Hatimaye Mbeya kumetulia

Biz2geza

Senior Member
Oct 12, 2011
117
20
Baada ya vurugu za wamachinga wakidai haki zao za msingi na wakitoa shinikizo kuwa hawataki kuongea na mtu mwingine yoyote zaidi ya rais wao sugu.wakidai kuwa hali itarejea ikiwa haya yafuatayo yatatekelezwa

1. Waakikishie kuendelea kufanya biashara katika maeneo yao.
2. Wenzao wote walioshikiliwa na polisi waachiwe bila masharti
3. Wote waliopo hospitali kutokana na majera ya vurugu hizo wapatie matibabu ya hali ya juu.

Baada ya kikao kilichofanyika kati ya sugu na serikali ya mkoa. Kandoro amekubali kutekeleza masharti yote matatu na wamachinga wanarejea katika maeneo yao. Kwasasa sugu anaongea na wapiga kura wake wanamshangilia mbaya.

Big up sugu wapiga kuwa wako wamekupa heshima kubwa sana na hii ni salamu kwa serikali kuwa nguvu ya dola haishindi nguvu ya umma.
 
Mkuu ahsante kwa taarifa!! Tuwekee na picha ya Mhe. Sugu akiwahutubia makamanda wa Mbeya!!
 
Chadema peoples power ................................................... Pinda alie tu kama alivyozoea
 
Watawala inabid watafakar ya kuwa aman haiji kwa kutumia vyombo vya dola bali mazungumzo!well done wana mbeya
 
walikuwa wapi muda wote mpaka wakapoteza roho za watu? hongera Mbeya kwa msimamo mliyoonyesha.kwa pamoja tunaweza
 
Nimeipenda hiyo wakazi wa mbeya kukataa kuongea na mtu yeyote yule ila Sugu. Hiyo ni nguvu ya umma na taarifa nzuri kwa JK na serikali yake.
 
wao wanawaona wabunge wa cdm ni wahuni lakini wanasahau kuwa hao ndiyo chaguo la wananchi na hawakuchakachua.walianza arusha kumuomba mbowe na leo tumeona kwa sugu kwanini hawakumuomba shitambala kama kweli yeye ndiye kipenzi chao?
Katika hili wamejionea jinsi nguvu ya umma ilivyokubwa.wanajeshi wanapita vijana wanawambia peoples power tunaongea na raisi wetu.
 
big up Mbeya..ndivyo migogoro inavyomalizwa kwa k usikiliza kilio cha wananchi na sio mabomu ya machozi na risasi za moto!
 
Mnashangilia wakati wenzenu tayari wameshapata kipondo na wengine wamepoteza maisha! Ama kweli watu hamnazo kabisa.
 
Sugu tutakupenda endeleza ukombozi wa nchi yetu tutapigania mpaka mwisho.
 
Sugu Moto chini tanlalalalalaaaaaaaaa ni moto chini Huyo ndo kiongozi si unakumbuka kuna kipindi polisi washawahi kuua watuhumiwa waliwaweka kwenye kaselo kadogo
 
baada ya vurugu za wamachinga wakidai haki zao za msingi na wakitoa shinikizo kuwa hawataki kuongea na mtu mwingine yoyote zaidi ya rais wao sugu.wakidai kuwa hali itarejea ikiwa haya yafuatayo yatatekelezwa
1. Waakikishie kuendelea kufanya biashara katika maeneo yao.
2. Wenzao wote walioshikiliwa na polisi waachiwe bila masharti
3. Wote waliopo hospitali kutokana na majera ya vurugu hizo wapatie matibabu ya hali ya juu.
Baada ya kikao kilichofanyika kati ya sugu na serikali ya mkoa. Kandoro amekubali kutekeleza masharti yote matatu na wamachinga wanarejea katika maeneo yao. Kwasasa sugu anaongea na wapiga kura wake wanamshangilia mbaya.
Big up sugu wapiga kuwa wako wamekupa heshima kubwa sana na hii ni salamu kwa serikali kuwa nguvu ya dola haishindi nguvu ya umma.

Jana wakati kikao cha bunge kikiendelea nilimwona Mh. Sugu anachat na Mh. Pinda, nkakumbuka ile taarifa ya spika kukataza wabunge kumsonga pinda wawapo kikaoni!

Nkajang'amua jioni kumbe alikuwa anambrifu yaliyokuwa yanajiri kule mbeya, yaani waziri mkuu anapewa taarifa na raisi wa mbeya ndo akaanza safari kuelekea mbeya,

hongera sugu kwakuwa active. chichiem kwishney mwanawane!
 
Wewe naona hujui kuwa ukombozi huwa kuna watu wakujitoa sadaka kwa ajili ya wengine. Naona huijui historia ya ukombozi ilivyo. Huwa ni lazima wachache waumie ili kutokee mabadiliko bila hivyo usitegemee watawala watawasikiliza. Hata kama watu wameuawa na wengine kujeruhiwa lakini watawala wamenyosha mikono fuatilia nini wamekubaliana.
 
Back
Top Bottom