Hatimaye Kikwete Afanya Kweli

Ninadhani ukisoma kwa makini utagundua tu kuwa Salim wengi wanmkataa kwa rekodi yake!

Hilo la uarabu linakuja baadaye kabisa. Na linaweza hata kuondolewa!


Ni kweli kabisa kuna baadhi ya Makabila yameprove ukabila kwenye nafasi tu cha chini! sasa ukiwa urais si watayafanya hayo makabila kuwa bora kuliko mengine maana mkabila hiyo ndiyo imani yake!

Na wakisha fanya hivyo makabila mengine yatanung'unika na mgawanyiko utanukia!

sidhani kama ni sahihi kabisa kusema kabila fulani halitakiwa kutawala bali ni kuwa makini na kujaribu kuwasomesha ili waelewe kuwa kabila lao siyo bora kuliko mengine. Lakini kubadili tabia ni kazi! ndiyo maana panga pangua wizi ukitokea iwe ndani au nje ya nchi mtu au watu wa kabila fulani utwasikia! hata wizi wa kuwa marekani

http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2006/05/29/67390.html

Tusipokuwa makni watanzania sasa tutanza kuogogwa nje ya nchi kama wanigeria!!!!!!!
 
Mkira, unaona umeingia kwenye mtego mlioutega wenyewe... Hivi kuna uwezekano gani wa watu wa kabila moja kuwa wengi zaidi nje ya nchi na hususan katika nchi fulani? Ukilinganisha Waha na Wachagga unafikiri ni wepi wako nje na kwa nini? Uhalifu hauna kabila wala dini!

Mkishaanza kuuliza uarabu wa mtu, hamna budi kuuliza juu ya Uchagga wa mtu au Unyakyusa wa mtu!! Hilo suala la uarabu halina nafasi na wala halistahili kuingia hata kidogo, hata kwa kisingizio cha kuipenda nchi!! Kama ni suala la rekodi, basi rekodi hiyo iwekwe wazi, kama ana utetezi autoe au akiri makosa!! lakini kumhukumu mtu kwa sababu anatoka kabila fulani au ni wa rangi fulani, ni kosa ambalo hatuwezi kumudu kulifanya!! Vigezo vyangu kwa kiongozi ni rahisi:

a. Awe ni Mtanzania kwa sheria ya uraia wa Tanzania
b. Awe ni mtu mwenye uwezo wa kitaaluma au kipaji kuongoza
c. Awe na rekodi inayoonyesha umahiri na kubobea kwake katika uongozi
d. Asiyewahi kutumia madaraka yake vibaya wakati wowote
e. Mwenye kuweka utii wake kwa Jamhuri na Katiba yake na si kitu kingine chochote.
f. Asiye mbaguzi wa aina yoyote.
g. Mwenye kutekeleza sera zenye kuleta maendeleo kwa Watanzania wote.


Mtu mwenye sifa hizo, awe mwarabu, mhindi, mchagga, mzungu, msukuma n.k na kama sera zake nakubaliana nazo basi huyo nitampigia kura!!! RANGI, KABILA, au NASABA ya mtu iwe MWIKO!!!!! As a matter of fact, ninasema chama chochote kinachohoji rangi ya mtu kwenye uongozi chama hicho kifutwe au kiongozi huyo avuliwe madaraka!!!
 
mwanakijiji ukinisoma vizuri hapo utaona kuwa ninasema kigezo cha kabila si muhimu kwa mtu kuwa rais wa Tanzania.

Ila ninachosema na ni obvious ukienda bongo ukamuuliza kila mtu na haihitaji hata cheti cha darasa la saba! utaona kuwa kuna baadhi ya Makabila yanaendeleza sana ukabila hasa katika ajira bila AIBU!

Ninakubalia na sifa zote ulizoziweka hapo juu na za kwenye katiba yetu isipokuwa ile ya umri zaidi ya miaka 40!

Kwa hiyo hayo makabila unayosema iko siku mtashika nchi HAKUNA WA KUWAZUIA ILA IKITOKEA TUKAWA NA RAIS MKABILA THEN BADALA YA KULALAMIKIA TATIZO MOJA LA RUSHWA NA UFISADI TUTAANZA TENA KUWA NA TATIZO LINGINE LA UKABILA HUONI HIYO NI MBAYA ZAIDI!

