Hatimaye mkuu wa chuo cha Mkwawa na wasaidizi wake wang'oka kwa wizi

Feb 3, 2012
77
48
Habari za uhakika kabisa ni kwamba Mkuu wa chuo cha mkwawa iringa amepewa barua ya kukabidhi ofisi ifikapo Jumatatu asubuhi sambamba na wasaidizi wake 2! Na hii inatokana na tuhuma nzito za matumizi na usimamizi mbovu wa mali za chuo hiko ikiwa ni pamoja na wizi wa pesa za mikopo kwa wanafunzi kutoka LOAN Board zinazomgusa moja kwa moja mkuu huyo! Tayari PCCB imewahoji kwa kirefu watuhumiwa wote wa wizi huo! Na hii inaashiria hatua moja ya kuwafikisha mahakamani wahusika wotze!
Source! Mtu wa ndani katika chombo cha maamuzi mkwawa.
 
Akishaondoka ofisini ndo mambo yameisha,hakuna kesi wala nini,pale duce kuna mmoja alikwapua kwa fujo,aliondolewa tu na bado anadunda mlimani,blandina nyoni kashitakiwa wapi?
 
Akishaondoka ofisini ndo mambo yameisha,hakuna kesi wala nini,pale duce kuna mmoja alikwapua kwa fujo,aliondolewa tu na bado anadunda mlimani,blandina nyoni kashitakiwa wapi?

Mkuu issue ya DUCE inaingiaje hapa?
 
Hoja yako inawezekana ikawa na mashiko! Mke wa waziri moja nyeti kutoka mikoa ya kusini ameteuliwa kukaimu nafasi ya ukuu wa Chuo! Ni kupeana ulaji kama kawaida!
 
Naomba nitoe sahihisho, kwa taratibu za chuo kikuu cha Dar es salaam, kiongozi anakaa miaka 3 na baada ya hapo mabadiliko yeyote yanaweza tokea. kwa upande wao mda wao umefika wa kuondoka. Pia hayo ni mabadiliko ya chuo kizima cha Dar es salaam na Campus zake. Pia viongozi wakubwa hawakuhusika na wizi huo, ni wale vijana wa chini na hilo linafahamika. ahsante
 
hawa jamaa ni wezi sana na ndio maana wanafunzi wanapata tabu sana wakati wanasoma, hakika kama serikali itakuwa macho na vyuo vingine wanaweza kung'oa wakuu wa vyuo wengi maana wanaonekana kuishi kama peponi .
 
Mtz Halisi! Search ilikuwa inaendelea katika Campus zote za chuo kikuu na wote walipendekezwa kuendelea na nafasi zao, lakini kutokana na madudu ya hawa waheshimiwa utaratibu huo umesitishwa kwa muda kupisha uchunguzi wa kina ili kuwafikisha Mahakamani wahusika wote! Hata hivyo mkuu wa chuo MUCE anahusishwa moja kwa moja na tuhuma hizi!
 
Habari za uhakika kabisa ni kwamba Mkuu wa chuo cha mkwawa iringa amepewa barua ya kukabidhi ofisi ifikapo Jumatatu asubuhi sambamba na wasaidizi wake 2! Na hii inatokana na tuhuma nzito za matumizi na usimamizi mbovu wa mali za chuo hiko ikiwa ni pamoja na wizi wa pesa za mikopo kwa wanafunzi kutoka LOAN Board zinazomgusa moja kwa moja mkuu huyo! Tayari PCCB imewahoji kwa kirefu watuhumiwa wote wa wizi huo! Na hii inaashiria hatua moja ya kuwafikisha mahakamani wahusika wotze!
Source! Mtu wa ndani katika chombo cha maamuzi mkwawa.

Na ndio maana naipigania Katiba Ya Kidikteta, itakayoondosha Western Styled Good Governance na kuleta Approved Dictatorship Governance.
 
Back
Top Bottom