Hatimaye Nape Nnauye atinga Igunga

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
...Akiandika katika mtandao wa Facebook kwenye profile yake katibu mwenezi wa CCM ndugu Nape Nnauye amedai katua Igunga leo asubuhi na kujihakikishia ushindi kwa asilimia 100...Na akatoa kejeli uchwara kwa watanzania kwa kusema na hapa namnukuu kama alivyoandika kwenye profile yake bila kubadilisha neno hata moja....

"Oooh Nape hataenda Igunga".... Nikiwa Igunga leo asb" USHINDI WA CCM IGUNGA NJIA NYEUPEEEE"


....Akaendelea kuchangia baada ya watu kucomment kwenye post yake........

"Mliuliza maswali ya kejeli hapa, nikajaribu kufafanua watu wakaendelea kukejeli tena ni jana tu kuwa mwenezi gani haendi kukisemea chama.. Sasa nipo Igunga njooni mseme tena waungwana.."


Mwisho wa kumnukuu..............

288612_262123397142414_100000342668655_927568_8099788_o.jpg
 
Eee,sihasa za kileo bhana,,,,,,,haya mi si mwanaigunga wanaigunga watapima wenyewe na wataamua
 
Always mfa maji haishi kutapatapa, hata mgonjwa anayekaribia kukata roho huwa anafarijiwa/kujifariji kuwa anapona. Anyway Labda kwa uchakachuaji ndio njia nyeupe. Lakin nawapa pole magamba kwa msiba wanaoenda kuupata kwa kuondokewa na Igunga.
 
Nadhani hoja za kisiasa ujibiwa kisiasa na si mipasho.Nakumbuka alijitokeza hapa katika thread moja ya ''wapi Nape'',alipata kejeli nyingi hapa kuwa amezuiliwa kwenda Igunga kupitia kikao cha kamati kuu ya Chama (CC).Wengi tuliamini hatokwenda kulingana na uvumi uliokuwepo sasa kama amefika basi kulikuwa na uzushi hapa tukubaliane.

Sidhani kama tunapaswa ku-challenge hili.
 
Huyu kijana amepata pesa zimemharibia mwili yaani anenepa hovyo siku hizi hata kusimama ni shida, asipo angalia atapata Obesity.
 
Adui mkubwa wa maendeleo ya nchi hii ni SIASA. SIPENDI SIASAAAAAAAA............
 
Nadhani hoja za kisiasa ujibiwa kisiasa na si mipasho.Nakumbuka alijitokeza hapa katika thread moja ya ''wapi Nape'',alipata kejeli nyingi hapa kuwa amezuiliwa kwenda Igunga kupitia kikao cha kamati kuu ya Chama (CC).Wengi tuliamini hatokwenda kulingana na uvumi uliokuwepo sasa kama amefika basi kulikuwa na uzushi hapa tukubaliane.<br />
<br />
Sidhani kama tunapaswa ku-challenge hili.
<br />
<br />
palikuwa na makubaliano ya kumtumia rostam kwenye kampeni igunga, msemakweli katibua ratiba kwa kumchana rostam. imebidi magamba kupanga upya ratiba ili nape apate angalau cha kujichekeshachekesha!
 
Back
Top Bottom