Hatimaye Wabunge Wafanya Kweli: Mkapa & Karamagi Nje!

Mkuu heshima mbele, uzinzi wa Kubenea kama upo kweli hauna mahusiano yoyote na ishu za Rostam na kutufanyia ujanja taifa letu, kama ni ishu ya uzinzi sidhani kama kuna anayeweza kutupa jiwe kwa yoyote bongo, halafu besides hiyo ishu ina thread yake,

Kubenea is doing a lot kwa ajili ya taifa letu, na kuna tunaomheshimu na kumuombea maisha marefu na aendelee na kazi yake nzito ya kujitoa mhanga kwa taifa letu,

Ni Mungu peke yake anyeweza kumlipia!

mkuu siku zote nakukubali sana, naungana na watanzania wote kumsaidia kubenea kwa njia yoyote itayokua ndani ya uwezo wangu, otherwise Rosham Akibhai bora anyamaze kama kina Lowasa wanavyofanya
 
Mkuu heshima mbele, uzinzi wa Kubenea kama upo kweli hauna mahusiano yoyote na ishu za Rostam na kutufanyia ujanja taifa letu, kama ni ishu ya uzinzi sidhani kama kuna anayeweza kutupa jiwe kwa yoyote bongo, halafu besides hiyo ishu ina thread yake,

Kubenea is doing a lot kwa ajili ya taifa letu, na kuna tunaomheshimu na kumuombea maisha marefu na aendelee na kazi yake nzito ya kujitoa mhanga kwa taifa letu,

Ni Mungu peke yake anyeweza kumlipia!


Heshima mkuu,

Sasa watu wanapenda wananchi waaachane na hoja za msingi.Hivi wakuu na huyo mramba mbona ameachwa tu maanake nadhani inatakiwa sheria zifuate mkondo wake.Huyu ni mtu ambae kwa madaraka yake ameliumiza sana taifa letu.Hafai hata kuwa mbunge huko Rombo.
 
Hakuna aliyesema Kubemea ni safi,ila kuchanganya hoja mbili kwa pamoja ni kutaka kuua hoja au ku-divert hoja ya kwanza.Tuache track ya ufisadi ibaki kama ilivyo halafu track ya uzinzi iwe nyingine ili haki ijulikane kwa kila track. Kwa hiyo basi kama kuna mtu ana ushahidi wa kutosha juu ya hili la uzinzi aanzishe thread nyingine ili tuijadili.
 
Ukisikia kula chumvi nyingi ndiyo huku sasa. Nilikuwa sifikirii kama bunge letu linaweza kuja kufikia hali hii ambayo lipo sasa. Ukweli huu ni muujiza kabisa. Sasa basi, hii ni hatua nzuri sana ya kuelekea ktk maendeleo ya kweli au ktk maumivu ya kweli. We have to understand that maana chuki pia inajengeka ndani ya wakulu wetu. Lakini hatua kama hii ni ya muhimu kuipitia na inamatunda yake maana kila sent itakayotumika itawekewa maelezo ya kueleweka. Tulikuwa tuko ktk wakati mgumu huoni pa kukimbilia hata kama umeonewa wakulu wote ni majambazi. Kila mmoja alikuwa anakimblia kuwa mkulu lakini sasa ni pa moto lazima ujiulize mara mbili kama ukiteuliwa kuwa mkulu. Lakini sasa nikipata kuonewa najua nikimbilie wapi, kwa Kubenea'''. Hii ndio hali tuliyo nayo sasa.
 
Na uyo kubebena si amebebena mke wa mtu ,au huko hamkutaki lazima muizame upande wa pili wa shilingi ,kamaa jamaa amebebena mke wa mtu basi alihitajika kunyongwa kabisa ,yeye ni muandishi ila sio sosi hivyo hata akihukumiwa kwa kubebena mke wa mtu basi sosi na waandizhi wanaoeshimu wake za watu wapo na wataandika tu.
Halafu hao wabunge wasiegemee kwa kubebena ,hilo alilolifanya kubebena walihitajiwa wao kulipa kipau mbele bungeni na sio raia ambao ni last choice ,waache kwenda hapo dodoma na kupiga makofi tu ,wafanye kazi waseme tusikie ,yako mambo kabakaba wanahitajiwa kuyatolea uvivu sio na mnangojea wazungu wawaletee data ,hivi siku zote za vikao vyenu mnataka kutuambia mlikuwa hamna mlijualo kama nchi inabebenwa.

Hilo la uzinzi watamalizana na mke wake. Hapa tuna-deal na ufisadi ambalo ni tatizo la kitaifa na Kubenea amekuwa mstari wa mbele kabisa katika mapambano ya kuwaangamiza mafisadi akiwemo Rostam.
 
Uzinzi? Wazinzi ni wengi mno ila hawadhulumu taifa. Haufanishwi na ufisadi....

Mkuu FMES heshma kwako,
Tunashukuru kama kalele za chura zinaanza kumzuia tembo kunywa maji
 
Nimefurahi njinsi wanaJF wanavyochambua issue vizuri na hapa ndio mchele na pumba vitaonekana na hii ndio njia nzuri ya kufanya uchambuzi na si kugombana na kutoa maneno makali,``keep it up all``
 
Hapa Bunge limefanya kweli. Bravo!! Watu kama Mwiba ni kuwaacha tu. Naona priority zao zipo katikati ya mapaja.
 
Wabunge wa bunge letu tukufu la wananchi, hatimaye juzi wameweza kuuvunja mkataba wa kampuni ya Karamagi, ambao alikuwa amepewa na Mkapa akiwa rais wa kuiendesha shughuli za kontena katika bandari yetu ya Dar.

According to the dataz, mkataba huo ambao ulitakiwa kuisha baada ya miaka kumi, lakini ukaongezwa na Mkapa kwa kuwashinikiza wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa bandari kuupitisha kwa miaka 15 zaidi. Lakini juhudi kubwa za wabunge na hasa kamati ya Miundo Mbinu ya bunge, wamekuwa wakiulalamikia sana mkataba huo na hata kufikia kuuvallia njuga, mpaka majuzi walipoufuta na kuubatili, ikiwa ni pamoja na kufutwa kwa kipengele kilichowekwa kwa makusudi na Mkapa, kutoruhusu competition ya aina yoyote ile na kampuni hiyo ya Karamagi, ambaye alionekana akitokwa na machozi wakati wote wa majadiliano ya uamuzi huo.

According to more dataz kutoka Dodoma, ni kwamba wabunge wengi wameshitushwa sana na habari za Rostam, kutishia kumshitaki Kubenea, kuhusiana na habari nyingi za ujanja mwingi wa mbunge huyo. Ukweli ni kwamba mbunge huyu amekuwa akitumia majina mengi ya bandia katika kuandikisha makampuni mengi ambayo yamekuwa yakitumika kuinyonya nchi yetu, according to the dataz hata kampuni ya Kagoda kwenye EPA ni mali yake mkulu huyu, lakini alimuandikisha Gulam, ikiwa ni pamoja na Dowans, na kwamba mali nyingi anazozichuma kutoka taiufa letu ameziwekeza Dubai,

Mkulu Kubenea, wabunge wengi wanakuomba usimame kidete na kwamba hata kama kukuchangia hela za wanasheria wa kukutetea zitachangwa, na pia wanatuomba nasi wananchi tusimame imara, ikibidi kumsadia Kubenea ili aweze kusimamia hii kesi iende mahakamani na ukweli usemwe wazi, kwa sababu ushahidi upo, na sasa hivi kuna watu wako huko Dubai, wakitafuta ukweli wote ulipo wa mali za mkulu.

Mungu Aibariki Tanzania, na Mpambano Yanaendelea, Juzi Ilikuwa Chenge, Sasa Bandari imerudi, our next stop Kiwira!

Mkuu, hapa umenifanya kifungua kinywa yangu ya leo imetereza sawasawa.Yaani nimejisikia kulengwalengwa na machozi ya furaha sana.
Mkuu FEMS hizi ndo habari ambazo mie nimezoea kuziona toka kwako.Habari zinazoonyesha uzalendo kwanza, urafiki na kujuana baadaye. Sasa sijui huwa ni kutokana na upepo au jinsi utavyoamka siku hiyo!!! Kama ni kulalia tumbo mkuu ndo kunakufanya uamke vizuri na kutuletea habari nzuri kama hizi nakuomba endelea kulalia tumbo tu(joke).
 
Mkuu MMJ,

Heshima mbele mkulu wangu, hebu tayarisha mitambo ndugu yangu sasa tulete Trekta la kutoka ndani ya bunge kwenye Radio yetu huko, litakuwa tayari anytime kuanzia tarehe 5/16/08,

nitakutafuta ndugu yangu ili tuzisikie kutoka kwenye mdomo wa farasi mwenyewe, jinsi Karamagi alivyokuwa akiangua machozi wakati wananchi wanafanya kweli!

Mpaka Kieleweke! Saa Ya Ukombozi Imefika hiiii!
 
Jamani nahisi hapa hapatoshi, tumechoka kabisaaaa. Ngoja tuende mahakamani tukirudi tutakuwa na wazo jipya. Mtanzania/tanzania sio kichwa/shamba la kutajirikia au kuchuma utakavyo
 
Mkuu Mwiba

""""ni Bora Kumbebena Mke Wa Mtu Kuliko Kulibebena Taifa Zima""
Mh
Kulikuwepo Na Mwanamke Kahaba Akakamatwa Na Kupelekwa Kwa Bwana Yesu Alipofika Pale Yesu Akaambiwa Huyu Kahaba Nasi Twaibiwa Waume Zetu ....wakataka Kumpiga Mawe Wamuue ...ndipo Alipowaambia Hakuna Alie Msafi Kama Kuna Mwenye Uhakika Yuko Safi Achukue Jiwe Aanze Kumpiga Wote Walirudi Na Kuondoka Kama """mwiba"""

*******ushindi Lazima********
 
Hongereni Jf
Hapa Ndipo Wakuu Wote Wanapoamini Hakuna Alie Juu Ya Mamlaka .....
Jf::::jamani Tunaitaji Kufanya Party Kwa Maamuzi Mazito Kama Haya Na Zaidi....tunaomba Tusikie Uchafu Wa Kiwira Umetoweshwa..wana Jf Huu Mwaka Wa Kula 4.....bravo Tuanzishe Thred Itakayoorodheshwa Mambo Ambayo Serikaliwanatakiwa Kufanya ...na Yapi Wamefaulu Yapi Bado...na Hayo Ambayo Bado Wana Jf
Tufe Nao Na Vizazi Vyetu Akuna Alie Juu Ya Mamlaka.......
 
Mkuu, hapa umenifanya kifungua kinywa yangu ya leo imetereza sawasawa.Yaani nimejisikia kulengwalengwa na machozi ya furaha sana.
Mkuu FEMS hizi ndo habari ambazo mie nimezoea kuziona toka kwako.Habari zinazoonyesha uzalendo kwanza, urafiki na kujuana baadaye. Sasa sijui huwa ni kutokana na upepo au jinsi utavyoamka siku hiyo!!! Kama ni kulalia tumbo mkuu ndo kunakufanya uamke vizuri na kutuletea habari nzuri kama hizi nakuomba endelea kulalia tumbo tu(joke).

Nyangumi,
Huyu Marshall Field (CCM Damu) unaweza kusema kuwa wakati mwingine ni kama huwa anapata 'revelation' ya aina fulani (kama yule Saul (Paul?) wa kwenye vitabu?

I only wish he had a firm and consistent stand on such important issues! However, I think there has been a persistent and encouraging stand lately!
Good work FMES.
 
Back
Top Bottom