LAKINI NAFASI YA KUWA RAIS IKO WAZI KWA KILA MTANZANIA NA MNA NAFASI KUBWA YA KUUPATA HAPO BAADAYE MAANA MWAKA JANA KANDA HIYO ILITOA WAGOMEA 6 KATI YA KUMI. KWA HIYO MIAKA IJAYO MKIENDELEA NA MOYO HUO MTAFANIKIWA TU. LAKINI CHA MAANA NI KUBADILIKA NA KUKUBALI KUWA SOTE NI WATANZANIA NA WOTE WAMESOMA JAPOKUWA MNA SHULE ZA SERKALI 265 HUKO MOSHI WAKATI DODOMA MAKAO MAKUU WANA SECONDARY 6 TU.

ANYWAY HILI TULIACHE MAANA LINAUMA SANA!!

LAKINI NINAKUBALIANA SIFA ULIZOWEKA KAMA UKO SERIOUS JE KWELI UNA IMANI KUWA IKO SIKU TUTATAWALIA NA MHINDI!!!!!!!!!!!!
SOMA HISTORIA YA NCHI MBALI MBALI! HUKO MAREKANI ULIKO JE WATAKUWA NA RAIS MWAFRIKA LINI??
BYE FOR NOW
 
mimi nimependezea sana na hii forum haswa, katika topic ya siaa maana mimi napenda sana maswala ya siasa, Baada ya hapo napenda niwapigie hodi ndani ya Ukumbi huu, kisha nikishakaribishwa nitaangusha mawazo yangu hapa.
siku njema
 
Kwikwikiw wacha kwanza nicheke maana naona watu mnaleta mahoka hapa .Haya ndiyo yale yale ya JK kuwakimbia watanzania huko Ugenini kisa watamuuliza maswali ambayo hayatamjenga .

Look Salimu UN alipigwa chini kwa Uarabu wake lakini ni Mtanzania wa kila kitu ila damu tu ya Uarabu Reagan akasema no huyu ni Mwarabu. Salimu kwao Zenji alipigwa chini kwa Uarabu wake na hao ndiyo wanaomjua zaidi kuliko sisi Wabara .

Swala kuwa mtu anafaa achaguliwe kisa ni Matanzania nooooooooooo Tanzania ni ya mtu mweusi na kumpa Mhindi njia ya kuingia Bungeni ni favour tu mambo kama haya yamewachukua wahamiaji katika Nchi zingine miaka kabla hawajawa accepted kwenye Mabunge yao lakini sisi Watanzania hatuna sana hayo ila wao wana mambo ya ajabu .

Lazima kuusimamia Utanzania kikamilifu maana hakuna Mtanzania ambaye anaweza kukaa Uarabuni ama hata India kesho aka qualify kuwa Raia akaishia Bungeni ama kwenye madaraka makubwa kama tunavyo waachia wageni hapa Tanzania .Unamkumbuka Jamal Waziri wa Fedha Mtanzania Mhindi na alikuwa Kipenzi cha Mwalimu ? Alipokufa alizikwa wapi kama si Canada ? Jamani tuangalie haya tuache kusema kwa urafiki ama manufaa binafsi.

Swala la Ukabila ni nyeti sana .Kama kweli mtu kashika Wizara kabila moja limeshika madaraka kila kona kwenye Wizara hiyo je unaona ni mchezo ? Whre do you place our Nation Unity ambayo tunaamini katika Tanzania kama Nchi na si Ukabila ?

We need fight this right now .Hii ni mentality ambayo ni ugonjwa pia .Nasema hakuna ku beep tunafanya kweli .Mkabila ma mtaifa hatufai.
 
Mzee Kimbembe,

Wachaga walikuwepo Hazina, na BOT (Freeman), hata kabla ya Mramba, toka enzi za yule Mhindi, baadaye Msuya(Mpare), Mtei (Mchagga), Kibona (Mbeya), Malima (Mzaramo), Kikwete (Mkwere), Yona (Mpare), Mramba (Mchagga), wachagga walikuwepo tu pamoja na kubadilishwa kwa mawziri weee, na ukiangalia hii list kwa makini ni lazima ukubali kuwa hawa wachagga kina Mengi hawa, katika bongo wana ujuzi fulani wa mahesabu ambao makabila mengine hatuna, ni vizuri tukubali yaishe! Wachagga kwa mahesabu ni namabri moja,

TRA huyo alikuwa Ben na mzee Sanare, ndio waliowajaza wachagga ambao no question kuwa ni qualified katika hiyo field I have no problem kukubali kuwa Wachagga ni wajanja long time kabla ya sisi wengine,

.....mimi ninakumbuka nikiwa boarding School jaamaa wa kichagga walivyokuwa tofauti na sisi makabila mengine, sisi tuko darasani jamaa wako maporini kutafuta madini, ngozi za chui na meno ya tembo, na wakirudi darasani kitabu kinapanda kama kawaida, Jumapili wao hukaa chini ya kivuli na kusikiliza miziki ya Jimmy Reeves na Doly Parton, sisi tunahangaika na kwenda mjini kuzurura bila sababu bro!

Mzee Mwanakijiji,

Ninaamini huko US wewe sasa ni naturalized Citizen, hebu kachukue fomu ya urais wa US kama watakupa hao wenzetu si ndio watu wasoijali ubaguzi!


Salim ni mwarabu wa Zanzibar, basi aende huko wampatie urais huku bara hatutaki! Tumekataa as taifa na hakuna aliyelalamika, njia iliyotumika NO! sio ustaarabu CCM wangemwambia tu ukweli kuwa wewe ni mwarabu, hizo nafasi zote za uongozi alikuwa anakupatia Mwalimu sio sisi ila hatukuwa na nguvu za ksiiasa, sasa tunazo tunakwambia hapana nenda visiwani kwenu huko! Na nyinyi mnaojifanya kina Mother Theresa hebu nendeni huko uarabuni mkajionee weusi wanavyofanywa na waarabu weupe, huyu Salim kule Adis alikuwa kaiajiri waarabu wa Oman tu, Mtanzania aliyemuajiri kule ni Bandora tu ambaye we know better kuwa ni Mrundi!

Asha Rose sio Mtandao hata siku moja, ni one of the only kiongozi Clean katika Ari mpya asiyekuwa na makundi, ninasema sio mtamndao wala mtu yoyote ni yeye na elimu yake na uwezo wake kikazi, nenda upitie kule wizara ya kina mama usikie vitu vyake akiwa pale, sasa hivi foreign kunawaka moto watu walikuwa wamezoea kulala tu, Mramba ni kiongozi bora na hata JK ilibidi ajieleze kwa kirefu kwa wafadhili kwa nini alimtoa kule hazina, kwani walisha tishia kutotoa tena misaada,

Tanzania hatuongozwi na mataifa ya nje, lakini ni lazima tujue kwa nini wanamkataa kiongozi wetu? Butross Ghali aliingizwa na wafaransa sio US, na US hawakupinga kwani siku zote Ghali alikuwa kwenye payroll ya CIA, na ndiye West waliyemtumia kumdanganya Sadat aweke mkataba na Israel, kama West walivyomtumia mke wa Gorbachev aliyekuwa CIA kuvunja USSR, hawa wote kina Annan ni walikuwa kwenye payroll ya CIA, ndio maana bwana Ghali alipokataliwa na US Congress ya Republican ya kina Gingrich wafaransa wakamchukua na kumpa ukatibu wa Francophone, hakupewa UN kwa ajili ya uarabu wake NO!, ila usaliti wake hio siku zote ndio tabia ya West. Hakuna mtu anayeingia Cuba na kutoka bila CIA kujua na kumfuatilia mpaka mwisho, Salim alipokuwa kule siku zote walikuwa wanamfuatilia ndio maana wana info zake kibao ambazo walimegea mwalimu,

lakin back to the point Salim ni mwarabu wa Zanzibar, kwa hiyo ni vyema akaanzia urais huko,

ndio maana mzee Kennedy alipumzishwa maana hakuwa Mzungu kama kina Clinton, Bush, Reagan, yeye alikuwa mu-Irish kwa West huyo sio mzungu, ndio maana Dukakiss alishindwa maana alikuwa Mgiriki au Mmanga huyo, sio Mzungu, ndio maana hawa kina Guliani na Pataki hawatapata chochote maana sio wazungu, Guliani ni Mtaliano, na Pataki Mhungary, sasa Tanzania tunafuata nyayo tu za Demokrasia za ukweli huko majuu Au vipi?
 
Wanabodi,
Sikupenda kabisa kuingia ktk mada hii ila nitajaribu kuweka record hapa clear, kisha wenyewe mtapima marefu ya hili swala..
Choveki was right...Salim alikataliwa na Marekani kwa sababu anatoka Black Africa!..Na Marekani pekee wali- veto kwa kisingizio hicho hali ukweli ulisimama kwamba Salim na Tanzania tulikuwa WAJAMAA, kwa tafsiri yao communists.
Sali hana back ground mbaya zaidi ya kuwa mwanachama wa Hizbu..Hilo ni swala la Zanzibar sio bara pia tukumbuke wakati ule vyama vyote hata Shiraz kilikuwa chama cha kinachotafsirika kwa rangi. Machungu yetu tuyageuze pia kuangalia waarabu ambao walikuwa nje kutazama viongozi wa Shiraz.
Kweli Mzee Es anaweza kuwa na point, kwa sababu sio kila raia anaruhusiwa kushika nafasi ya Urais.. sii Marekani, Arabuni wala Uchina. rais ni wadhifa tofauti kabisa na nafasi ya kazi na trust me tunaweza tafsiri tunavyopenda lakini Mzungu hawezi tawala China wala Mchina kutawala Ulaya..
Binafsi naweza kusema case ya Salim kidogo nzito kutokana na historia ya nchi yetu. Ukichunguza kwa makini unaweza kuta familia ya Salim ilikuwepo Pemba hata kabla ya Wagogo kufika Dodoma toka south, ama Wahangaza kufika Ngara kutokea huko Ethiopia via Rwanda!.. sasa hapa na ni raia!
Hapohapo sikubaliani na madai kuwa mtu yeyote kwa rangi ama kabila kuchukua Urais kama hatakuwa mzawa, bila asili ya Tanzania, na kubwa kuliko yote - yeye, wazazi ama nasaba yake ni raia ya nje waliohamia Tanzania.
Kwa maana yangu hata sisi tunaopigania uraia wa nchi mbili basi ikija siku ya kupigania kiti cha rais sidhani kama ni vizuri kuwa huru.
 
Bob,

Maneno yako ni sawia, sasa huyu mzee Salim akagombee kwao Zanzibar, huku bongo tunasema hivi huko kwao kwa waarabu wenziwe kwa nini wanamkataaa! Mbona mnataka kututonea sisi tu wabantu huku bongo aende akagombee huko wa-Hizbu wenziwe,

Jamani ninasema hivi kuliko kutawaliwa na mwarabu basi afadhali Mtandao, zimwi tunalolijua!
 
Wana Uchumi,

Na salute wote kwa michango yenye akili....safi sana jamani sometimes inabidi kupongezana ..

Son of dead millionaire,

Vipi zilete mzee tuwagawie wananchi wenye njaa au mzee mwishoni alizitoa kwenda kwenye charity:)
Karibu

FD
 
Hata mimi nilikuwa sitaki kujiingiza kwenye hii mada ya SAS maana tuliizungumizia kwa kina sana kule uchaguzi.com wakati wa kampeni. Lakini mawazo ya ubaguzi yanapojitokeza sana, inabidi nasi tuchangie tena.

Ukiangalia jinsi CCM wanavyotupatia viongozi utagundua kuwa sifa kwa kweli sio jambo la msingi sana. Mara nyingi, kama sio zote, watu wasio na sifa ndio wamepata uongozi mzito na watu wenye sifa zao hutupwa nje haraka sana. Nakumbuka vizuri jinsi Juma Mwapachu alivyochujwa mapema tu katika kugombea ubunge wa Afrika Mashariki dhidi ya mpinzani wake ambaye ilikuja kujulikana baadaye alikuwa na matatizo ya akili. Lakini aliukwaa ubunge wa Afrika Mashariki kwa miaka 6! Wakenya, Waganda waktuuliza: ina maana ilishindikana kupta watu 9 kutoka miongoni mwa Watabzania mamilioni. Ni kutokana na kutokuchangua watu kwa mujibu wa sifa, michango ya wabunge wetu wengi katika Bunge la Afrika Mashariki imepwaya mno na kutoa taswira kuwa Tanzania hakuna watu wenye uwezo.

Kwa sifa za uongozi ni uonevu kumlinganisha Salim na kwa mfano, JK. Hili lilithibitika katika mada iliyochambuliwa kule uchaguzi.com. Fliga angetusaidia kama ange-post baadhi ya mada za kule.

Kumtilia shaka SAS kwa Kigezo cha rangi ni kuthibitisha kiwango cha chini kabisa cha ustaarabu na maendeleo walio nao ccm. Na siamini kama kweli ndio ilikuwa sababu kubwa ya kumkataa. Ila ambacho nina uhakika nacho ni kwamba Mkapa alikuwa hataki mtu yeyote ambaye angemzidi performance. Na alijua mtu kama JK ni uswahili tu, ataishia kubwabwaja, at the end of the day, hamna cha maana cha kushikika.

Malecela, Lowasa wote walikataliwa, tena Malecela mara mbili-hawa wana uarabu gani? CCM kama hawakutaki watatafuta kila sababu. Ubaya ni kwamba sababu wanazotoa siku zote ni zile za kuchafua ubinadamu na utaifa wa mtu.

Sisi sote ni watanzania, tuwakatae watu kwa vigezo vya kisayansi na kistaarabu, sio sababu za kushusha ubinadamu na utanzania wa watu wengine.
 
Mimi binafsi siko tayari kuingia kwenye huu mtego wa kabila, rangi na nasaba!! Kwa sababu sijui ni wapi tutaweka mpaka!!! Je Mchagga Mwizi, Mbadhirifu, na Mkandamizaji ni bora atutawale kwa vile tu yeye ni mtu mweusi na mbantu mwenzetu kuliko kutawaliwa na Chotara wa kiarabu ambaye ni mwajibikaji, anayejali watu, anayezingatia sheria na kiongozi bora? Yaani tumkatae huyo chotara kwa sababu tu yeye ni chotara na tumkubali mchagga kwa sababu yeye ni mbantu mwenzetu!! Kwenye mtego huo sitanasa!! Zimwi likujualo wakati mwingine linakula na kusafisha sahani nzima...!!!
 
Mwanakijiji umesema lakini bado nasema huyu Salim hana sifa za Uongozi .Mimi sitaki kuingia kwanza kwenye rangi yake naomba nipewe uwezo wake wa uongozi na walpi alikuwa kiongozi wa maana akafanya mambo yae ya maana .Hii ndiyo nasema kwamba Salim mbali na uarabu pia si kiongozi hata mara moja na hana sifa za uongozi .

Lakini pia ukweli upo kwamba kwa Uarabu kuongoza watanzania milioni kibao ni dhambi kwa mungu na kufuru mbele ya mababu zetu .Kumbuka Tanzania tulisema hakuna ubaguzo tukawapa akina Bandora madaraka , na Wanyawaranda kibao leo hii wako wapi ? Rangi na Utaifa ndugu ni muhimu kwa Nationa Security .Leo tuna watu wanakimbia Nchi wanajiita Watanzania kumbe ni warundi .Kumbuka Kinana alipopata Uwaziri wa Ulinzi Somalia walifanay sherehe na ndipo wakati huo wasomali wengi waliingia Tanzania .Ushahidi upo kwamba Kinana hakuzaliwa Tanzania ila alikuja kashikiliwa mkono .Leo hii anatuvuruga na ndiye mmoja wa think tank wa CCM lakini ni msomali yuleeeeee.

Nimeona Mugishagwe anauliza juu ya Jamal Amir Marehemu Mhindi yule wa Kitanzania waziri wa fedha na kipenzi cha mwalimu leo kaburi lake TZ liko wapi kama kweli alikuwa Mtanzania wa nia ?? Lazima Dunia imefikia mahali pa kuangalia watu kama akina Keenja kuacha kugombea Ubungo warudi kwao na si kuharibu majimbo na kurudisha nyuma maendeleo ya watu ni mfano huo.Watu wamesema Salim aende agombee kwao Zanzibar tuone kama atapata huko basi nasi tutamfikiria kuna ubaya huo ??

Mwizi wa kichaga hawezi kupewa Nchi landa kwa nguvu za CCM ambao najua hawako tayari kuachia Nchi hata kama watashindwa lakini bado tunasema Tanzania inahitaji kiongozi Mzawa si wakuja , anaye jali na anayeijua Tanzania na kuwa na Uchungu na kizazi hiki na kijacho .Nadhani tuwe wazi tuongee yote halafu tutafute suluhu badala ya kusema huingii katika mtego na unaua issue baadaye tunaanza kujuta .Tuongee hapa kwa uwazi .
 
Mzee Mwanakijiji said:
.......awe mhindi, mchagga, mzungu, msukuma n.k na kama sera zake nakubaliana nazo basi huyo nitampigia kura!!! RANGI, KABILA, au NASABA ya mtu iwe MWIKO!!!!! As a matter of fact, ninasema chama chochote kinachohoji rangi ya mtu kwenye uongozi chama hicho kifutwe au kiongozi huyo avuliwe madaraka!!!

Pokea mkono mwana Kijiji, pia Ahsante kwa maelezo safi na ambayo hayahitaji kuongezewa kitu.

Ubaguzi ndo ambao umesababisha rwanda na burundi mamilioni wakachinjana kwa mapanga, Uganda wanaisikia amani bombani tu, somalia tunaiona je, kwanini tuendekeze ubaguzi hapa nchini? Kama SAS ana kasoro nyingine nakubali hafai kuwa kiongozi, ila kama kasoro yake ni uarabu hapo kamwe sitakubaliana na kigezo hicho. Kwa bahati nzuri humuhumu wengine weshaonyesha mashaka yao ya baadhi ya makabili huu wote ni ubaguzi na ukabila ambao kwa taifa letu utakuja kutuletea madhara na kuturudisha nyuma sana.

Mengi yameongelewa na siwezi kuongeza ila nitakubaliana na yeyote ambaye atafuata hiyo mising aliyointoa mwana kijiji.
 
