Hatma ya Meshack Opulukwa (mbunge wa Meatu) kujulikana Mei 4

MNYISANZU

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
7,048
1,102
Hatma ya mbunge wa jimbo la Meatu kupitia Chadema mh. Meshack Opulukwa itajulikana may 5 mwaka huu. Hii ni kufuatia kesi ya kupinga ushindi wake iliyofunguliwa mahakamani na aliyekuwa mgombea wa CCM bwana Salum. May 5 ndio siku rasmi ya jaji kutoa maamuzi.

Source: Radio Free Africa, kipindi cha matukio.
 
Hatma ya mbunge wa jimbo la Meatu kupitia Chadema mh. Meshack Opulukwa itajulikana may 5 mwaka huu. Hii ni kufuatia kesi ya kupinga ushindi wake iliyofunguliwa mahakamani na aliyekuwa mgombea wa CCM bwana Salum. May 5 ndio siku rasmi ya jaji kutoa maamuzi. Source: Radio Free Africa, kipindi cha matukio.
aliiba kura kwani?.
 
mgombea wa magamba Salum Mbuzi si ndiye aliyewanyanganya tractor wanakijiji na kutaka kuchukua madawati aliyonunua wakati akiwa mbunge
 
hivi hawa magamba wanahila gani na wapinzani! Naona hukumu zao zote kwa ss ni trh 2 na trh 5!! Kuna nini hapo jmn?! Hakika tumeanza na Mungu na tutamaliza na Mungu.
 
Kila kitu kina mwisho CCM imefika mwisho ndio maana inahangaika sana,
"Kuwa namba 1 kwa muda haishindikani ila kuwa namba 1 milele haiwezekani"
 
Yaani magamba vinganganizi karibu majimbo yote walioshindwa walifungua kesi, wakijua kwa kutumia udhaifu wa mahakama na rushwa wanaweza kushinda!! Arusha? ubungo?? ilemela?? singida mashariki??meatu?? duh!!!!
 
Huyu mpiganaji Opulukwa (wengine tumezoea kumuita OP) ni mpiganaji ninayemkubali sana. Mwaka 2005 alidhulumiwa yeye, lakini nashangaa sasa wanataka kumuengua kwa mizengwe tena. Nafikiri wanataka ku-frustrate wananchi ili wasiwachague wapinzani. Maana muda wao mwingi na resources hutumika mahakamani, na mara nyingine haki isitolewe. Huu ni upepo tu, utapita na zama mpya zitawadia.
 
Tuombe Mungu Haki ikatawale maamuzi ya Jaji. Na giza na Pesa zikashindwe.
 
Tundu Lissu hukumu 27/04/2012

Makongoro Mahanga hukumu 02/05/2012

Meshak Opulikwa hukumu 04/05/2012

Tusubiri matokeo. Hiyo ya Makongoro naskia tayari ameshamuonga Jaji Tsh35,000,000/=
 
mgombea wa magamba Salum Mbuzi si ndiye aliyewanyanganya tractor wanakijiji na kutaka kuchukua madawati aliyonunua wakati akiwa mbunge

Kuna mzee wa kisukuma nilishamsikia akimwambia mwenzake kuwa ''USIWE KAMA MKIA WA MBUZI...HAUSTIRI UCHI NA WALA HAUFUKUZI NZI''...

Sasa sijui alikuwa anamaanisha Mbuzi yupi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom