Hatma ya Warioba mikononi mwa JK

  1. Ni kwa nini vigogo wanaobanwa ni wale tu ambao wako mbali na Wanamtandao?
  2. Ukiangalia utaona kuwa wote wanakomaliwa, kesi zao ni nyepesi nyepesi ambazo sio ajabu serikali itashindwa, ndio maana yule mbunge akahoji ni kwa nini serikali inashindwa kwenye kesi zake nyingi?
  3. Kesi zenye ushahidi kibao kama za akina RA, Lowassa, Chenge n.k. hazipelekwi mahakamani, kwa nini utumiaji wa sheria uko selective?
Haya ni maigizo tu ya kuwaonyesha wahisani wanaochangia bajeti kuwa JK yuko serious na pia kuwakomoa wale wasiompigia magoti huyu mkuu na wala sio sheria msumeno.


Ahsante sana makaayamawe, Mtandao bado umeshika UTAMU ndani ya chama na serikali ndiyo maana hakuna hata mwanamtandao mmoja ambaye ameshafunguliwa kesi pamoja na kuwa kuna ushahidi wa kutosha dhidi ya wanamtandao mbali mbali. Angalia TICTS ya Karamagi, pamoja na Bunge kuidhinisha kuvunjwa kwa mkataba wa kampuni hiyo na Serikali lakini kuna USANII wa hali ya juu katika kutekeleza kilichoidhinishwwa na Bunge mpaka Mkullo kufikia kusema kwamba mwenye uwezo wa kuvunja mkataba huo ni Kikwete pekee. Sasa kama Bunge la Tanzania limeshaidhinisha kwamba mkataba huo uvunjwe Kikwete anangoja nini tena!?

Angalia ushahidi chungu nzima dhidi ya Rostam katika Kagoda na Richmond lakini hakuna wa kumgusa maana huyu ni mwanamtandao muhimu sana aliyefanikisha mengi ili kuhakikisha Kikwete anaibuka kama mgombea wa CCM. Na wanajua kumgusa huyu kunaweza kukawa ndiyo mwisho wa wanamtandao kama tunavyoujua kama ataaamua kuanika kila kitu kilichofanyika katika kampeni za Kikwete kuhakikisha kwamba anaibuka kama mgombea wa CCM katika uchaguzi ule wa 2005. Angalia hawa akina Subhash, Chavda, Manji, Jeetu kuna ushahidi chungu nzima dhidi yao kutokana na utajiri mkubwa waliojilimbikizia, lakini hakuna wa kugusa. Na mimi naamini kabisa kwamba kama Kikwete atapita 2010 hizi kesi za EPA zitafutwa kwa madai ya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha dhidi ya washtakiwa.

Kwa kifupi sasa hivi nchi yetu imejaa USANII wa hali ya juu kuanzia ngazi za juu za uongozi katika chama na serikali, vyombo vyetu vya dola ikiwemo polisi, mahakama, TAKUKURU na hata ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka. Let's wait and see how this Warioba's saga unfold
 
Back
Top Bottom