Hatimaye Fedha za Rada Chakavu (Tsh 29.5 bilion) toka BAE systems zarejeshwa BOT (Tanzania)

BAADA ya vuta nikuvute ya muda mrefu kuhusu kurejeshwa fedha za ziada zilizotumika katika ununuzi wa rada, hatimaye Serikali ya Uingereza imeingiza Sh29.5 bilioni kwenye akaunti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), tawi la Uingereza kama marejesho ya fedha hizo.

Uamuzi huo wa Uingereza kurejesha fedha hizo, unakwenda sambamba na ombi lake la kutaka watuhumiwa wote wa hapa nchini waliohusika na ununuzi wa rada hiyo mtumba kutoka Kampuni ya BAE Systems, washitakiwe Tanzania au Uingereza baada ya kubainika dosari kwenye ununuzi huo ambao kama ungefanyika kihalali ungehitaji Pauni 10.5 milioni, kununua rada mpya. Akizungumza na gazeti katika mahojiano maalumu jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Fedha, Mustapha Mkulo, alisema fedha hizo tayari zimekabidhiwa kwa tawi hilo la BoT nchini Uingereza ili ziweze kurejeshwa nchini.

Mtazamo wangu

Kabla ya ununuzi wa hii Rada wachunguzi wa mambo ya kijamii walishaona dalili ya ufisadi, Serikali ikapigiwa kelele na wazalendo na hata watu wa nje wanaoitakia mema nchi yetu kuwa serikali isinunue hii Rada, lakin serikali ilisema kuwa Rada hii ni muhimu sana katika ulinzi wa Anga la Tanzania. Rada ikanunuliwa kifisadi na kibabe, mbaya zaidi, ule umuhimu wa Rada hii katika usalama wa hauonekani, kwani Juzi juzi tu Ndege ya kijeshi ya Qatar ilitua kiwanja cha kimataifa (KIA) ikasomba wanyamapori wetu na kuondoka bila Rada hii chakavu kudetect utuaji na uondokaji wa ndege hiyo. Sasa hapo KIA Rada imeshindwa kudetect, je Rada hii itaweza kudetect ndege zinazotua Loliondo, Mugumu, Nyarugusu, Nyamongo etc??? Hii inaonyesha kuwa ununuzi wa hii Rada haukuwa kwa maslahi ya Taifa bali ilikuwa ni kuingizana mkenge tu ili wezi wachache wanufaike. Kwa kweli huitaji tochi kumulika mwizi katika sakata hili la Rada.

Ningetegemea baada ya tukio hili JK, Pinda, Werema, Hosea, Feleshi na wale wataalum wetu wa Intellegensia (Kova na Mwema) wote kwa pamoja wahakikishe wezi wote waliowezesha wizi huu kutokea wanashughulikiwa. Lakini cha ajabu utaona jinsi ambavyo viongozi hawa walivyokosa uzalendo na jinsi walivyo wasaliti kwa Taifa, watajifanya wahajui kilichotokea na watajifanya kutekeleza agizo la Uingereza la kuitaka Serikali ya Tanzania ishitaki hao wezi wa Rada ni kukubali Ukoloni Mamboleo.

Cha ajabu viongozi hawa hawa ndiyo wale ambao wapo mstari wa mbele kuitetea Dowans ilipwe kwa kigezo cha utawala wa Sheria, ninatarajia katika sakata la wizi huu wa Rada, viongozi hawa wawe pia mstari wa mbele katika kuhimiza utawala wa sheria na wahakikishe sheria inachukua mkondo wake kwa wezi wote walohusika katika wizi huu. Hakika hiki ni kipimo kingine kwa Serikali ya CCM ambayo hadi sasa inasifika kwa kulinda mafisadi. Nini maoni yako juu ya suala hili????

Source. Mwananchi 06/12/2011

Hapa dawa ya haya mambo ni kuandamana tu kama tukiona
hawa jamaa hawaelewi ni kuwa wakali kwani huu ni upuuzi
mtupu Clear shot alijitahidi sana kulizuia suala hili akiwa na
Cameroon lakini wapi.
 
Cha ajabu kuna waziri 1 mjinga anasema eti..waingereza wenyewe mbona hawajawashtaki wahusika wa kwao, inakuwaje watulazimishe sisi (TZ) tuwashtaki wa kwetu? Hii ni kauli ya waziri wa TZ, inakera sana!
 
Kwenye hoja za msingi kama hizi ni nadra sana kukutana na wale MACD+Kina Elton JOhn=FF, Rejao, Topical, na wenzao wengine(wanajijua). Anzisha taarabu na hoja za chuki binafsi za kumsema mtu wao au amabye sio mtu wao utaona wanavotoa povu kwa kutumia bongo zao za mende!
 
BoT tawi la Uingereza??????sijaelewa kama BoT wana matawi nje ya nchi au wana akaunti kwenye benki za nje ya nchi? Waandishi wa habari tafitini vizuri kabla ya kuandika msije onekana kuwa nyie ni zao la shule za kata
Nadhani alimaanisha hizo fedha za zimeingizwa kwenye account ya BOT iliyopo Uingereza.
 
Hapa dawa ya haya mambo ni kuandamana tu kama tukiona hawa jamaa hawaelewi ni kuwa wakali kwani huu ni upuuzi mtupu Clear shot alijitahidi sana kulizuia suala hili akiwa na Cameroon lakini wapi.
Tatizo letu bado tu waoga sana hata kwenye kufwatilia mambo yenye maslahi kitaifa. Huu uoga ndio unaotumiwa na wezi wa CCM kila mara ktk kufanikisha wizi. Kama tungekuwa wakali, wangeacha huu wizi wa aina hii.
 
Kwa kweli inauma. Hivi kweli hawa wangereza wana siri gani na serikali ya Tanzania. Tulishawaandikia email kwamba hatutaki hizi hela za watanzania zipitie mikono ile ile iliyozitapanya mwanzo. Kitendo cha wangereza kuzirudisha kupitia serikali hii hii, majambazi haya haya, ni kutudharau sisi watanzania wa kawaida.
 
Waziri (Chikawe)wa utawala bora amekuwa mtetezi namba moja wa watuhumiwa hawa,Mawaziri kama hawa hawatufai,Ningekuwa na mamlaka ningemfuta kazi mara moja
 
Cha ajabu kuna waziri 1 mjinga anasema eti..waingereza wenyewe mbona hawajawashtaki wahusika wa kwao, inakuwaje watulazimishe sisi (TZ) tuwashtaki wa kwetu? Hii ni kauli ya waziri wa TZ, inakera sana!

WAZIRI CHIKAWE,'unaogopa kumtaja watakupa sumu'
 
kumbe tungepata radar mpya 2 au 3 kama tungeomba punguzo kwa kuwa tuna purchase nyingi....sasa wakati huo sheria ilikuwa hairuhusu vitu chakavu ,,,itakuwaje sasa imepitishwa hii ya used ,,,,kaazi kweli 50 yrs halafu bila aibu wanakaa wanajisifu najuta kuwa na ccm tz
 
Kwenye hoja za msingi kama hizi ni nadra sana kukutana na wale MACD+Kina Elton JOhn=FF, Rejao, Topical, na wenzao wengine(wanajijua). Anzisha taarabu na hoja za chuki binafsi za kumsema mtu wao au amabye sio mtu wao utaona wanavotoa povu kwa kutumia bongo zao za mende!


Na wewe kweli unajiita Great Thinker?

Pole sana . Wewe weka hoja si kutusi member wengine. Kumbuka kuwa kila mtu ana haki kamili kuchangia chochote kile kwene mada yoyote ile ilimuradi tu asivunje sheria za JF. Kumbuka kizuri kwako basi ni kibaya kwa mwenzio.

Punguza jazba na chuki na lete hoja na mchango wako wa mawazo kuhusu mada husika.
 
Ikumbukwe hoja ya fedha za rada iliibuliwa bungeni na wabunge wa upinzani hasa chdm!huu ni ushindi mkubwa na sifa nzuri kwa wanaharakati wapenda maendeleo na aibu kwa wahujumi uchumi(ccm)
 
this is too much umefika wakati sasa watanzania ni lazima wachukue hatua juu ya mustakabali wa nchi yao kwa sababu waliowakabidhi mali kuilinda wanashirikiana wa wezi kuwaibia.
 
Dah! Pesa zimekuja,sasa watu watalipwa mishahara ya desemba mapema ili christmass iwe nzuri
 
Back
Top Bottom