Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Tendwa sasa anywea kwa Chadema
Na Khamis Mkotya
HATIMAYE Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amekubali kukutana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya kuwapo mvutano baina yake na chama hicho.
Hatua hiyo inalenga kumaliza tofauti zilizopo baina ya msajili na chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Jitihada za kutafuta suluhu hiyo inafanywa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Dk. Emanuel Makaidi, ambaye ameingilia kati uhasama huo.
Akizungumza na Mtanzania jijini Dar es Salaam jana, Dk. Makaidi alisema anasikitishwa na uhusiano tete uliopo baina ya vyombo hivyo viwili.
Dk. Makaidi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha NLD, alisema amefungua mlango wa kutafuta suluhu baina ya msajili na chama hicho kwa faida ya taifa.
Chadema ilisitisha uhusiano na ofisi ya msajili na kulazimika kutangaza mgogoro na kiongozi huyo kutokana na kuchukizwa na kauli yake ya kutishia kukifuta chama hicho.
Msajili alitishia kufanya hivyo kwa madai kuwa chama hicho ndicho kilichosababisha mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel tena, Daud Mwangosi.
Dk. Makaidi alisema licha ya kuanzisha jitihada hizo kwa muda sasa, lakini jitihada zake zimegonga mwamba baada ya kushindwa kukutana na viongozi wa juu wa Chadema.
Dk. Makaidi alisema uwamuzi wa kutafuta suluhu hiyo ulifikiwa katika mkutano wa wadau wa siasa ulioitishwa hivi karibuni na Tendwa, ambapo Chadema haikuhudhuria.
"Chadema na msajili wa vyama wote ni wadau wa siasa, kwa hivyo misimamo yao hii ikiendelea itakuwa haina tija kwa taifa zaidi ya kuendeleza chuki na uhasama.
"Chadema kususia shughuli za mtu aliyewasajili, hii si sawa na pia msajili kutishia kukifuta chama tena chama kikuu cha upinzani alichokisajili mwenyewe pia nayo si sawa.
"Kwa kutambua hilo, ndipo tunapotafuta suluhu. Tunataka wakutane wazungumze na kujadili waone namna ya kumaliza tofauti zao badala ya kila mmoja kubaki na msimamo wake.
"Pamoja na kwamba nimeshindwa kukutana na viongozi wa Chadema, lakini nataka wananchi wajue zipo jitihada zinazofanywa za kurejesha wao," alisema.
Hata hivyo Dk. Makaidi alisema tayari msajili huyo amekwisharidhia kukutana na viongozi wa chama hicho ili kumaliza tofauti zao, baada ya kufanyika kazi kubwa.
"Oktoba 16 nilikwenda kwa msajili, pamoja na kumweleza kushindwa kwangu kukutana na viongozi wa Chadema, nilimwomba msajili afanye kila analoweza akutane na viongozi wa Chadema.
"Awali msajili alipinga wazo langu akisema kuwa atawezaje kuwaita watu ambao hawamtambui. Lakini nafurahi baada ya ushawishi mkubwa hatimaye msajili alikubali.
"Wapo watu wanaoweza kubeza na wengine wakaona kama Chadema wanabembelezwa. Hapana, katika hali kama hii ni vigumu kuiepuka Chadema katika mazungumzo.
"Kwanza Chadema ndiyo official opposition (kambi rasmi ya upinzani) bungeni. Pia ni chama kikuu cha upinzani nchini, hakuna namna ya kuikwepa.
"Napenda kutumia fursa hii kuwaomba viongozi wa Chadema wakiitwa na msajili wakubali ombi la msajili ili kumaliza tofauti zilizopo. Kuendelea kubaki na msimamo haitusaidii kama taifa," alisema.
Akizungumza na Mtanzania kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sasa.
Mnyika alisema chama chake kilikwishapeleka barua Ikulu kulalamika namna kinavyohujumiwa na kueleza kuwa wanachosubiri kwa sasa ni majibu ya barua hiyo na si vinginevyo.
Source: Mtanzania