sasa sijui mwenzetu hii tafsiri yako hapa ikoje, ndio maana waze husema kua uyaone, kuna wengine tulikuwa nao hapa shule za secondary, ufundi, uganga nk nk walikuwa nasisi kwenye mashirika yetu haya ya kiserikali/umma, lakini rwanda baada ya vita hao wakatimukia kwao? sasa sijui kwao ni wapi? kibondo, kasulu, karagwe au nchi jirani?
kwa hiyo watu kama hawa lazima "control order" iwepo wengine walikuwepo ug , wakaondoka na vifaa vya kijeshi. nk nk
nenda leo hii malasyia/singapore, nchi hizi ni new tigers on the block, na wameendelea saana kwa sababu ya uwepo wa wachina/na wa hindi lakini leo hii wenyewe wanatahayuri uchumi/uwepo wa watu wa asili ya nje ya malasyia/singapore.
tuje hapa zanzibar na bara wao wenyewe wanasema bila kuwepo kwa taratibu, ipo siku zanzibar itakuwa zanzibara, hivyo wangependa kuona kunakuwepo kwa utaratibu kidogo wa ku-control hii hali.
kwanza unajua kwamba kuna nchi moja ya bara la asia ambalo sisi mpingo wanatuona kama ni manyani? wana kuchekea kwa sababu unabidi, ikiwezekana wangependa kukuona u don't exist.
ukienda kwa nchi za wenzetu kama sweden , etc wataangalia huluka yako hadi miaka 5 ili kuweza kusema wewe angalau unafaa faa kuwa mwenzetu yaani kama huna criminal record, enzi zile wa tanzania walivyo vamia sweden, hiyo ilikuwa ni mojawapo ya vigezo vya ku-fit in
 
Rai ya Jenerali

jenerali2.jpg
Nkaba nyin'embwa yange

lC.gif
Jenerali Ulimwengu​
Agosti 18, 2010
rC.jpg

WIKI jana nilijadili suala la watu wazito, wenye nyadhifa kubwa, wenye historia zinazoeleweka, na wenye wingi wa miaka inayowatambulisha kama wazee, lakini hujidharaulisha kwa kutoa matamko ya kipuuzi yasiyofanana na sifa hizo alimradi wajibu hoja za kudumu kwa majibu mepesi ya mpito. Wiki jana ilikuwa ni ya Pius Msekwa, Makamu wa Mwenyekiti wa CCM na matamko yake kuhusu uoza ndani ya chama chake. Wiki hii tena, mzee mwingine wa CCM, Katibu wa Uenezi, John Chiligati, naye ameamua kujiingiza katika kundi hilo la kujisemea ‘bora liende”.
Chiligati, yeye, ameamua kumzungumzia kijana wa CCM, Hussein Bashe, ambaye hivi majuzi tu, mjini Dodoma, amekatizwa safari yake ya kuwania ubunge kutokana na kile kilichoelezwa kuwa tatizo la uraia.
Chiligati aliwaelezea waandishi wa habari mjini Dodoma alfajiri ya Jumapili kwamba Bashe ameachwa katika mchujo wa wagombea kwa sababu yeye ni raia wa Somalia, na kwa hiyo si raia wa Tanzania. Aliongeza kusema kwamba chama chake kilifanya uchunguzi kikishirikiana na Idara ya Uhamiaji na ndipo ikagundulika kwamba Bashe si raia wa Tanzania, hata kama alizaliwa Tanzania.
Hadi hapo sioni tatizo. Tatizo linakuja pale Chiligati alipotamka kwamba kesi ya Bashe ni sawa na ile ya mwandishi wa makala hii , “aliyekuwa kada wa CCM” na akavuliwa uraia wake katika miaka ya nyuma.
Nakiri kungali na mapema kwamba haipendezi kwa mwandishi wa makala hii kutumia safu hii kuzungumzia suala linalomhusu binafsi. Nasema haipendezi, lakini ni halali katika hali fulani fulani. Nitajaribu kueleza hapa chini.
Wahaya husema kwamba mtu akibanwa mbavu kuhusu jambo alilotenda na akataka kusema uongo atasema, nkaba nyin’embwa yange. Nilikuwa pamoja na mbwa wangu. Maana yake ni kwamba, kama mnataka ushahidi wa hili ninalosema muulizeni mbwa wangu.
Kwa mitindo mbali mbali na katika mazingira tofauti hii ni silaha inayotumiwa na watu wanaotaka kusema uongo unaofanana na ukweli. Kwa mfano, inawezekana kweli Bwana Bigambo alikuwa na mbwa wake wakati wa tukio husika, lakini haiwezekani kwa mbwa wake kutoa ushahidi, kwa hiyo kuwapo au kutokuwapo kwa mbwa huyo hakuna uhusiano na ushahidi wa Bigambo. Anapoteza lengo tu, na ingawa kwa juu juu anasema ukweli (mbwa wake alikuwapo) lakini anasema uongo (mbwa hawezi kutoa ushahidi).
Ili kuwafariji akina Chiligati, ninaweza kuwaarifu kwamba hawako peke yao, kwani hata wakubwa wa dunia wanatumia vijisilaha kama hivyo wanapokuwa wameshikwa ‘pabaya.’ Miaka kadhaa iliyopita, wakati Marekani wanang’ang’ana kwenda Iraq kumwondoa Saddam Hussein, Marekani walipambana na upinzani mkali mno kutoka kwa maswahiba wao wa Magharibi waliokataa kubariki vita ya Marekani dhidi ya Iraq. Tunamkumbuka Dominique de Vilpein, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa na jinsi walivyoshikana mashati (kwa maneno) ndani ya mkutano wa Baraza la Usalama.
Katika mabishano makali yaliyofanyika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kila aina ya mbinu zilitumika kutetea upande huu na ule, kila mmoja akivutia upande wake. Ilikuwa dhahiri kwamba dunia haikukubaliana na mantiki ya Marekani kuivamia Iraq, na kwamba Marekani walikuwa wamedhamiria kufanya kile walichoazimia na kwamba wangetumia maguvu, hata kama Umoja wa Mataifa ungewakataza.
Lakini, kwangu mimi binafsi, tamko lililoashiria kuchoka kwa uchovu na ubabaishaji wa mantiki ya Marekani ni pale ofisa wake mwandamizi alipoiingiza Tanzania katika ubishi huo, kwa kutamka kwamba hata Tanzania ilipoivamia Uganda haikufanya hivyo kwa kibali cha Umoja wa Mataifa. Ati nkaba nyin’embwa yange.
Huyu msemaji wa Marekani alifanya purukushani (hii ndiyo maana halisi ya neno hili) kuhusu chanzo cha vita baina ya Tanzania na Idd Amin, yaani uvamizi alioufanya Amin dhidi ya Tanzania, na kwamba ilichofanya Tanzania ilikuwa ni kutumia haki yake ya msingi ya kujibu mapigo katika ulinzi wa ardhi yake. Msemaji wa Marekani alisema ukweli (Tanzania haikupata ridhaa ya Umoja wa Mataifa) wakati papo hapo akisema uongo (Iraq haikuivamia Marekani).
Mantiki ya nkaba niny’embwa yange huweza kupata mashiko miongoni mwa wasemaji na wasikilizaji waliojijengea utamaduni wa fikra nyepesi zinazotafsirika katika matamko mepesi sawia. Katika jamii iliyojizoeza kufanya mambo yake (pamoja na kufikiri) fasta-fasta, muhimili mmoja wa mtazamo wa maisha ni kwamba hutakiwi kuumiza kichwa chako kufikiri. Unachotakiwa ni kuwa mjanja ili uweze kubakia bambucha.
