Hatimaye Subhash Patel amvaa Reginald Mengi

Jana tarehe 30 april Ndg Subhash Patel kupitia kwa wakili wake Julius Lugazya kawafungulia kesi wahariri na magazeti yao ya nipashe na guardian,wakurugenzi wa radio uhuru na ITV pamoja na mwenyekiti wao Mengi kwa kashfa za kumuita fisadi papa na kudai alipata mchuchuma kwa mizengwe.Anawataka waombe radhi ndani ya siku saba na wamlipe fidia ya shs bilioni kumi

Huyu Subhashi Pateli anajiamini kwasababu anajua kwamba ana"support" ya vigigi wakubwa serikalini ambao pia ni mafisadi wenzie........
Lakini....aliyewaweka hawa mafisadi madarakani ni nani..?
Kwa hiyo kama ni sisi....basi na tuendelee hivi hivi....mwishowe...wapiga kura wote watafahamu utajiri wa nchi unapelekwa wapi.....na matokeo yake......kuangushwa kwa mafisadi wote pamoja na mtetezi wao mkuu...Halafu tuone hawa masubhashi watatetewa na nani...!!!


My Vision...
 
Hata papa huvuliwa akaletwa nchi kavu na kufanywa kitoeo.

Lakini ni mpaka avuliwe, akiwa bado baharini ni mbinde kweli kweli kwani hashikiki kirahisi.

Ikishindikana kabisa itabidi tukaushe bahari ili tuwapate Mapapa hawa.
Kelel zote hizi wanajivunia maji yalowazunguka.
 
Wacheni ubaguzi yapo mambo ya kushugulikia katika Taifa hili na sio ubaguzi, kama hao mapapa wamekuwa wakubwa na kuanza kuwakodolea mimacho mtakuwa hamuwafanyii haki.

Waswahili tuna msemo usemao kikulacho kinguoni mwako, sasa na tujiulize ni kipi hicho kilicho nguoni mwetu, jawabu kwa upande wangu ni CCM hata jina linalingana au bado hamjaona ni jinsi gani hilo jina CCM linalingana ila siwashangai kwa sababu ni WaTz ni wavivu, samahani ndivyo viongozi walio madarakani wanavyo tuona.

CCM=Chama Cha Mapapa ,ndio maana yake ,hivyo wananchi wajengwe kukikataa chama hiki cha Sultani CCM kama walivyojengeshwa kule Zanzibar na hususani Pemba ,Pemba ni mfano tosha wameiweka pembeni CCM bila ya kuwakalia kooni mapapa ,hapo mtaona kuwa mmewekwa kwenye mgando kuhesabu mapapa ,na mtamaliza miaka na uzee kuwakumba Mipapa inazidi kunenepa na mwisho kufanya mihujiza ya kugeuka nyangumi.
 
We subiri wanajidai kelele tu sahizi kwa kuwa ubwabwa upo jikoni ikifika 2010 utapakuliwa, kila mtu atasogolea sahani kwa haohao wanaowaita mapapa, si unajua CCM kwa kuzuga, wenzao kule visiwani hawana joto, jeshi tu na wapiga kura hewa ndo vinawakawiza, kuiweka bench CCM, hakuna cha fisadi papa wala nguru.
 
Mimi nina mtizamo tofauti.
Ninaamini itakuwa kazi kweli kweli KUTAFSIRI nini maana ya FISADI PAPA huko mahakamani.

Hapo ndo nitakapokuwa nacheka........
fisadi , pl mafisadi { English: seducer, pl seducers }
noun 5/6an [ photos: upload ]





fisadi , pl mafisadi { English: libertine }
noun 5/6an [ photos: upload ]





fisadi , pl mafisadi { English: evil person[ derived: Arabic ] }
noun 5/6an [ photos: upload ]





fisadi , pl mafisadi { English: destroyer, pl destroyers[ derived: Arabic ] }
noun 5/6an [ photos: upload ]

