Hatimaye Jerry Muro ashinda kesi yake

Nadhani atarudi kazini na kendelea na kile kipindi chake ili kupigana na rushwa. Asiogope aendelee na vita ile aliyoianza.


TBC walishasitisha ajira yake siku nyingi mkuu! Baada ya TIDO kuondoka naye inasemekana walimfutilia mbali.
 
Mtu anaomba rushwa, anakamatwa na wala rushwa, uchunguzi unafanywa na wala rushwa, ushahidi unatolewa na wala rushwa, mwendesha mashtaka mla rushwa na hakimu mla rushwa pia. Mnatarajia hukumu iweje hapo?
 
Ameachiwa achiwaje? vipi tuhuma dhidi yake,zilipikwa? Na nani,na kwa sababu gani...vipi jina lake baada ya muda wote huo wa kupakana matope....naomba ufafanuzi kidogo hapa!


Tumpe muda apumue then kusafisha jina atajua yeye lakini nadhani baada ya kupata nakala ya hukumu .
 
hatimaye Mwandish wa habari Jeri Muro ameachiwa huru.mwandishi huyo aliyekuwa anafanya kazi TBC alikuwa anakabiliwa na kesi ya kudai rushwa...

Mara zote haki uwa haipotei bali inacheleweshwa tu....naamini kwa hili la Jerry Muro ni fundisho kwa watawala wetu wanatamani kila siku kukandamiza haki za watu waosema ukweli..naamini Mungu amewaaibisha watu waliokuwa hawamtakii mema Jerry..kwa upande mwingine naomba Murro arudi kwa nguvu zaidi kwenye kazi yake na kwenye habari zake za uchunguzi..ila asirudi TBC1 nadhani pale sio mahali pa-usalama wake na uhuru wa kufanya kazi zake...Namshukuru Mungu kwa ushindi wa Jerry Muro...ni ushindi wa wenye haki dhidi ya watawala wahuni,wahuaji,watesaji,mafirahuni nk....
 
Kuna ile imani kuwa wanawake wengine ni nuksi, ukioa tu umekwisha! Kwa maana hiyo huyu aliyeolewa na Muro kaleta baraka. Kama ndivyo basi hongereni ma-SHE wote! Naomba niulize, Gerry tutamuona tena TBC au ndo niaje hatima yake kazini?
 
endelea kudhani upo juu ya sheria kuna siku tutawachoma vijiti makalioni kama gadaffi.
kwa akili yako Jerry alikuwa anafanya mchezo mchafu???????????

Ameponea tundu la sindano. Waandishi wa habari wanaomba rushwa sana wasiandike habari fulani. Inawezekana yeye hakufanya hhivyo, lakini it is no wonder kuwa inawezekana aliomba rushwa. Wanafanya hivyo sana tena sana
 
Sasa hivi itabidi tu awe anafanya kazi za back office. Kuuza sura kwenye TV sasa noo!
 
Obama alikuwa na jibu moja tu kwa wale ambao hawakuamini kuwa Osama amekufa. Obama alisema ' you will never see Osama walking on this planet again'. Mimi nasema ' you will never see Jerry Muro employed again'
Ushindwe na ulegee..kwani wewe ndio Mungu?hata asipoajiriwa Tanzania ataenda kuishi Kenya hawana matatizo na miungu watu wanaodhani watatawala milele.
 
Thanx!God kasikia maombi ya wapenda haki km mi2!
Hongera kaka!
Cha mno waliokuchafua washtakiwe coz 2mekumic sanaaa ucku wa habari ulikuwa unabang mbaya!
 
Sheria za nchi zinasema ukishashtakiwa mahakamani hutakiwi kuajiriwa tena na kampuni yoyote ile. Huyu Jerry Murro imekula kwake moja kwa moja.


Mkuu kama kuna sheria inayosema hivyo ni batili na inatakiwa kufutwa mara moja. Kwasababu wabaya wako wanaweza kukuzushia kesi na kukupeleka mahakamani ili upoteze kazi na mwisho wa siku ushinde kesi wakati kazi ishapotea!

Nafikiri sheria itakuwa inaongelea ukisha hukumiwa na kukutwa na kosa!
 
Back
Top Bottom