hatimaye serikali yaridhia kuwarudisha madaktari (interns)waliofukuzwa muhimbili

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
hatimaye serikali imeridhia kuwarudisha madaktari wanaopata uzoefu kazini(medical interns) ambao walifukuzwa kutoka hospitali ya taifa muhimbili hivi karibuni.haya yamesemwa na ujumbe wa waziri mkuu uliofika kukutana na madaktari waliopo kwenye kikao cha muda mrefu.ujumbe huu unaongozwa na waziri wa afya,katibu mkuu na mganga mkuu kiongozi.

my take
kilichoshindikana wiki mbili zilizopita kimewezekana leo lakini kwa gharama za maisha ya watu.huu ni uzembe wa waziwazi kwa viongozi wa wizara husika.kwa vyovyote vile ni lazima wawajibike kama wanavyotaka madaktari.
 
Serikali ya CCM ni kiziwi mpaka ione ishara kulikua na haja gani ya kukwepana kati ya madaktari na watumishi wa wizara ya afya

nafikiri ni wakati muafaka kwa waziri na naibu wake ku step down
 
Waliokufa wametolewa sadaka kwa ajili ya 2015!
Tz tz nchi yenye mali nyingi watu wengi wa ulaya wana....endelea kuimba
 
Serikali ya CCM ni kiziwi mpaka ione ishara kulikua na haja gani ya kukwepana kati ya madaktari na watumishi wa wizara ya afya

nafikiri ni wakati muafaka kwa waziri na naibu wake ku step down
walichokuwa wanaogopa ni kipi hasa,kwa nini walete majivuno huku wakijua wanaotibu watanzania ni madakatari na sio waziri ambaye kazi yake ni kupokea sifa tu.hawastahili kuendelea kuongoza kwani hiki ndio kilikuwa kipimo sahihi kwa uongozi wao.
 
imeniuma sana kwa uzembe wa serikali kutowasikiza madaktari imegarimu
maisha ya binti wa mfanyakazi mwenzetu na ndie alikuwa kipenzi chake
amefariki leo asubuhi kwa kukosa matibabu
mama wa watu kazirai hata alipoamka haongei na mtu.
 
hapo kwenye red naona Watanzania ndipo tunapaswa kugeukia. Ukweli ni kwamba kama hawa watu walishindwa kujua kuwa walipaswa kufanya hivyo mpaka maisha ya watu yapotee, na sasa kwa vile tumejua kuwa waliozembea sio madaktari bali ni wao basi wawajibike kwa yaliyokwisha tokea.

Kiutendaji hatuwezi kuendelea kuwaamini maana walikuwa na muda wa kutosha kutueleza ukweli na hawakufanya hivyo. Hizo nafasi haziwezi kukosa wa kuzishika maana watanzania tupo karibia million 50
hatimaye serikali imeridhia kuwarudisha madaktari wanaopata uzoefu kazini(medical interns) ambao walifukuzwa kutoka hospitali ya taifa muhimbili hivi karibuni.haya yamesemwa na ujumbe wa waziri mkuu uliofika kukutana na madaktari waliopo kwenye kikao cha muda mrefu.ujumbe huu unaongozwa na waziri wa afya,katibu mkuu na mganga mkuu kiongozi.

my take
kilichoshindikana wiki mbili zilizopita kimewezekana leo lakini kwa gharama za maisha ya watu.huu ni uzembe wa waziwazi kwa viongozi wa wizara husika.kwa vyovyote vile ni lazima wawajibike kama wanavyotaka madaktari.
 
Serikali ya CCM ni kiziwi mpaka ione ishara kulikua na haja gani ya kukwepana kati ya madaktari na watumishi wa wizara ya afya

nafikiri ni wakati muafaka kwa waziri na naibu wake ku step down

Wameshindwa kazi. Waliofariki kwa kukosa huduma katika kipindi hiki wamewalaani viongozi hao kabla ya kufariki.
 
na madai mengine ya madaktari yatatatuliwa?

Hakuna hata dai moja lililojibiwa.
Mbaya zaidi anayejiita mtoto wa mkulima a.k.a mzee wakulia asiyeweza kufanya maamuzi yeyote, yawe marahsi au magumu, ameingia mitini na kumtuma Hawa Ghasia na vilaza wanne( Haji, Nkya, Deo na Nyoni) ambao hawakupewa nafasi yakuzungumza kwa madai yakutokuwa na imani nao. Pia wao ni sehemu ya matatito, hvyo kamati haikuona ni vyema kuwasikiliza, zaidi ya kuwapa mapendekezo ya Wajumbe kuyapeleka kwa Waziri mkuu, huku moja ya mapendekezo hayo ni wao kuachia nyazfa zao kwa kuzorotesha shughuli za wizara.
Mgomo Bado unaendelea, madaktari tutakutana pale Star line kesho kujadili zaidi
 
Inaumiza kuona wagonjwa wanavyoathirika na huo mgomo,lakn sasa madaktar wafanye nn km hawaskilizwi kwa hoja zao za msingi?.Nadhani kwny mchakato wa katiba mpya tuangalie uwezekano wa kuwa na viongozi ambao si wana siasa kwenye sekita nyeti.
 
hii ni sehemu ya madai ya madaktari!!
Huduma Duni wanazopata wananchi.
Uboreshaji wa huduma za afya; Wakati viongozi wakikimbizana kwenda nchini India kwa matibabu,kumekuwa na hali ya kuzorota kwa huduma za afya katika kiwango ambacho hakivumiliki tena, na hali hii kwa kiwango kikubwa inasababishwa na ukosefu wa vifaa tiba, madawa na wataalamu wa afya katika hospitali zetu, mfano ni katika hospitali za manispaa ya Temeke, Mwananyamala na Amana ambapo wagonjwa wanalazimika kujinunulia vifaa tiba na dawa kwa gharama kubwa licha ya wagonjwa kuchangia katika mfuko wa matibabu ya kijamii.
Wakati huo huo, ni kitendo cha aibu na fedheha katika karne hii kwa wagonjwa kulala chini hasa katika hospitali ya rufaa kama Muhimbili na kwingineko. Hali hii licha ya kuwa kero kwa wagonjwa na ndugu zao lakini pia inajenga mazingira magumu kwa watumishi wa afya.
 
Hakuna hata dai moja lililojibiwa.
Mbaya zaidi anayejiita mtoto wa mkulima a.k.a mzee wakulia asiyeweza kufanya maamuzi yeyote, yawe marahsi au magumu, ameingia mitini na kumtuma Hawa Ghasia na vilaza wanne( Haji, Nkya, Deo na Nyoni) ambao hawakupewa nafasi yakuzungumza kwa madai yakutokuwa na imani nao. Pia wao ni sehemu ya matatito, hvyo kamati haikuona ni vyema kuwasikiliza, zaidi ya kuwapa mapendekezo ya Wajumbe kuyapeleka kwa Waziri mkuu, huku moja ya mapendekezo hayo ni wao kuachia nyazfa zao kwa kuzorotesha shughuli za wizara.
Mgomo Bado unaendelea, madaktari tutakutana pale Star line kesho kujadili zaidi

hivi ni shida saana kwa tanzania bldg agency au nhc kujenga nyumba au ma-flat karibu ya hospitali kwa ajili ya wataalamu wetu wa afya inluding manesi? kuongeza vitanda hospitalini na majengo pia , kuwepo kwa vifaa vya kutosha nk ili wanaonde apollo wapungue na tuwatumie na kuongeza ujuzi wa wanataaluma wetu.
 
Hilo litaondoa madai ya mazingira bora ya kazi kama nyumba, posho za mazingira hatarishi na madai ya nyumba?
 
Back
Top Bottom