Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,190
Si Kikwete wala CCM waliowahi kuamini katika kuandikwa upya Katiba yetu. Hivyo wao kuzalisha Tume ya Katiba IKULU badala ya BUNGENI tayari ni safari ya maafa kwa taifa letu kama washikadau wote wa katiba hawatahusika na kila hatua tangu mwanzo.
Watanzania, tukidanganyika katika ahadi za ajabu ajabu kukumbatia wachafu na mipango yao kuuteka nyara nia njema ya raia wa Tanzania kujiandikia katiba wapendavyo,
Na kwamba huku tukijua fika kuwa watu hao ni wachafu kwa mienendo yao tangu kwenye uchakachuaji wa uchaguzi mkuu wetu na ufugaji mzuri wa ufisadi nchini,
Na kwamba wachafu hao baadaye kwa ghiliba zao wakaja wakaambukiza huo huo uchafu wao kwenye kutuchafulia na kutia masizi ya kifisadi nia yetu njema ya kujiandikia katiba mpya baada ya zaidi ya miaka 50 nchini,
Na baada kwa uchafu wao huo au ghiliba tukaishia ama na mchezo mchafu au katiba mpya chafu, basi moja kwa moja kila mmoja wetu ajiandae kuhukumiwa vibaya mno na historia ya taifa hili.
Maggid, Mwanakijiji na wengine wengi wenye uwezo wa kuona haya lakini mkaamua kuyafumbia macho, zingatieni haya ninayoyasema hapa kwa leo na kesho.
Siwezi nikawa shetani jana na kuwaibieni haki yenu ya kuchagua hapo 2010 halafu mwaka unapogeuka 2011 na mimi sasa nikageuka malaika wa kuwapiganieni walalahoi HAKI ya kupata katiba mpya niliyoshindwa miaka kuamini miaka yote kukubali kubadiliswa.
Hoja yangu ni kwamba Kikwete kama mwenyekiti wa taifa wa chama cha siasa tayari ni INTERESTED PARTY ambaye hawezi akaaminiwa na kujikabidhi hata sehemu moja ya hatua mbalimbali za kupatikana kwa katiba mpya.
Laa sivyo, tujaribu kupanda basi hili HATARI na hapo baadaye kidogo wananchi waje wagundue WAMECHEZEWA SHERE na kikundi fulani kuibuka na kusema 'CCM, Ushindi ni LAZIMA' baada ya ghiliba nzima, dalili zote zinaonyesha kwamba kutakua HAPATOSHI tukiingia uchaguzi 2015 bila katiba mpya iliozaliwa kwa ushirikishwaji wa wananchi wote kwa kila hatua tangu mwanzo!!!