King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 51,328
- 67,762
mkuu hawa jamaa usiwape kauli za kuwasamehe kirahisirahisi hivyo. wameshatunyanyasa mno hawa, sehemu za migodini kule Mara binadamu na mifugo tunadhurika na makemikali ya migodini, tukiwaambia wanaanza kutudhihaki. in-short hawa magamba wameshatusulubu vya kutosha hasa hizi awamu za pili, tatu na nne. yaani ni wadhulumaji na wanyang'anyi wa mchana kweupe. wanajijari wao tu na washikaji zao. hawa sio watu wa kusamehe kirahisi. tuwatoe kwanza madarakani halafu ndio tufikirie kuwasamehe.
Nyerere alishawahi sema kwamba katika hawamu zilizopita wamefanya ya kijinga na ya maana,sasa inabidi hawamu inayokuja(jk/mkapa) watoe mabaya na waendeleze mema! Sasa cha kushangaza hawamu hii inafanya ya kijinga tu,dawa yao 2015!! Hawa Jamaa sijui wanafikiri watatawala milele? Kulikua na Kina Hitler,kina Kuku wazabanga,Gaddafi,Al-Capone,wako wapi?