Hatimaye Serikali Yakubali

Sabi Sanda

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
409
31
Wakuu,

Inatia moyo kuona kuwa hatimaye Serikali imeafiki wazo la kuwafundisha Wanafunzi wetu kwa Njia ya Televisheni. Baadhi yetu tuliandika wazo hili kwa kirefu miaka mitano iliyopita na temeendelea kuliandikia kila mara. Inatia sana faraja kuona kuwa hatimaye limekubalika na utekelezaji wake utaanza rasmi mwakani na shule za majaribio zitaanza mwaka huu mwezi wa nane---Someni Gazeti la HabariLeo la Leo 18/05/2010 uk wa 1.
 
Hii itakuwa na maana iwapo tu
1. TV zitasambazwa katika shule nchi nzima
2. Solar Power itatumika sehemu ambazo hazina huduma ya umeme
3. Pesa za kutosha zitatengwa kwenye bajeti ya mwaka ujao [vinginevyo ni wale wanafunzi wa mijini tuu ndiyo watakaonufaika na mafunzo hayo
 
.....kivipi? mbona sijaelewa!!!. hebu dadavua kufundisha kwa njia ya television, how
 
Video conferencing, online tuition, videotapes, audiotapes etc. Lakini StarTV walikwisha anza siku nyingi kuwa na kipindi cha darasani! Je watatumia cable television?
 
Sasa nyie kama mlianza kuomba miaka mitano iliyopita infrastructure mliiona inafaaa? Maana hawa jamaa huwa wanaamlia juu sasa ebu ona mwezi wa nane wanaanza na shule kadhaa sasa kuna maadalizi kwa hili au inakuwaje? naomba maelezo kaka.
 
naanza kufikiria vibaya....je wanafuzi wa vijijini ambako hakuna TV watafanyeje?na kwa nini wafundishwe na tv?kama wameshindwa kumuelewa mwalimu wataye muuliza maswali na kujadili nae,je hizo tv zitasaidia?jamani tutabaki wajinga mpaka lini?
 
Hii itakuwa na maana iwapo tu
1. TV zitasambazwa katika shule nchi nzima
2. Solar Power itatumika sehemu ambazo hazina huduma ya umeme
3. Pesa za kutosha zitatengwa kwenye bajeti ya mwaka ujao [vinginevyo ni wale wanafunzi wa mijini tuu ndiyo watakaonufaika na mafunzo hayo

Abunuwasi, Kimsingi hivyo ndiyo itakavyofanyika. Aliye na document ya TANZANIA BEYOND TOMORROW (TBT) naomba atuwekee hapa.
 
Back
Top Bottom