Swahili Example: lilichumwa na kutupwa na fisadi asiyejua uzuri wa ua [Sul]




fisadi , pl mafisadi { English: corrupt person, pl corrupt people }
noun 5/6an [ photos: upload ]
fisadi , pl mafisadi { English: seducer, pl seducers }
noun 5/6an [ photos: upload ]





fisadi , pl mafisadi { English: libertine }
noun 5/6an [ photos: upload ]





fisadi , pl mafisadi { English: evil person[ derived: Arabic ] }
noun 5/6an [ photos: upload ]





fisadi , pl mafisadi { English: destroyer, pl destroyers[ derived: Arabic ] }
noun 5/6an [ photos: upload ]

Swahili Example: lilichumwa na kutupwa na fisadi asiyejua uzuri wa ua [Sul]




fisadi , pl mafisadi { English: corrupt person, pl corrupt people }
noun 5/6an [ photos: upload ]

PAPA anabakia kuwa shark.

Source: Search Results for 'fisadi' | Matokeo ya Utafutaji kwa 'fisadi' | The Kamusi Project

Kwa sasa nabakia neutral. Maana kila mtu mwenye asili ya kiasia akifanikiwa basi ni FISADI.

Du tunabagua sana jamani!
 
Jana tarehe 30 april Ndg Subhash Patel kupitia kwa wakili wake Julius Lugazya kawafungulia kesi wahariri na magazeti yao ya nipashe na guardian,wakurugenzi wa radio uhuru na ITV pamoja na mwenyekiti wao Mengi kwa kashfa za kumuita fisadi papa na kudai alipata mchuchuma kwa mizengwe.Anawataka waombe radhi ndani ya siku saba na wamlipe fidia ya shs bilioni kumi


Kwa hiyo huyu ndiye yule mwenye Kashifa ya Mchuchuma na ndiye yule aliyekuwa na Kikwete kwenye kuchangia ujenzi wa shule, na ndiye yule mwenye kashifa ya jengo la UVCCM !!?????
 
Tuna shida kwamba mtu akishapata utajiri, tunasahau ujinga wake na ufisadi wake.
 
Huyu ndiye aliyekuwa mweka hazina wa kamati ya mtandao wakati wa kinyang'anyiro cha kumtafuta mgombea wa CCM yeye ndiye alikuwa anakusanya na kusambaza mabilioni yaliyotumika katika kuhonga wajumbe ili kununua kura za kumbeba jamaa ili aingie IKULU.
Aiseeeee !!!!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Ushkaji gani wa kujengeana mahekalu?? sometime inachosha..
a favour for a favour..subash mchafu hio sio siri..haendi mahakamani huyo.
Kuna jamaa ataseme ni mshkaji wake kamnunulia private jet.....dunia haina usawa kabisa
 
Mzee Mengi anazungumza kwa 'metaphor' amewataja mafisadi papa ambao ni dam dam na JK, kwa lugha nyingine Mengi amemtaja JK kama mlinzi wa mafisadi papa,
aminini msiamini, this time kibao kinamgeukia Mengi, lets wait and see.
Japo Mengi ni Mafia, mapapa ni mamafia na JK nyuma yao!.
Nothing happen...JK alikua msela wa mjini...mambo makubwa alikua anayachukulia simple na maisha yalienda
 
Mengi alikuwa anagombana na kila mtu aliemzidi pesa, nakumbuka yeye na kina Idd simba walianzisha movement ya wazawa vs magabacholi. Nyerere aliwaita makaburu wakaufyata...
Subash patel alikuwa mfanyabiashara makini sana na aliitumia vizuri elimu yake
 
Mengi alikuwa anagombana na kila mtu aliemzidi pesa,,nakumbuka yeye na kina idd simba walianzisha movement ya wazawa vs magabacholi.
Nyerere aliwaita makaburu wakaufyata...
Mengi alikuwa na hasira nao kutokana na tabia yao ya uporaji wa waziwazi wa raslimali za nchi!
 
Somo la kwamba binadamu hawezi ishi mile Ni lives Sana

Banza stone alitupa wimbo mzuri Sana inaitwa mtu na pesa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom