Hatimaye kitendawili cha lowasa kuhamia chadema chatenguliwa leo.

unajua watanzania tunapenda sana ku label watu vibaya..kwa hali ya maisha yetu haya ..kila mtanzania ni mwizi ila tunatofautiana fursa tu ...mwacheni mzee wa watu kama mwizi haya lakini mwisho wa siku akitaka kuja chadema tutamkubali au kumkataa kwa kuangalia vigezo ....nadhani tushafahamiana
 
Labda niwakumbushe. Ni nani aliyechukua uamuzi mgumu wa kutoa maji ziwa victoria pamoja na wamisri kugoma? ni nani aliyevunja mkataba wa city water? ni nani aliyeshauri mkataba wa richmond uvunjwe? ni nani aliyesimamia ujenzi wa shule za kata na alipoondoka kila kitu kikasimama?,. Naomba tuwe wakweli kila mtu ana madhaifu yake.
 
Jamani naomba mnisaidie jambo moja,hivi hasa ufisadi wa huyu Lowassa kwa nchi yetu ni nini?Najua alijiuzuru uwaziri Mkuu kwa kashfa ya Richmond,lakini je,anahusika vipi na ufisadi?
Nimekuwa nikimchukia huyu Lowassa kwa namna tofauti kidogo ambayo si ya kisiasa ni ya kiutendaji zaidi na inanigusa mimi binafsi.
Wakuu naomba mwenye data za huyu jamaa anisaidie hapa maana nimekuwa nikitafuta data zake lakini sizipati.

Kwani unataka mpaka TBC watangaze ndio uamini? kwa taarifa yeye yuko behind the EPA na mengi aliyofanya Rostum Aziz yana mkono wake lakini haya hayawezi kutangazwa na TBC na ndio maana hadi leo wamiliki wa kagoda hawatajwi...
 
Back
Top Bottom