Hatma ya Makamba CCM kujulikana leo

Kikwete pia naye astaafu Urais maana tangu alipoingia madarakani 2005 hakuna cha maana chochote alichokifanya zaidi ya usanii na uVDG.
 
Kwa taarifa za awali leo mambo yote kuhusu makamba yangejulikana, mliopo jirani na tukio au wale wenye habari plz tupeni feedback!
 
makambapos.jpg


HATMA ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba inatarajiwa kujulikana kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho kinachoanza leo. Kikao hicho kinaanza asubuhi hii mjini hapa, huku kukiwa na taarifa kuwa sekretarieti yake huenda ikavunjwa. Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani ya CCM, zinadai kuwa uamuzi huo unachukuliwa ikiwa ni hatua ya chama hicho kujivua gamba linaloonekana kuchuja mbele ya umma.

Chanzo chetu cha habari kilidai kuwa, baada ya kuvunjwa sekretarieti, Makamba ambaye ndiye mwenyekiti wa sekretarieti hiyo, atawasilisha taarifa ya kuomba kustaafu. Hatua hiyo inamwezesha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuteua sekretarieti nyingine ambayo itakiongoza hadi mkutano mkuu unatarajiwa kufanyika mwakani.

Zaidi: Hatma ya Makamba CCM kujulikana leo
EMT, baada ya kutuhabarisha, ulitakiwa utu update. CC hajapanga ajenda za NEC, hivyo NEC haijakutana leo, itakutana kesho.
 
waulize CCM! kuna watu ni wanachama wa ccm wazuri, mnachachatuka na kuhemuka kuhusu makamba na hatma yake,wha for? halafu bila aibu unauliza wana JF vipi! makamba na hatima yake inanihusu nini mimi nisiye mwana CCM?
 
Back
Top Bottom