Hatimaye posho mpya za wabunge zafutwa rasmi

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,932
32,337
Wanabodi.
Hatimaye nyongeza ya posho za vikao vya wabunge kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 zimefutwa, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema.

Kauli hiyo rasmi kutoka kwa kiongozi wa Bunge imekuja baada ya kuwapo kwa taarifa za kutatanisha kuhusu posho hizo..

Baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge kutangaza Rais Jakaya Kikwete, aliidhinisha lakini Ikulu ikakanusha.

Ndugai alisema posho hizo hazijawahi kulipwa kwa kuwa Rais hajatoa kibali cha kufanyika hivyo.

Hakuna cha spika alisema hapo Ikulu imesema Rais hajasaini posho zitaendelea zile za zamani kama kawaida.

SOURCE: MWANANCHI FEB 14 2012
 
Hiyo haitoshi, zingefutwa kabisa hata hizo 70,000/-. Watu wenyewe kazi yao kulala tu na kupumulia masaburi,hizo 80,000/- za kujikimu zinawatosha sana hawa wachumia tumbo.
 
Kuna mtu anatakiwa awajibike hapo. Serikali moja lakini kauli tofauti tofauti. PM kauli yake, Spika kauli yake, naibu spika naye na mwisho Mkuu wa Serikali na Nchi naye anakanusha.
 
Hiyo haitoshi, zingefutwa kabisa hata hizo 70,000/-. Watu wenyewe kazi yao kulala tu na kupumulia masaburi,hizo 80,000/- za kujikimu zinawatosha sana hawa wachumia tumbo.

Kwa mujibu wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano uliopitishwa katika kikao cha bunge la bajeti 2011 posho zote za makalio zitakuwa zimefutwa!
 
Wewe binafsi unalisemeaje suala hili?..maana wewe hutabiriki, si ndege si mnyama!

PakaJimmy
Huyo ni Mnyama Popo.
Ingawa ana mabawa huyo bado si ndege kwa maana anamatiti yanayonyonyesha kama mammals wengine.
Please note-elimu ya Kibiologia inahitajika ili uewze kumfahamu vizuri.
 
Kabla ya kutolewa kwa taarifa hii ilitakiwa Rais awe ameshamwondoa Waziri Mkuu na kulivunja Baraza la Mawaziri. Haiwezekani viongozi waliokabidhiwa dhamana ya kuliongoza taifa letu wanakuwa na kauli tata na zinazopingana kwa kiasi hicho.

Aidha, Wabunge walitakiwa pia kupiga kura ya kutokuwa na imani na Spika kwa kauli zake tata bungeni na nje bunge pia.
 
Good move. Sasa wale walioupotosha UMMA (Pinda na Makinda) wameomba radhi?
Na sijui ni kwa nini instinct zangu zinaniambia hii kitu imewekwa pending kwa muda tu.
 
Huyu Ndugai si ndio hadi alikuwa anataka hadi kutoa watu roho kwa ajili ya hizo posho. Leo ndo anajifanya na yeye hazikubali. Mnafiki mkubwa huyo.
 
Hiyo haitoshi, zingefutwa kabisa hata hizo 70,000/-. Watu wenyewe kazi yao kulala tu na kupumulia masaburi,hizo 80,000/- za kujikimu zinawatosha sana hawa wachumia tumbo.

au wangepewa wabunge wa CDM maana hao ndo wanafanya kazi kweli kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom