Hats off to Jenerali Twaha Omar Ulimwengu

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,268
17,097
Wakuu,
Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa makala za 'Rai ya Jenerali' toka zilipoanza nadhani 1994(Gazeti la Rai wakati huo)...zinanivutia lakini hizi za toleo lililopita(Na.146 Raia Mwema) na wiki hii (Na.147 Raia Mwema)...zimenigusa sana hasa hii ya leo....huyu bwana alikaa kimya sana kuhusu sakata lake la uraia lililoibuliwa na serekali ya Mkapa....lakini leo kwa upeo wa hali ya juu na kwa utaalamu mkubwa wa kiuandishi amenifanya nimuelewe vizuri sana....nimeshindwa kuiweka makala hii hapa....lakini amemmaliza Chiligati kwa hoja ya kumhusisha yeye Jenerali na suala la Bashe.....laiti waandishi wetu wengine wangeandika kama huyu bwana basi mabanzi ya mbao katika macho yetu,kutu katika bongo zetu na nta katika masikio yetu vingetokomea kabisa.

Thank you Jenerali if you are in the forum!!!
 
Nami nimemsoma Jenerali. Lakini angetutendea haki zaidi kama angeeleza alilimalizaje sakata lile. Pengine ingekuwa msaada mkubwa kwa wengine ambao naamini wako wengi wanaokumbana dhahma kama hii. Kuwashambulia Kitine na Mkapa ambao tayari ni "spent forces" hakujatusaidia sana mashabiki na wasomaji wake. Baadhi yetu tulikuwa tunajua waliomwandama.
 
Hivi Jenerali naye alituhumiwa kuwa raia wa nchi gani?
RWANDA ya KAGAME. Mimi naishangaa Tanzania yetu. Nchi kama Marekani ina raia wa nchi zote duniani na imeendelea kwelikweli tena kwa kuzitumia mbongo na vipaji vya raia hawa "wakuja"!
 
Nami nimemsoma Jenerali. Lakini angetutendea haki zaidi kama angeeleza alilimalizaje sakata lile. Pengine ingekuwa msaada mkubwa kwa wengine ambao naamini wako wengi wanaokumbana dhahma kama hii. Kuwashambulia Kitine na Mkapa ambao tayari ni "spent forces" hakujatusaidia sana mashabiki na wasomaji wake. Baadhi yetu tulikuwa tunajua waliomwandama.

Muulize privately (nadhani atapenda hivyo)....... jenerali@gmail.com
 
Wakuu,
Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa makala za 'Rai ya Jenerali' toka zilipoanza nadhani 1994(Gazeti la Rai wakati huo)...zinanivutia lakini hizi za toleo lililopita(Na.146 Raia Mwema) na wiki hii (Na.147 Raia Mwema)...zimenigusa sana hasa hii ya leo....huyu bwana alikaa kimya sana kuhusu sakata lake la uraia lililoibuliwa na serekali ya Mkapa....lakini leo kwa upeo wa hali ya juu na kwa utaalamu mkubwa wa kiuandishi amenifanya nimuelewe vizuri sana....nimeshindwa kuiweka makala hii hapa....lakini amemmaliza Chiligati kwa hoja ya kumhusisha yeye Jenerali na suala la Bashe.....laiti waandishi wetu wengine wangeandika kama huyu bwana basi mabanzi ya mbao katika macho yetu,kutu katika bongo zetu na nta katika masikio yetu vingetokomea kabisa.

Thank you Jenerali if you are in the forum!!!

binafsi namkubali kama mmoja wa wandishi sugu katika nchi hii.... utakuwa umanisaidi mimi na wanajamii humu kama utafanikiwa kuiweka makala hii humu ndani!!
 
Kimsingi ukiwa focused sana na mambo yanayowafaidisha wakubwa watakutafutia jiwe la kuhangaika nalo kama wanavyomfanya Mtikila. Kama mkapa angeshupaliwa kwamba ni wa Nchumbichi, Nyerere kuwa mtusi na watu wote wa mipakani wakasogezewa nje ya nchi, ni mgogo tu ambaye angebakia kuwa mtanzania halisi kwa kuwa majirani zao wote ni ndani kwa ndani.

Hata Komba n Mzulu! Wabantu wote waende kwao Matebeleland. Mwisho wa siku Tanzania haina wenye nchi, wote ni wahamiaji tu. Kudadadeki. Sasa ndio maana by streets definition ni mchezo mchafu.
 
Siri ya Tanzania kuwa na makabila 120+ ni kutokana na biashara ya utumwa zaidi.Njia kuu za kupitishia watumwa kwa upande huu wa Afrika ziliishia Tanzania (Kilwa,Bagamoyo,Pangani na Zanzibar) kwa hiyo makabila mengi sana yalitoka nje ya mipaka yetu ya sasa na kuja ku settle hapa.Ila nadhani ingekuwa haki kuwa watu wote waliokuwepo wakati wa uhuru(1961) na Muungano(1964) pamoja na uzao wao uliofuta baadaye wawe automatically ni raia na sio kundi la watu wachache wenye nguvu za mamlaka kuamaua nani ni Raia,based on muonekano wa sura yake.Binafsi nilipata shida sana kupata passport kutokana na muonekani wangu kwa sura ambao sijui hata ulikotokea.Jamaa wa Immigration walinipa taabu sana kupata hiyo pasi,ati siyo Raia nami nikawaambia basi nirudisheni huko mnakodhani mimi ndio kwetu.
 
okey Jenerali anabakia kuwa kielelezo cha uandishi wakichunguzi, wakikachero, uandishi wenye kalamu kali, ambayo haiogopi mshindo nyuma, kwake ukweli usimama.
 
.
Ahsante kwa kazi nzuri, ila tunaomba ututumbukizie toleo NO 147

Ntakusaidia, kwani mimi nilisoma nae darasa moja Form V na VI pale Tabora School (1967-68). Jina lake hasa ni Twaha Khalfani lakini alipenda kuitwa 'General' Khalfan (Note: 'General' a siyo ('Jenerali'). Nakumbuka wakati tunajaza fomu za kufanya mitihanbi ya A level tuliruhusiwa kubadili majina yetu tuliyokuwa tunatumia (tukitaka) kwa hivyo yeye aliandikisha General T. K. Ulimwengu.

Kubadilisha kutoka 'General' kwenda 'Jenerali' alifanya baadaye kwani bila shaka 'General' did not sound right and appeared too outlandish.
 
.
Ahsante kwa kazi nzuri, ila tunaomba ututumbukizie toleo NO 147

Raia Mwema toleo jipya kwenye mtandao huwa linawekwa siku moja baada ya nakala chapishi kutoka Tanzania. Kwa hiyo mkuu mimi na wewe tusubiri tu kesho ndio tulisome mtandaoni.
 
Siri ya Tanzania kuwa na makabila 120+ ni kutokana na biashara ya utumwa zaidi.Njia kuu za kupitishia watumwa kwa upande huu wa Afrika ziliishia Tanzania (Kilwa,Bagamoyo,Pangani na Zanzibar) kwa hiyo makabila mengi sana yalitoka nje ya mipaka yetu ya sasa na kuja ku settle hapa.Ila nadhani ingekuwa haki kuwa watu wote waliokuwepo wakati wa uhuru(1961) na Muungano(1964) pamoja na uzao wao uliofuta baadaye wawe automatically ni raia na sio kundi la watu wachache wenye nguvu za mamlaka kuamaua nani ni Raia,based on muonekano wa sura yake.Binafsi nilipata shida sana kupata passport kutokana na muonekani wangu kwa sura ambao sijui hata ulikotokea.Jamaa wa Immigration walinipa taabu sana kupata hiyo pasi,ati siyo Raia nami nikawaambia basi nirudisheni huko mnakodhani mimi ndio kwetu.

Nakuunga mkono kwenye hili suala la uraia. Inabidi tufikie mahala ambapo vigezo vya nani ni raia vinawekwa wazi kabisa. Ni jambo la hatari sana kuwaachia watawala waamue nani aitwe raia leo na nani ataitwa mgeni kesho. Ila nawaonea huruma sana CCM kwani kisu wanachokatia leo ndicho kitakachotumika kuwakata kesho wakishawekwa kando. Bahati mbaya hicho kisu kitakuwa kimenolewa zaidi ili kukiongezea makali. Natamani kuiona siku hiyo ambayo watawala wa leo watakuwa watu wakawaida, watawaliwa kama tulivyo sisi wengine!
 
Kimsingi ukiwa focused sana na mambo yanayowafaidisha wakubwa watakutafutia jiwe la kuhangaika nalo kama wanavyomfanya Mtikila. Kama mkapa angeshupaliwa kwamba ni wa Nchumbichi, Nyerere kuwa mtusi na watu wote wa mipakani wakasogezewa nje ya nchi, ni mgogo tu ambaye angebakia kuwa mtanzania halisi kwa kuwa majirani zao wote ni ndani kwa ndani.

Hata Komba n Mzulu! Wabantu wote waende kwao Matebeleland. Mwisho wa siku Tanzania haina wenye nchi, wote ni wahamiaji tu. Kudadadeki. Sasa ndio maana by streets definition ni mchezo mchafu.

kwa kweli mimi ilinishangaza sana enzi za mzee mkapa kusema jenerali si raia ilhali yeye mwenyewe inasemekana ni nchumbiji boy! pengine kuna jambo lilitokea mpaka jenerali akawa denounced. Jenerali should tell us nini kilitokea/au alifanya nini mpaka rafiki yake wa zamani (as they say) akamdenounce ili na mimi nijue maana inasemekana hata mimi babu wa babu wa babu yake na baba wa babu yangu alihamia hapa wakati hata haijaitwa Tanganyika au East africa Germany nisije nikanyanganywa uraia nikikwaruzana na wakulu au watoto wao.
 
Siri ya Tanzania kuwa na makabila 120+ ni kutokana na biashara ya utumwa zaidi.Njia kuu za kupitishia watumwa kwa upande huu wa Afrika ziliishia Tanzania (Kilwa,Bagamoyo,Pangani na Zanzibar) kwa hiyo makabila mengi sana yalitoka nje ya mipaka yetu ya sasa na kuja ku settle hapa.

Ila nadhani ingekuwa haki kuwa watu wote waliokuwepo wakati wa uhuru(1961) na Muungano(1964) pamoja na uzao wao uliofuta baadaye wawe automatically ni raia na sio kundi la watu wachache wenye nguvu za mamlaka kuamaua nani ni Raia,based on muonekano wa sura yake.

Binafsi nilipata shida sana kupata passport kutokana na muonekani wangu kwa sura ambao sijui hata ulikotokea.Jamaa wa Immigration walinipa taabu sana kupata hiyo pasi,ati siyo Raia nami nikawaambia basi nirudisheni huko mnakodhani mimi ndio kwetu.

Hapo kwenye red; hilo mbona ndilo lililotokea kwatai wa Uhuru wa Tanganyika na pia wakati Tanzania inaundwa!! Au mimi nimesoma kwa makengeza?
 
Wapendwa huwa sipendi kuweka nakala za gazeti hapa kwa sababu naona kama si kuwatendea hako wenye gazeti ila kwa hii nakala naona nivunje mwiko hapa hiyo para ya mwisho
 
Attachments

  • Nkaba Nyin.pdf
    581.2 KB · Views: 145
Back
Top Bottom