Jamani maneno mengi ya siasa na haki za binadamu, ndio bongo siku zote mineno mingi lakini on this one yaani Salim hapana wote tuna macho ya kuona kuwa hatufanani naye sio mwenzetu huyu!,

Enzi za Mwalimu tulikuwa tunaogopa kusema sasa tuna nafasi ndio tulianzia Dodoma kumpa ukweli kuwa mzee si mwenzetu,

Now guys ni kweli we can talk back and forth it good for the forum, lakini huu ukweli ambao hatuhitaji kuambiwa ni vigumu kuukwepa, hapa hata siasa na usawa wa binadamu unafika mwisho, Dodoma alikataliwa kwa sababu tu ya uarabu wake sio siri, na pia ukiwauliza viongozi waliohusika watakwambia maneno ya uongo,

Suala la ubaguzi ni la damu na always wote huwa tunahusika in one way or another, ni natural sio masuala ya kujifunza siku zote binadamu tunataka kuwa karibu na tunaofanana nao, nyinyi kina Choveki na wenzako mwisho mtatuletea mambo ya ndoa za mashoga maana mna maneno mengi ya progress na ndiko mnakoelekea, mambo mengine ni kuyaacha tu kama yalivyo sisi ni weusi na waarabu ni tofauti hata tabia zetu hazifananani, hapa hamna siasa wala lecture ni mwisho wa yote, kila mtu aende kwao, na kwenye urais wa nchi yetu hatuwezi kuwa compromise kwani hata huko majuu tunajua walivyowakali inapokuja kwenye urais msituponze na hizo siasa zenu za nje nyingiiiiiii!
 
Mzee Es said:
Jamani maneno mengi ya siasa na haki za binadamu, ndio bongo siku zote mineno mingi lakini on this one yaani Salim hapana wote tuna macho ya kuona kuwa hatufanani naye sio mwenzetu huyu!,............nyinyi kina Choveki na wenzako mwisho mtatuletea mambo ya ndoa za mashoga maana mna maneno mengi ya progress na ndiko mnakoelekea, .........weusi na waarabu ni tofauti ...... hapa hamna siasa wala lecture ni mwisho wa yote, kila mtu aende kwao, na kwenye urais wa nchi yetu hatuwezi kuwa compromise kwani hata huko majuu tunajua walivyowakali inapokuja kwenye urais msituponze na hizo siasa zenu za nje nyingiiiiiii!

Mheshimiwa ES na wana bodi wengine,

Hapa nadhani tunajaribu kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya uongozi m bovu ambao miaka 45 baada ya uhuru kipindupindu bado kinaua watu Dar, huko vijijini wala usiseme ndo hata rekodi au takwimu hakuna! Eti mika 45 ya Uhuru bado mama na dada zetu wanatembea maili kadhaa kufuata maji, miaka 45 ya uhuru mtanzania anamuuzia mtanzania mwenzake nyama ya mbwa akidanganya kuwa ni ya swala nk......Swali ni kuwa je tunaenda mbele au tunarudi nyuma??? Bado tunaambiwa eti mtu amefeli darasa la saba kwa hivyo yeye basi...na anaishia la saba, je mtanzania huyu si kama anahukumiwa kifo cha polepole? (hii ni zaidi ya asilimia 80 ya vijana wetu) Miaka 45 baada ya uhuru hakuna kiongozi anayeamini hospitali au daktari mtanzania mwenzake hivyo hata check up tu (siyo matibabu) inabidi aende majuu. Je ni tusi lilioje kwa hospitali au madaktari wetu?? Miaka 45 baada ya uhuru kila mtu inabidi akimbilie Dar kwani kila kitu ni Dar!!

Halafu tunaendelea kuambiana ati lazima mgombea urais awe mweusi ndiyo akubalike. Ukiangalia na kuchunguza utaona kwamba wanaoinadi nchi wala hawana uchungu nayo je kwanini watudanganye wakati wanataka kura zetu.

Siyo kama tunaleta viswahili au siasa nyingi bali tunaangalia tatizo la nchi yetu kutoka kona tofauti na yenu mnayoangalia...Nakubali tuna maneno ya progress yote ni kwa ajili ya kusaidia watanzania wote wa mijini na vijijini bila kujali jina la baba, mama, pesa, kabila au rangi ya huyo mtanzania....Mnajua kuwa hata wakati watu walipoanza kudai uhuru wapo waliokataa wakiamini kuwa lazima nchi itawaliwe na wazungu tu, sasa basi sasa kibao inabidi kigeuke, siyo lazima kiongozi wa nchi awe mweusi, umuhimu ni kuwa lazima awe mtanzania tu.

Nitamalizia kwa kusema hivi hata Watutsi walisema vivyo hivyo..."...hawa wahutu si wenzetu na ni tofauti nasisi na hatuwezi kuishi nao nchi moja..."
 
Wanabodi jamani mweee!
Issue hapa ilikuwa JK hatimaye kafanya mavitu! leo tumegeuza mchezo mzima na kuwa Salim.
Sote kwa pamoja tunaelewa nini kimefanyika kutokana na makosa yetu wenyewe.
1. Ni kweli hakuna nchi ambayo inaweza kumpa Urais mtu mwenye asili ya nje. Vyeo vingine vyote wanaweza kupewa lakini sio rais na katiba zao zimefafanua. Myahudi, Mchina ama Mwarabu hawezi kupigania urais Marekani hata kama wazazi wake wote ni Wamarekani kwa uraia.
2. Tofauti na nchi nyingine, Tanzania tumeruhusu kikatiba kuwa na watawala wenye asili ya nje kikatiba, hii imetokana na historia yetu.
3. Kisiwa cha Pemba ambacho ni sehemu ya Tanzania kina asilimia kubwa ya waarabu -Wa -Oman kwa hiyo tunapomkataa Salim ina maana tunaukataa muungano.
4. Hakuna kati yetu anayeweza kusema ukweli nani Mtanzania halisi! Asili ya Wazaramo wali-immigrate kutoka Kenya miaka hiyo ya utawala wa Sultan hali waarabu walikuwepo tayari Bandari salama. Je, wazaramo pia hawaruhusiwi kuwa marais?... kama ni rangi je, mnamkubali M7 kuliko Salim.
Tamaduni na mila zetu tofauti na nchi nyingine. Hatuna lugha wala kabila dominant. Kiswahili kama moja ya tamaduni yetu haina tafsiri kwa rangi. Tusiyatumie mazingira ya nchi nyingine kuwa mfano wetu. Huyo Salim hata kwa kiapo hawezi kukubalika kwa waarabu kama first citizen,yamewakuta Wazanzibar kibao waliokimbilia Oman miaka ya sabini. Walipewa uraia wa pili na kuwekwa ktk kambi kama wahindi wekundu huko Marekani..wanajulikana kama Zenjibari! -Yaani watu weusi, hali watu hawa waarabu!
Salim:- Ni juhudi za Salim akiwa mwakilishi wetu Umoja wa mataifa, South Africa iliwekewa vikwazo.
Ni juhudi za Salim akiwa balozi China tuliweza kuijenga reli ya Zambia.
Kuwa kiongozii wa OAU sio kazi ndogo, sioni kiongozi mwingine zaidi yake toka tanzania ambaye angeweza kupita nafasi hiyo. It's a gift to the nation.
Jamani turudi kwa JK, panishment aloipata Salim ktk uchaguzi inamtosha - kwani hatarudia makosa - Shukran ya punda ni mateke.
 
Hii Habari baada ya kuisoma nimeona ni vema . Tupige kelele
ili chama cha CCM kiwangalie matajiri wake kwa macho mawili!!

Na siyo tu kukimbilia michango yao mikubwa at the expense of our people being killed!!

Lengo ni kuhamasisha JK na wana CCM wengine kusafisha chama!
Ili konokono watoke! Nia aibu kwa chama kikubwa kama CCM kukubali kupokea majambazi kuwa viongozi wao simply tu kwa TAMAA YA KUCHANGIWA HELA TENA WAKATI WA UCHAGUZI! HILI LISIKALIWE KIMYA WALIJADILI KWENYE KIAKO CHAO CHA JUNI 2006. NIMEANZA KUFARIJIKA KUWA YALIYOSEMWA KUHUSU WABUNGE WALIOGUSHI VYETI WAMEANZA KUFUATILIWA!
LABDA NI WAKATI MUAFAKA HIYO TOPIC IFUFULIWE(ILIKUWA HOT TOPIC BCSTIMES). LEO NIMESIKIA KUWA WATATU TAYARI WAMEHOJIWA NA DCI NA WOTE NI WA CCM.


HABARI KUHUSU TAJIRI JAMBAZI NI HII

Imetolewa mara ya mwisho: 02.06.2006 0947 EAT

•
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya kizimbani akituhumiwa ujambazi

sogeza Habari Zinazoshabihiana
• Mwenyekiti CCM Wilaya atuhumiwa kwa ujambazi 30.05.2006 [Soma]
• Mfanyabiashara wa Arusha kizimbani akidaiwa kutapeli 19.05.2006 [Soma]
• 'War Bus', wenzake wakamatwa Arusha 24.04.2006 [Soma]

*Asomewa mashitaka tisa ya wizi wa magari, silaha
*Ni mfanyabiashara anayemiliki kiwanda cha samaki
*Nako Dar kesi ya Askofu wa Marekani yanguruma

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa CCM wa Wilaya ya Musoma Mjini, Bw. Joseph Obeto, amefikishwa kizimbani kwa tuhuma za ujambazi ikiwamo kukutwa na magari ya wizi, silaha na risasi.

Mwenyekiti huyo alifikishwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Musoma, ambapo alisomewa mashitaka tisa.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Bw. Kapita Mwaruka, mtuhumiwa huyo alisomewa mashitaka tisa yakiwamo ya kukutwa na magari ya wizi na kughushi hati za magari.

Pia mashitaka mengine aliyosomewa ni kukutwa na risasi kubwa tofauti na bastola aliyokutwa nayo, hivyo kuashiria risasi hizo zilikuwa ni kwa ajili ya matumizi mengine.

Bw. Obeto ambaye pia ni mfanyabiashara anayemiliki magari na kampuni ya KOTRA, alijisalimisha katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Musoma mwanzoni mwa wiki hii, baada ya Polisi kumtafuta.

Naye Grace Michael, anaripoti kuwa shahidi wa kwanza wa upande wa mashitaka katika kesi ya kujipatia zaidi ya dola za Marekani milioni mbili kwa udanganyifu kupitia jina la Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Bw. Jimmy Julius (45) ameieleza mahakama jinsi watoto yatima na wajane walivyokesha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, wakisubiri msaada kutoka Marekani.

Ushahidi huo ulitolewa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Bi. Euphemia Mingi. Mshitakiwa katika kesi hiyo ni Askofu wa Kanisa moja la Marekani, Bw. Peter Mutafungwa.

Ilidaiwa kuwa wajane, watoto yatima waliokuwa uwanja wa ndege siku hiyo walikuwa wakisubiri msaada wa tani 360 za chakula, viatu, dawa na dola za Marekani 2,250,000 kutoka kwa mshitakiwa huyo.

Bw. Julius ambaye ni Mwenyekiti wa Shirika la Jamii linajishughulisha na kutoa misaada kwa watoto yatima, wajane na wasiojiweza, alidai waliahidiwa kupewa msaada na shirika la Children Pastors International, lililoko Marekani kupitia Taasisi ya Mwalimu Nyerere.

Alidai kuwa baada ya kuambiwa kuna msaada huo walipewa maelekezo na Bi. Angela Chaila ambaye ni Mwandaaji Mipango wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, kuwa wanatakiwa kutafuta kibali cha msamaha wa kodi ili msaada huo uweze kuletwa nchini.

Bw. Julius alidai mahakamani, kuwa walifanikiwa kupata kibali hicho ambacho walipewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baada ya kutuma kibali hicho, Bw. Mutafungwa alidai kimechelewa, hivyo aliwataka wakate tiketi ya ndege kwenda Marekani na kurudi, ili aweze kuleta msaada huo.

Baada ya kupata ujumbe huo, waliamua kwenda kuchukua mkopo katika Benki ya Akiba wa sh. milioni moja na kuwachangisha wajane na watoto yatima sh. 600,050 ambazo walizitumia kwa kukata tiketi ya Bw. Mutafungwa, ambaye alitakiwa kuwasili nchini Septemba 30, mwaka juzi ambapo aliahidi kuwa atalipa gharama hizo baada ya kufika Dar es Salaam.

Alidai kuwa siku hiyo ilipofika, yeye na vikundi mbalimbali vya utamaduni, watoto yatima, wapiga picha na wajane, walikwenda uwanja wa ndege kwa ajili ya kumpokea Bw. Mutafungwa, ambaye aliwasili saa 6 usiku, na baada ya kumpokea, alisomewa risala na kuchezewa ngoma na waliambulia kukumbatiwa, na hakuwa na kitu chochote alichokuja nacho kama alivyokuwa ameahidi.

Bw. Julius alidai baada ya kumpeleka kwenye nyumba waliyokuwa wamemwandalia, walimwacha apumzike na aliwaomba kuwa fedha hizo angezilipa Oktoba 2, mwaka juzi, lakini hakuweza kufanya hivyo, aliendelea kuwazungusha bila kuwapa misaada kama alivyotakiwa.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kesho mahakamani hapo ambapo upande wa mashitaka utakuwa na shahidi mwingine.
Tuma kwa Rafiki Nakala inayochapika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom