Hatma nyumba za serikali yapata kigugumizi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Hatma nyumba za serikali yapata kigugumizi

2008-09-14 11:12:02
Na Restuta James

Ikiwa imebaikia siku moja tu serikali itwae nyumba zake ilizoziuza kwa maofisa wake wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, utata umeibuka juu ya utekelezaji wa azma hiyo kutokana Wizara ya Miundombinu kutupiana mpira kuhusu sakata hilo.

Hadi jana, Nipashe ilipowasiliana na viongozi wa Wizara ya Miundombinu kujua kama watumishi waliotakiwa kurudisha nyumba hizo, wamefanya hivyo, haikupata jibu.


Wizara hiyo mwishoni mwa mwezi Agosti ililiambia Bunge kwamba hadi Septemba 15 (kesho), watumishi walionunua nyumba zaidi ya moja wanapaswa kuzirejesha vinginevyo watapelekwa mahakamani.

Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, alitoa taarifa hiyo wakati alipoisoma bungeni kuhusu utekelezaji wa Azimio la Bunge la uuzaji wa nyumba za serikali.

Katika taarifa hiyo, Dk. Kawambwa alisema watumishi wanne waliouziwa nyumba zaidi ya moja, wanatakiwa kurejesha nyumba ya ziada na kubakiwa na moja kama utaratibu ulivyo.


Watumishi hao pamoja na sehemu zao za kazi kwenye mabano ni Dk. Edna Moses (Wizara ya Afya), nyumba Na. 1288129 mtaa wa Chang`ombe (Dar es Salaam) thamani ya nyumba ni milioni 18, Veronica Mabula (Bohari Kuu), nyumba Na. G3, mtaa wa Mabatini (Mwanza), thamani ya nyumba ni Sh.749,000, Sweetbert Bajuza (Afisa Tawala wa Wilaya), nyumba Na. 5&6, mtaa wa Bomani (Karagwe), thamani ya nyumba Sh. milioni 1.6 na Agnes Chamshana, nyumba Na. 3681,B2,B3, Bomani Area, Wilaya ya Lushoto, thamani ya nyumba Shilingi milioni mbili.

Hata hivyo Dk. Kawambwa, alipohojiwa na gazeti hili kuhusu utekelezaji wa azma hiyo ya serikali alisema \"Nipo jimboni kwangu wiki ya pili sasa, naomba uzungumze na msemaji wa wizara atakueleza mchakato mzima ulipofikia.

Alipohojiwa, msemaji wa Wizara hiyo, Martin Ntemo, alisema jambo hilo linashughulikiwa na maofisa wakubwa wa wizara.
``Sijui utaliandikaje ila hadi sasa majibu ya uhakika hayajapatikana...wakubwa wanaoshughulikia jambo hili hawako tayari kusema,`` alisema.

Alisema ``Bado linafanyiwa kazi...nahofia kukupa takwimu ya watu wanaodaiwa na kiasi cha fedha ili tusitofautiane na takwimu zilizopo kwa maofisa wengine, tafadhali elewa hivyo nilivyokueleza,``


Dk. Kawambwa aliposoma taarifa ya serikali kuhusu uuzaji wa nyumba za serikali alisema tayari nyumba za baadhi ya mabalozi, jaji na mawaziri ambazo ziliuzwa kinyume cha taratibu zimetwaliwa.

Hata hivyo alisema bado kuna nyumba 52 zilizouzwa kimakosa ambapo 34 kati yake zipo katika maeneo ya hospitali, 10 makambi ya magereza na nane polisi.

SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom