Hatimaye Wazungu wa ATM wapata dhamana

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
Mashine ya ATM.

Hatimaye wazungu wawili ambao ni raia wa Bulgaria wanaoshtakiwa kwa madai ya kuhusika katika wizi kwa kutumia mashine za ATM, wamepata dhamana.

Watuhumiwa hao, Nedco Stancher, 35 na Stella Nedilcheva, 23, wamepewa dhamana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Waliarwande Lema baada ya kutimiza masharti yote ya dhamana.

Wakipewa dhamana hiyo leo asubuhi, watuhumiwa hao wametakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao wamesaini hati ya dhamana ya shilingi milioni 21 na kuwasilisha hati zao za kusafiria.

Pia Wazungu hao wametakiwa kutotoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kuwa na kibali cha mahakama.

Upande wa Mashtaka wa kesi hiyo ambao unaongozwa na Wakili wa Serikali Beatrice Mpangala, umekubaliana na watuhumiwa hao kupewa dhamana na kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena mahakamani hapo Oktoba 27, mwaka huu.

Katika mashitaka yao, watuhumiwa hao raia Bulgaria wanadaiwa kushirikiana na wenzao ambao hawakuwepo mahakamani hapo, kula njama ya kutenda kosa; kitendo ambacho kinadaiwa kufanyika Julai mwaka huu, siku na sehemu isiyofahamika katika jiji la Dar es Salaam.

Shtaka lingine linalowakabili watuhumiwa ni la kughushi kadi za benki za visa, mali ya Barclays inayomilikiwa na Golga Sikolono wakijifanya kuwa ni za kwao.

Wazungu hao pia wanadaiwa kuwa kati ya Julai 10 na 11, mwaka huu walijipatia Sh milioni 14.5, mali ya benki hiyo kinyume cha sheria, huku wakijua kuwa ni kosa.

CHANZO: ALASIRI http://ippmedia.com/
 
Back
Top Bottom