Hatimaye ZEC yatoa ushahidi jinsi uchaguzi ulivyoharibiwa kwa hujuma

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg


Baada ya maneno ya muda mrefu na shutuma kwenda kwa tume kuwa "imeufuta" uchaguzi bila kufuata taratibu,hatimaye Tume imekuja na ushahidi wa nyaraka za form namba MUR.12A zinazoonyesha jinsi hujuma ilivyofanywa kuuvuruga uchaguzi na hivyo kupelekea uchaguzi kuwa "batili" na hatimaye kuipa ZEC mamlaka ya kisheria ya kuufutilia mbali uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa ZEC ndugu Jecha S Jecha aliuthibitishia umma kuwa uchaguzi wa mwaka 2015 uligubikwa na ukiukwaji mkubwa wa kanuni, taratibu na sheria za uchaguzi na hivyo kuufanya kuwa batili.

Ubatili wa uchaguzi huo unaopaswa kurudiwa 20/03/2016 umezidi kuanikwa kwa ushahidi wa nyaraka za form za uchaguzi. Kwa mfano katika kituo cha Skuli ya Mabaoni [HASHTAG]#23801[/HASHTAG] Jimbo la Chonga namba 2909 form ya matokeo ya uchaguzi haina muhuli wa tume, hii ni sababu ya kufanya matokeo haya kuwa batili na haramu.Pia katika kituo cha Gamba [HASHTAG]#2008[/HASHTAG] form ya matokeo ya uchaguzi imefutwa futwa kwa juu na hivyo kusababisha majina na tarakimu kutoonekana kwa uzuri, hali hii pia inaleta ubatili na uharamu wa matokeo na hatimaye kutia doa uchaguzi wenyewe.

Katika kituo cha Mwembe Makumbi [HASHTAG]#21618[/HASHTAG] Jimbo la Chumbuni form ya matokeo imefutwafutwa na kupandikiza majina ya mawakala wengine ambao hawakuwepo wala kuhudhuria ktk eneo(kituo) cha uchaguzi, hii ni sbb nyingine ambayo inaipa ZEC nguvu za kubatilisha uchaguzi huu na kuamuru urudiwe 20/03/'16.

Kiwanja cha Mpira Masumbani katika Jimbo la Chumbuni,kituo hicho matokeo yake ni batili sababu yameandikwa tena kwa kalamu juu ya maandishi ya kivuli na saini imewekwa zaidi ya mara moja, katika Jimbo la Chake Chake Pemba, form katika kituo cha kupigia kura jina la kituo halionekani na namba haisomeki na form imepigwa muhuli wa Serikali ya Mapinduzi ya Z'bar badala ya muhuli wa ZEC.Eneo kubwa katika vituo vya uchaguzi kisiwa cha Pemba,mihuli na majina mengi yameghushiwa kama yanavyoonekana katika form hizi zilizoambatanishwa.

Kwa sababu hizo,na nyinginezo nyingi kama za wajumbe wa tume kupigana,uchaguzi huu ulikuwa batili na wala ZEC isingeweza kutangaza matokeo sababu kungezuka vurugu zisizokuwa na maana.

Hivyo kwa ushahidi huu wa nyaraka za form za uchaguzi Z'bar kuwa na mapungufu, Tume ya uchaguzi Zanzibar iliona hujuma hii na kuamuru uchaguzi huo kurudiwa.
 
zanzibar kulikuwa na vituo zaidi 1500 vya uchaguzi kwahiyo vituo hivyo saba haviwezi kusababisha uchaguzi mzima kurudiwa na hata kama ingekuwa vituo 100 pia isingesababisha uchaguzi mzima kufutwa ila sheria ya uchaguzi ya mwaka 1984 inasema wazi endapo uchaguzi utaaribika au kutofanyika kwa ajili ya hali ya hewa au chochote kile basi uchaguzi wa kituo usika utaairishwa na sio kurudiwa mpaka siku ya pili yake, Jecha amefuta matokeo pekee yake kwa kuwa anajua wazi kuwa endapo malalamiko hayo yangefikishwa kwy kikao cha zec hasingekuwa na uwezo wa kuwashawishi wajumbe kufuta uchaguzi. ushaidi huu ilibidi autoe kwa zec wenzake kwanza kabla ya kuhukumu huwezikuwahukumu watu kwanza halafu unaleta ushahidi baadaye.
 
Kama hayo ni kweli nani wa kulalamika na wapi hayo yanawezwa kupingwa <je ZEc inayomamlaka ya kulalamika au wagombea ndio walipaswa kuzuka na malalamiko ni wapi walipigana wajumbe wa tume na kwa nini matokeo yalikwisha kamilika kila kona na kufikia wagombea kupewa fomu za ushindi na masuali mengi tu ambayo Jecga kama akiwekwa kiti moto hawezi kuyajibu ,tuondoleeni upumbavu wenu hayo makaratasi yaliyopitwa na muda hayakubaliki. Wala hayahalalishi utangazaji wa marudio ya uchaguzi pia hayahalalishi kuufuta uchaguzi mzima,michoro hio Jecha akmuoneshe mungu wake anaemruhusu kusema uongo na kuibatilisha haki.
 
walikuwa wapi muda wote? ni vituo vingapi makosa kama haya ualitokea? kura za rais jpm na lowasa ziko sawa ila mawakala hao hao ndio hawana mihuri, wamekosea majina yao etc. huu ni ujinga tunaopashwa kuutoa mioyoni mwetu
 
Hivi wazanzbar hawakumpigia Kura JPM?? Au JPM alipigiwa Kura ktk vituo maalumu mbali na hivyo vilivyosababisha uchaguzi ukawa feki???
Chaguzi mbili tofauti zilizofanyika wakati mmoja na sehemu moja, vitendea kazi tofauti!
 
Back
Top Bottom