Hebu tuangalie Chiligati anasema nini kuhusu kijana Bashe na mwandishi wa safu hii. Kijana huyu alikuwa, hadi juzi (sijui leo) kada wa chama-tawala, tena kada wa msitari wa mbele ambaye amekifanyia kazi chama hicho hadi juzi. Mwandishi huyu wakati akivuliwa uraia hakuwa tena kada wa chama hicho, akiwa amehitilafiana na uongozi/utawala wa juu wa chama hicho kuhusu masuala ya msingi.
Kijana Hussein Bashe, ambaye sasa anatolewa kafara na wale alioamini ni wazee wake, alikuwa bado anayo hamu ya kukitumikia chama chake katika wadhifa wa juu zaidi. Mwandishi huyu alikuwa amestaafu ubunge na ujumbe wa NEC na alikuwa amejikita katika harakati za asasi za utetezi pamoja na uandishi na uchapishaji wa magazeti makini ambayo hayakusita kuiambia serikali na chama-tawala kwamba “mfalme yu uchi, na korodani zinaonekana.”
Utamaduni wa uroho na kunyang’anyana matonge ndani ya chama-tawala, kama tulivyoushuhudia siku za hivi karibuni huzaa uchafu wa kila aina kiasi kwamba mtu anahitaji pua zenye sugu iliyoingia sugu ili asisikie uvundo unaotoka huko. Katika utamaduni huo, watu hutafunana wenyewe kwa wenyewe, wakubwa wakiwatafuna wakubwa wenzao, wakubwa wakivimeza vitoto vyao, na vitoto navyo viking’atang’ata visigino vya wazazi wao.
Naamini kwamba wamo watu ndani ya chama-tawala ambao hawakumtaka Hussein (kwa sababu walitaka mbunge wao) na wakaona kwamba mbinu ya kumzuia ni hiyo ya uraia, hasa kwa sababu sura yake inaashiria asili yake. Huyu wamemuweza, kwa sababu, pamoja na maneno ya Chiligati, bado ni dagaa, hajawa hata kambale, achilia mbali papa. Mbona wengine hawawagusi?
Katika majungu wanayopikiana ndani ya chama-tawala, baadhi ya wanachama wasiomtaka Mustafa Mkulo walipeleka pingamizi dhidi yake na wakaenda Dodoma kushadidia pingamizi yao wakati wa kikao cha NEC. Chiligati hakusema kama uamuzi juu ya Mkulo ulitoka ndani ya Idara ya Uhamiaji au ndani ya NEC. Kati ya Bashe na Mkulo bila shaka ipo tofauti.
Shauri analoliingiza Chiligati katika sakata ya Bashe ambalo linamhusu mwandishi huyu lilianza kwa watawala kutafuta njia ya kunyamazisha baadhi ya sauti za ‘kuudhi.’ Kinara wa kampeni kuhusu uraia wa mwandishi huyu alikuwa ni kachero mwandamizi mstaafu ambaye kwa wakati huo alikuwa amelazimishwa kujiuzulu uwaziri katika serikali ya rafiki yake, Benjamin Mkapa, kwa sababu alikuwa amegundulika na gazeti la mwandishi huyo kuhusiana na wizi wake wa fedha za Serikali kwa kisingizio cha ugonjwa bandia wa mkewe.
Waziri huyo mwizi (labda tumwite ‘mwiziri’), badala ya kwenda jela, akawa anahaha mitaani na kuapa kwamba ama zake ama za mwandishi huyu. Waziri huyo akafunga safari hadi mikoa ya magharibi, na hata katika nchi jirani, kutafuta ‘ukweli’ kuhusu mwandishi huyu, na kufikia hitimisho kwamba mwandishi huyu si raia wa nchi hii, wakati wote akiungwa mkono na mkuu wa nchi wa wakati huo. Wote wanajua kilichofuatia.
Mwandishi huyu, tofauti na Bashe, hakuwa anatafuta cheo wala nafasi ya uongozi; alikwisha kuchoshwa na unafiki uliokuwa umemzunguka kila mahali, na hususan wanasiasa uchwara wanaoingia madarakani kwa ahadi ambazo, ukiwachunguza kwa undani, si kwamba wanashindwa kuzitekeleza, bali hawajawahi kuwa na nia yo yote ya kuzitekeleza.
Tusichanganye mambo, hata kama utamaduni wetu ni wa ‘chakachua.’ “Usomali” wa Bashe hauna uhusiano na uamuzi wa NEC (mbona chama-tawala kinao ‘Wasomali’ wengi tu, tena waandamizi na hawazungumzwi?) na wala hauna uhusiano wo wote na tatizo lililompata mwandishi huyu. Na wala maamuzi mengine yaliyochukuliwa na NEC kwa visingizio (sababu zina sehemu zake) kadhaa hayafanani na maamuzi mengine ambayo hayafanani na visingizio hivyo:
Watoa rushwa na wanunua kura wamo ‘kibao’ ndani ya orodha iliyopitishwa na chama-tawala, na pia majangili maarufu na maharamia mashuhuri wa kila aina. Wakabila, wadini, wabaguzi wa rangi, washirikina, walaghai, wauaji wa albino, wauza unga.. kama kuna dhambi isiyowakilishwa ndani ya orodha ya wagombea waliopitishwa juzi na NEC, dhambi hiyo haijateremshwa duniani.
Wakubwa, kwa kuamini kwamba wananchi wanaowatawala ni wajinga, wanaendelea na kauli zao nyepesi, ambazo zinaashiria fikra nyepesi.

Raia Mwema Toleo Na 147
 
halafu huyu Amiri Jamal mwenye aliende kuzikwa canada, na ndio aliye shikilia wizara ya fedha, sasa sijui mwenzetu hii tafsiri yako hapa ikoje, ndio maana waze husema kua uyaone, kuna wengine tulikuwa nao hapa shule za secondary, ufundi, uganga nk nk walikuwa nasisi kwenye mashirika yetu haya ya kiserikali/umma, lakini rwanda baada ya vita hao wakatimukia kwao? sasa sijui kwao ni wapi? kibondo, kasulu, karagwe au nchi jirani?
kwa hiyo watu kama hawa lazima "control order" iwepo wengine walikuwepo ug , wakaondoka na vifaa vya kijeshi. nk nk
nenda leo hii malasyia/singapore, nchi hizi ni new tigers on the block, na wameendelea saana kwa sababu ya uwepo wa wachina/na wa hindi lakini leo hii wenyewe wanatahayuri uchumi/uwepo wa watu wa asili ya nje ya malasyia/singapore.
tuje hapa zanzibar na bara wao wenyewe wanasema bila kuwepo kwa taratibu, ipo siku zanzibar itakuwa zanzibara, hivyo wangependa kuona kunakuwepo kwa utaratibu kidogo wa ku-control hii hali.
kwanza unajua kwamba kuna nchi moja ya bara la asia ambalo sisi mpingo wanatuona kama ni manyani? wana kuchekea kwa sababu unabidi, ikiwezekana wangependa kukuona u don't exist.
ukienda kwa nchi za wenzetu kama sweden , etc wataangalia huluka yako hadi miaka 5 ili kuweza kusema wewe angalau unafaa faa kuwa mwenzetu yaani kama huna criminal record, enzi zile wa tanzania walivyo vamia sweden, hiyo ilikuwa ni mojawapo ya vigezo vya ku-fit in
August,
Jamal alifia Canada kwa sababu ndiko anakoishi binti yake. Alikuwa ameachana na mkewe na alipougua binti yake akamchukua kumtunza.
Serikali ya Mwinyi ilisita kupeleka fedha arudishwe nyumbani na binti yake did the needful. Huwezi kuwafananisha hata siku moja haya matapeli ya sasa kina RA na Amir Jamal. He served the country well.
 
Ni kujuzana tu ndugu yangu...unajua mchangiaji alitoka nje ya hoja kidogo....unapomuita mtu tapeli shurti uwe na ushahidi na mojawapo ni kuwa kafikishwa mahakamani

Mkuu wewe ndiye uliyeleta hoja hapa ya kumpamba Tapeli, ninachosema ninakisimamia na ushahidi upo wazi kwa watu wengi tu, usifikiri kama wengi hawajibu na kukaa kimya basi jamaa sio tapeli. Nadharia yako ya kifikishwa mahakamani ni muflisi. Ushahidi huwa hauletwi kwa madai kwenye hili jukwaa bali kwa subira na kuweza kumeza umangimeza wote ambao utajitokeza. Natumaini Ulimwengu mwenyewe yupo humu sio siri na yeye anafahamu utapeli wake.

Ni makosa makubwa kulinganisha wageni jinsi wanavyokumbatiwa katika nchi za magharibi na kufikiria huwa ni mteremko jinsi wengi wanavyofikiria kwenye hili jukwaa. Loopholes na njia za mkato kwa wenzetu hazipo.
 
Haya maswala ya uraia Tanzania Yanatokana na roho za kimaskini... Na siku zote mimi napinga maneno ya watu wanaosema ati maskini ni wastaarabu na wenye huruma sana kwa sababu hawana nguvu ya fedha. Lakini ukweli ni kwamba ukitaka kuwapima, weka sinia la ubwabwa utawaona wanavyotiana makucha ya macho na hata kutoana roho kwa sababu ya pande moja la nyama. Na mara zote huwa hakuna atakaye shiba kati yao isipokuwa kujiongezea maradhi kwani katikati hupindua sinia na wali wote huishia mchangani..

Hizi sheria zetu za kuwaita wazawa sio Watanzania hadi wazazi wao hasa baba awe Mtanzania inatokana na mila inayokumbatia Ukabila zaidi ya Uraia..Ni vichekesho sana kuona ati baba Mtanzania aliyekwenda kusoma Urusi na kuzaa mtoto ambaye hajawahi fika Tanzania anapata uraia wa baba kuliko Mtoto aliyezaliwa Tanzania na kukulia Tanzania kwa sababu tu baba yake sio Mtanzania. Kwa maana hii wapo watoto nje waliozaliwa wana haki ya Utanzania ingawa hawajawahi kukanyaga nchini kuliko watoto waliozaliwa nchini na wanaishi nchini kwa vibali.

Kama kweli sheria yetu ndio inasema hivi basi tumechemsha sana kwa sababu Tanzania ina mchanganyiko wa makabila sijapata kuona na kama tukianza kuwachambua kila mmoja wetu nina hakika tutafukuza wengi sana. Na hata madai ya kwamba wale wote waliokuwepo nchini kabla ya Uhuru wamepata uraia moja kwa moja ni uongo tu kwa sababu wakoloni wengi tu walikuwepo nchini (wawekezaji) wakati wa Uhuru wetu na bado waliondoka ama kuondolewa wakihesabiwa kama ni raia wa nje. Hivyo historia ya Utanzania haina kipimo isipokuwa kwa jinsi viongozi walioko madarakani wanavyojisikia.

Toka mwaka juzi rais JK akitembelea nchi za nje, aliwaomba kwa msisitizo Watanzania warudi nyumbani kuwekeza...Ebu nirudie tena WATANZANIA warudi NYUMBANI kuwekeza... hii inaingia akilini kweli.

Haya maajabu ya Mussa Watanzania hao hao wakiingia nchini hupewa visa ya miezi MITATU tu kukaa nchini hata kama wamekuja kuwekeza laa sivyo wachukue kibali cha kuhamia kwa gharama isiyopungua dollar za Kimarekani 1,600. Na hata kama wamekuja wekeza kwa mtaji unazidi kiwango cha dollar 300,000 bado watu hao walishindwa kukamilisha taratibu za usajili ktk miezi hiyo mitatu hivyo kuwalazimu kutoka nje ya nchi na kuomba visa tena. Ni adhabu kubwa kuwekeza Tanzania kwani hakuna matayarisho ya aina yoyote ile kwa wawekezaji kama huna rangi na lafidhi ya mkoloni mtawala wetu.

Sasa wakati nchi yetu inahitaji vijana wenye uwezo mkubwa ktk maswala yote ya ujenzi wa nchi yetu na hakika badala ya serikali kutumia mabillioni kwenda kuwasomesha nje hawa vijana wamechukua jukumu lao wenyewe na familia zao kutafuta elimu nje, leo wanaitwa ni WAKIMBIZI.. ati wameikimbia nchi hali vijana hao wasingeweza kupata elimu hiyo pasipo kuchukua hatua walizochukua. Na kibaya zaidi leo tunaambiwa ati kina Rostam ndio Watanzania kuliko hawa vijana waliokwenda nje kutafuta elimu na kadhalika.

Kwa sababu ya mfumo huu mbovu vijana wengi wameingia shule feki ili kupata elimu haraka na kurudi nyumbani ili mradi wasipoteze Uraia wao. Ni vigumu sana kwa kijana Mtanzania kuweza kujisomesha UK, US au Canada akiwa raia wa nje kwa muda wa miaka mitano au zaidi... Ni karibu na haiwezekani ama ndio kujiunga na vyuo vya mitaani na kupata cheti kisichojulikana kimataifa.

Na kwa bahati mbaya wale walioweza kusoma kweli hawana sababu ya kurudi nchini ikiwa kweli wanakuwa treated kama foreigners hali baba zao ni Tanzania Citizen. sasa ebu nyie nambieni huyo Bashe sio Mtanzania kwa sababu baba yake hakuwahi kuukana Usomali, iweje Mzawa mwingine anayeishi nchi za nje asiwe raia wa Tanzania ikiwa baba yake hakuwahi kuukana Utanzania!

Jamani nachoweza kusema tu ni kwamba kwa kila mtu aliyefikisha umri zaidi ya miaka 18 huyu ni mtu mzima na ana uweo wa kuchagua Uraia kwa utashii wake ikiwa ktk nafasi tata kama ya Bashe. Iwe hata hatukubali Uraia wa nchi mbili lakini tuwe na maamuzi ya kisheria yanayochuja rabsha kama hizi za kutazama Upande mmoja tu wa sheria kama kisu butu..

Mkuu hapa umeongea mambo meengi sana mazuri na ndio hali halisi.

Lakini ntajaribu kusaidia kimawazo katika eneo moja la vyuo ambavyo umeita ni feki.

Kwa mfano UK kuna vyuo lukuki ambavyo vinafundisha masomo mbalimbali katika ngazi ya diploma na advanced diploma kwenye maeneo ya Computing, Hotel Management, Accounts na mengine.

Sasa ukimaliza Advanced diploma siku hizi, kuna option ya kuingia second year au kumalizia third year katika vyuo vikuu mbali mbali nchini na mwisho kutunukiwa degree yako kulingana na pass ulizo nazo katika diploma na advanced diploma zako na ikiwa si za kuridhisha basi utaambiwa ni lazima uanze mwaka wa kwanza wa University na ndio wengi huishia hapo kwenye Advanced diploma kwani uwezo wa kulipa £15,000 kwa mwaka unakuwa ni ndoto.

Kwa mfano umesoma mpaka level ya Advance Diploma kwenye computing ya IMS (Institute for Management of Information Systems) au ABE AU NCC unaweza kukubaliwa kuijunga na university yoyote ile kulingana na pass zako na ukaingia kusomea degree na mwisho ukapewa degreee yako na kuwa graduate.

Mfano mwingine ni kwenye accounts, labda umesomea diploma hadi advanced diploma na kufanya mitihani ya bodi mojawapo kati ya ICM, CIMA au ACCA, unaweza kukubaliwa kuingia university provide umefaulu vizuri katika kila ngazi ya vyeti hivyo.

Hii yote ni kwa sababu miaka miwili ya diploma na advance diploma inalinganishwa na miaka miwili ya university na suala la pass nzuri za candidate zinaangaliwa kwa makini na university husika.

Mkuu Mkandara, kwenye miaka ya mwisho ya tisini kulikuwa na vyuo feki vingi sana ambavyo vilikuwa vikishiriki kuwaalika wanafunzi ughaibuni hasa UK na nakumbuka kuna chuo maarufu kilichokuwa kikiitwa South Chelsea kule kusini mwa jiji la London ambacho kuna watanzania wengi wamepitia hapo na kutapeliwa na baadae kuangalia utaratibu mwingine wa kuhangakia maisha.

Mtindo ulikuwa ni kufanya application kama kawaida na mtu akiishatia mguu huku ughibuni basi inakuwa ni akili kichwani. Sasa iwe mtu ametumia njia ipi hio yote ni maisha na kama umefanikiwa basi unashukuru Mungu na kama hujafanikiwa basi unabaki kuhangaika na kuongoja saa ya ukombozi.

Kwa sasa hakuna vyuo feki na vingi vinadhibitiwa kwa mtindo wa kuorodheshwa katika database ya wizara ya mambo ya ndani ya UK au USA na kama ukitaka kwenda kusoma katika vyuo hivyo ni lazima viwe ndani ya database hiyo. Pia ukitaka kuhama chuo inabidi uvifahamishe vyombo vinavyohusika ili ieleweke kwamba wewe unahama.

Sasa linakuja suala kwa mfano nchini UK mtu amefanikiwa kumaliza degree yake bado ana uwezo wa kuomba kufanya kazi ili apate work experience na anaruhusiwa kufanya kazi hiyo kwa mwaka mmoja na ikiwa utakuwa mzuri mahali hapo basi mwajiri wako atakuombea kibali kingine ambacho kitakuwa initially miaka miwili na baadae miaka mitatu ambayo inafanya mtu awe amekaa miaka mitano ndani ya kazi yake hiyo.

Hivyo dhana ya kwamba Ughaibuni kuna vyuo feki si imara sana kuzingatia kwamba hata watu wenye fwedha iwe za CCM na serikali au za madili wanaweza kuwaleta watoto wao wakasoma na kulipiwa £15,000 kwa mwaka na wakawa na uhakika wa kurudi Tanzania na kupata ajira katika vyombo mbalimbali vyenye majina. Ipo mifano mingi ambayo sina haja ya kueleza ya watoto wengui walosoma Ughaibuni na kurudi nyumabi kwani wanajulikana.
 
Niambie nani anaishi legally marekani, UK ,Canada bila ya proper documents!! ukijulikana huna wanakung'oa 24. Sisi tumewapa Warundi uraia 160,000 niambie ni taifa gani lingine limefanya hivyo. Hawa Warundi wamefuata taratibu baada ya kukaa kama wakimbizi.
Rais Mkapa aliwahi kwenda nchi moja ulaya, kwanza aliambiwa nchi hiyo ina watanzania zaidi ya 300. Katika mkuatano na raia hao walikuja 20 tu, wengine wote walikuwa wasomali waliobeba passport za Tz.
Tusipokuwa na system inayochuja hawa wahamiaji haramu siku moja ita kuwa hivi, Mkuu wa majeshi ni jenerali Ndikumana Basogilile Habiryamana, waziri wa ulinzi ni Mutua maina wainana, Mkuu wa polisi ni Ssemogerere Kironde, spika ni Mr Patel Somjii. Wote hawa likizo wanarudi makwao!!! tupo salama hapo.?
Lakini huwa nauiliza swali moja, Ni mtanzania au mwafrika gani yumo ndani ya bunge la India. Ni mtanzania gani ameomba na kupewa urai wa India au Saudi Arabia?? Muulizemni Balloteli nini kinampata Italia. Hivi unaweza kuwa mbunge wa Somalia na ukabaki salama! Unaweza kuwa mbunge wa Burundi bila kuwa mtutsi au Mhutu? Tena nimekumbuka, kuna Sheikh mmoja alikuwa maarufu sana Dar kwa miaka mingi akiwa na NGO yake, huyu alikuwa anasafiiri na passport za Tanzania, hivi leo ni senator wa bunge la burundi!!!!!!!
Mimi ninachoweza kukubaliana na wengi ni kuwa mamlaka inayotoa au kukataa uraia ni Uhamiaji na si CCM, laikini msismamo wangu unabaki pale pale lazima tuwe na raia waliofuata utaratibu wa nchi yetu!

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Ningependa kujibu Maswali kadhaa uliyoyauliza..

Yes kuna wananchi wasio na majina sawa/ya kufana na majority lakini wamo bungeni au ni maraisi pia...President of the USA"Baraka HUssein Onyango Obama" Upo hapo, kwa nini ..kwa sababu kazaliwa USA na mama ambae ni raia wa USA na baba ambaye ni Mkenya..90% of the US congress is Jewish descendants of Eastern European Immigrants..

Mhamiaji ni mhamiaji mpaka apewe uraia anakuwa na haki sawa na wewe hata kam anaitwa Mashuzi ya Mototo you get ie?
Wasomali walioenda UK and Other western countries like US and Canada hawajaenda wakakaa kitako kwamba wamefika, ila wanafight every single day? kama unataka kujua leo hii the 1st Black/Muslim Congressman ameingia congress because of Somali people in Minessota..Ayan Hirsi in Holand went on becoming a Minister..Listen Hata kama haupendi watu wasiofanana na wewe au wasio na rangi kama yako, nakuone huruma kwa sababu watu wanazaliwa Tanzania na wanadai haki kama kila Mtanzania na mkiwanyima haki zao wana simama kupigania haki zao..
Kitu kimoja ambacho nina uhakika nao..Bashe kazaliwa Tanzania amefanyiwa tuhuma na kusabishwa kukosa kiti cha Nzega kwa uonevo..Kama yeye ana genes of Somali origin I know for sure he will fight for his rights, Intellectually, kiakili..Ofcourse in Somalia leo watu waliomfanyia uhasidi they would have met different circumstancces I for sureknow that they wouldnt be standing today in Lumumba"if you know what i mean".

Na huyo Sheikh alienda Burundi kaenda huko kwa sababu nyie watanzania mna ajenda za kuwafukuza watu wenye different agenda than yours because they argue /kubishana na mke wako au Ridhwani kikwete. Kwa hiyo mwache huyo sheikh atumikie watu wanaomthamini...Lakin Hussein Bashe amewaganda na anapenda nchi yake atafight, miaka mitano ni muda mfupi..Nitakuwa nimekaa mlimani nafundisha na nikimuona Hussein Wazairi naah RAISI...
Cheers
 
Ntakusaidia, kwani mimi nilisoma nae darasa moja Form V na VI pale Tabora School (1967-68). Jina lake hasa ni Twaha Khalfani lakini alipenda kuitwa 'General' Khalfan (Note: 'General' a siyo ('Jenerali'). Nakumbuka wakati tunajaza fomu za kufanya mitihanbi ya A level tuliruhusiwa kubadili majina yetu tuliyokuwa tunatumia (tukitaka) kwa hivyo yeye aliandikisha General T. K. Ulimwengu.

Kubadilisha kutoka 'General' kwenda 'Jenerali' alifanya baadaye kwani bila shaka 'General' did not sound right and appeared too outlandish.
Enzi hizoooo,siku hizi tunaitana nyumbu..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom